Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Hii ni Falacy of Generalization. Sio Wanasayansi wote wanakataa uwepo Wa Mungu. Tuwe makini na Hearsay.
uwe unasoma kwa makini mkuu, itakusaidia kujibu majibu sahihi kwa kile unachokiquote.
'' hapo nimekuwa specific kwa wanasayansi wasio amini Mungu'' Sijasema wanasayansi wote hawaamini Mungu Tangu comment ya kwanza.
 
Mkuu ni kweli na nakubaliana na wewe kuwa sitakiwi kuwa lateral kwenye kila kitu cha kwenye bibilia, Ila nakubaliana na kuwa Rateral kwenye mambo ambayo ni rateral katika bibilia na Yamethibitika kuwa lateral kwenye Bibilia.
Ungeonyesha madhaifu ya hiyo kutoka20 kwa nini sio lateral ili namimi nionyeshe kuwa ni lateral tuchanganua vizuri zaidi.

Binafsi naamini.
Matukio ya Mwanzo sio mafumbo au mambo ya kufikilika ni historia halisi. Yesu aliamini hivyo Mitume waliamini hivyo. Katikati ya Historia hiyo kunaweza Kuwa na Matukio ya Njozi, na mengine ya Mifano. Ila Hili la Uumbaji ikiwa Muhusika amelitolea ufafanuzi sioni haja ya kulazimisha usayansi, au kuliforce tukio linyenyekee wanasayansi hata kama Mungu amefafanua.
 

Baada ya uthibitisho wa Ellen kwenda Mbinguni bila kufa kwanza na huko kuona Amri ya sabato imezingirwa na "utukufu?"
 
1: Bibilia imeweka msingi wa Kila kitu hiyo ndiyo point yangu kuu katika maelezo niliyokupa. Imeweka facts za Milele ambazo uvumbuzi wowote wa kisayansi unajengwa juu yake, na haziyumbishwi na wasanasayansi na mavumbuzi yao. Na kuyumba kwa wanasayansi hakuwezi kuziyumbisha zitadumu milele hata kama zikiaminiwa na watu wawili tu dunia nzima.

Miongoni mwa facts kuu hizo au naziita evalasting principles au formula
* Mungu ndiye Muumbaji. Hili Litabaki hivyo hata dunia ikatae.
*Mungu aliyemuumbaji, Anapaswa kuaminika kwa Kauli zake mwenyewe kuliko Kauli za Kiumbwaji.
*Wanasayansi wanajaribu kuchunguza kazi za Mungu za Uumbaji, Uchunguzi huo unaweza kupelekea kuvumbua ukweli wa kazi zake au Kupotosha ukweli huo. Katika Hili Kilichosemwa wazi kwenye Maandiko Matakatifu ndio Basis ya Ukweli huo.
*Sayansi inamipaka, ya ufahamu na uelewa Juu ya Kazi nzuri ya Mungu.
Bibilia haijatoa kila formula ya kisayansi na sijasema hayo maana haijazungumzia hata pai. Ila inatoa msingi au general formula za kumsaidia Mcha Mungu asivurugwe na kuchanganyikiwa na chochote kutoka kwa Mwanasayansi haramu au Halali.

####
Lengo la Bibilia ni nini?
'' Kwa Maana Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanaye wa pekee, ili kila amuaminie asipotee bali awe na Uzima wa Milele'' Yohana 3:16
Kwangu mimi hili ndio lengo na dhumuni kuu la Maandiko Matakatifu. Ukombozi wa Mwanadamu. Ndio maana Yesu mwenyewe alisema Maandiko Yote yanamuelezea Yeye. Hata Hiyo Mwanzo ni Yeye ndiye Muhusika wa uumbaji.
Lakini pia Bibilia inasema '' Neno Lako ndiyo taa ya Miguu yangu na mwanga wa njia yangu''. Nje ya Bibilia utatembea gizani, na Kila kilichonje ya Bibilia ikiwa kitakizana na Ukweli mkuu wa Bibilia ni GIZA.
Bibilia inatufanya Tusewe watoto wachanga tena, Tukitupwa huku na kule na Kila upepo wa Elimu na mafunzo.

Pili
Sijasema Popote Kuwa Bibilia ikikusudia Kufundisha Sayansi, Bali Nimesema na nasema Bibilia ni Kitabu sahihi Kilichoweka kanuni/Formula na Misingi zinazoweza Kumsaidia Mwanadamu Asipotoshwe na Sayansi Potoshi na Awe Bora na Imani Yake kwa Mungu Ikue kwa Mavumbuzi na sayansi Sahihi.
Lakini Kusema hili Haimaanishi hakuna tips katika Bibilia ambazo ni scientifically correct, maana Bibilia imegusia vitu kama Rain formation Mungu akimthibitishia Ayubu Kuwa Yeye ndiye fundi wa hizo mifumo, Dunia duara kama mdau Kituko kazungumzia na tips kadhaa ila sio lengo kuu la Bibilia Maana Yote hayo hayatakuwa na Maana kama ukayajua na ukachepuka kwenye Lengo Kuu Wokovu wa Mwanadamu Kupita Kristo Yesu.

tatu
Hatujifunzi Sayansi Kutokea Kwenye Bibilia. Ila kama nilivyoonyesha Huko Juu Bibilia Ni nanga ambayo itamsaidia anayeiamini asiyumbishwe na tafiti potoshi au sahihi za Kisayansi. Mfano wa Tafiti Potoshi kwa Imani Yangu ni kudanganya watu Dunia imeumbwa miaka mamilioni Kisa Sayansi imesema Imegundua huku Bibilia Imeliweka wazi Kuwa ni Siku sita ambazo kwa Genealogy za watu wa Bibilia hatufikishi huko wanakozungumiza. Pia Basis na assumptions wa hizo observation ni kanusho la kazi njema ya Mungu aliyoweka msingi wa Kuikumbuka kupitia Sabato ambayo Yesu anasema waliwekewa wanadamu ili wakumbuke hilo zoezi ingawa mabillioni hawaoni umuhimu wa kufanya hilo.

nne
Pamoja na Kazi njema ya Ukombozi ambayo ndiyo msingi wa Bibilia, Imekusudiwa kuzuia upotoshaji wote wa kisayansi, kiphilosophia, Modernism, historia, elimu etc. Na Inatutaka Kuweke kando Kila fikra ijiinuayo KINYUME NA ELIMU YA MUNGU bila kujali inatoka kwa prof,scientist,padri,mchungaji hata Malaika.

SAYANSI NA AKILI ALIZOTUPA MUNGU.
Bibilia inasema '' Moyo (Human Mind) ni mdanganyifu na Unaugonjwa wa Kufisha, ni nani awezae Kuujua? Yeremia 17:9
Hii tu, inatosha kuendea tafiti za Kisayansi na Kisomi kitaaluma kwa utulivu huku tukiwa na taadhari kwa sababu zimefanyika kwa sababu zao na watu wa kawaida wenye ubinadamu uliofungamana na dhambi wanaweza kuja na hitimisho potoshi au sahihi, Danganyifu au Lenye muelekeo sahihi.
Mfano: Utasimama upande upi katika jambo ambalo hata wanasayansi wanapingana japo ni tokeo la akili hizo Mungu alizotupatia?
Utayaacha katika viwango Vya Nadharia tu au assumptions hata kama zinaungwa na dunia nzima haimaanishi ni Kweli. Sio mimi tu nasema haya hata galileo alisema ''
KATIKA SAYANSI MAMLAKA YA MAONI YA WATU ELFU MOJA, YANAWEZA YASIWE NA THAMANI SAWA NA FIKRA YA MTU MMOJA ''.

HITIMISHO.
Sipingi Sayansi, Ila siungi mkono Kila kitu katika Sayansi kama Fact. Kwanza hata wenyewe huwa wanaziita NI NADHARIA. Ila Kauli za Mungu sio NADHARIA. Kwa nini Sayansi unaona kama naijadili kwa Kutumia Bibilia japo Bibilia ijazungumzia UKOMBOZI. Sayansi ya Sasa Inafunua Pazia na Kuingia Kwenye mambo ya Imani na Bibilia Na Kuanza kuyatafsri na Kuyatolea Matamko. Mfano hata hili La Uumbaji na Umri wa Duñia. Ninaona ni Heshima Kubwa mno Kusimama na Kauli ya Mungu na Kuweka kando nadhalia zote katika hili. Hii hainifanyi nizichukie. Mimi nimesoma sayansi japo kwa kupapasa hadi elimu ya juu ya awali, hata nikiamua kutafuta PHD ya Geology nitasoma hayo yote ya mamilioni ya miaka kama nadharia ila fact ni Kauli ya Mungu kuwa Dunia Iliumbwa Siku sita Ya Saba akapumzika. Hakuwaandikia wasomi wa theolojia aliwaandikia wakina mama na wababa waliotoka utumwani, masikini wasio na elimu, akaagiza watoto wajulishwe katika hilo nimechagua kuelewa kama hao walioandikiwa na kuambiwa Wasiyaache maana hiyo ndiyo akili yao na ufahamu wao.

mkuu nimeandika maneno mengi ili kuchambua kwa kirefu kidogo maana inainekana hunielewi vizuri naamini nini na siamini nini.
 
Utofauti lazima utakuwepo kwa sababu Bible inafanya hesabu kuumbwa kwa Adam ndo mahesabu yameanzia hapo wakati science inapima miamba. Ikumbukwe kwenye Bible binadamu ndo wa mwisho kuumbwa na mchakato wa uumbaji ulikuwa wa miaka mingi sana.
 
sio Kweli.
Kabla ya Gregory Calender kuwepo Siku ya Kuanza Jioni hadi Jioni ambayo inahitimisha masaa Ishirini na nne ilikuwepo.
Ni Mungu aliyeumba Dunia na Vyote Vilivyomo aliyesema Alifanya YOTE sio baadhi Ndani ya Siku sita.
Na Alipozungumzia hilo, alisema literally kuwa Siku sita alifanya Yote kwa Kutamka.
Unadhani Mungu anahitaji miaka Millioni ngapi Kusema Neno Likawawa Mwamba???
Huku ni Kumshushia Heshima Mwenye enzi.
 
Utofauti lazima utakuwepo kwa sababu Bible inafanya hesabu kuumbwa kwa Adam ndo mahesabu yameanzia hapo wakati science inapima miamba. Ikumbukwe kwenye Bible binadamu ndo wa mwisho kuumbwa na mchakato wa uumbaji ulikuwa wa miaka mingi sana.
Hesabu ya bibilia inakamilikia Kuumbwa kwa adamu, haianzii kuumbwa Kwa Adamu.
na Ilikuwa ni SIKU ya Sita ya Uumbaji.
Mungu akamuumbia adamu siku ya SABA Ili angalau Iwe weekend ya Mwanadamu akumbuke kuumbiwa uumbaji wa siku Sita.
Ila Kwa Sababu adamu wa leo tumegoma, na hatutaki kusikia hilo, na wengine wameamua kuwa wakorofi zaidi kwa kunyofoa hayo maelezo kwenye Amri za Mungu. Upotofu huu utakuwa mkubwa sana, na Wengi wanaoamini haya soon watakuwa atheists.
 
Baada ya uthibitisho wa Ellen kwenda Mbinguni bila kufa kwanza na huko kuona Amri ya sabato imezingirwa na "utukufu?"
Kutoka 20:11. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.

'' Petro na Mitume wakajibu wakasema, IMETUPASA KUMTII MUNGU KULIKO MWANADAMU'' Matendo 5:29
Nje ya 24hrs Creation Kuna maelfu ya nadharia kwa jina la Uumbaji wa mamiaka ya milioni.
Jiandae kuogelea kwenye Bottomless pit la mamilioni ya miaka huku unaacha ukweli mwororo wa Kauli sahihi na dhahiri ya Mungu huku ukitumia vikokotoo vya lugha za kiebrania kama mbeleko.
Kufanya Tallying ya Uumbaji wa Bibilia na secret evolution Ideas based on bible utafanikiwa at Infinity.
 
Ulimwengu ama dunia???,kama ni dunia sidhani hataka miaka 6000 imefikisha??

dunia haijafikisha hata miaka 10000,fatilia ujio wa sirians from planet x..
 
Kabla ya day 1 Biblia inasema
‘In the beginning God created the heavens and the earth. And the earth was formless and void, and darkness was over the surface of the deep; and the Spirit of God was moving over the surface of the waters. Then God said, “Let there be light”; and there was light. And God saw that the light was good; and God separated the light from the darkness. And God called the light day, and the darkness He called night. And there was evening and there was morning, one day.’

Hii mistari inaonyesha kwamba UUMBAJI ulianza baada ya kuwepo a VOID and FORMLESS EARTH. Roho ya Mungu ikielea juu ya maji
Hayo yalitokea kabla ya kuanza uumbaji wa day one. Hata mtoto wa kindergarten anaweza kudadavua hii.
Umbaji wa mwanga ulianza day one wakati maji na miamba ilishakuwepo, Ndio maana nasema UUmbaji wa Miamba hakufanyika katika six day (This are NOT literal days, utaendelea kujidanganya mpaka lini ndugu
 
Mungu aliumba Mbingu na Nchi hapo mwanzo. Sio Maji na Miamba.
Hapo Kuna Mawili Sentensi hiyo inaanza na summary ya kazi Yote aliyoifanya kisha akaanza kuichanganua.

Pili, Aliumba hayo Mwa Milisecond ambayo inamezwa na Siku ya Kwanza.
2
Kwa nini najenga hoja hizi ambazo unaweza kuona natembea juujuu bila ufahamu wa Bibilia na siri zake.
Mungu anataka tusitafute habari za Mqmbo yake kwa waganga, wqchawi wasihiri hata wasomi.
Kuhusu hili, Bibilia au mwqnzo Ingeishia hapo tungekubaliana ila Mungu alieyeumba Vyote Kuanzia Mbingu na Nchi na Vyote Vilivyomo amerudia mahala mahala kuwa alifanya Yote kwa Muda wa siku sita. Sio alizijaza mbingu na nchi ndani ya Siku Sita.

Kosa mnalofanya kulazimisha nadharia za Sayansi zitally na mambo ambayo Mungu ameshayafafanua huku mkiegemea kwenye evolution. Bibilia Ingeishia Mwqnzo 1 na 2 Tungechanganyikiwa ilq hili limefafanuliwa vizuri kwenye amri Kumi. Yesu naye akatia Muhuli kuwa Aliumna Siku ya Saba kwa aajili ya Wanadamu.
Wakosoaji wa Bibilia Waislam, Atheists na Higher cliticals ndio wanautamaduni wa kung'ang'ania kistali huku wakiwa hawataki ufafanuzi ndani ya Bibilia ulio wazi mahala pengine pakifafanua tukio hilohilo.
Katika Hili naomba niendelee kuwa mjinga kuliko kujiunga na wenye hekima wa dunia hii.
 
Hii ya microsecond tukubaliane ni ya kwako tu!
Hakuna mtu anayekataa kuwa Mungu hakuumba mbingu na nchi
Ila haya mambo ya uumbaji kuna a lot of misinterpretations kuanzia kwenye tafsiri ya hizo siku sita na the creation process
Nataka tu kukuambia kuwa intentively Mungu ametuficha kabisa juu ya uumbaji wa dunia na ulimwengu na ndio maana alianzia kutufunulia pale kwenye mwanga na kuendelea ambayo hata hizo alizotufunulia alieleza in pieces.
Hivi unajua kuwa Mungu aliumba tena kwenye Chapter 2
Chapter 1 aliwaumba mwanamume na mwamake kwa pamoja Mwanzo 1-26
Na katika chapter 2 akamuumba mwanamume kwanza halafu akaja kumuumba mwanamke kutoka kwenye ubavu wa mwanamume
Kama Miamba na maji iliumbwa kwa microsecond kama unavyosema halafu mwanadamu akaumbvwa kwa siku nzima si unaona hapo unaleta confusion na hata mwenyewe baada ya miucrosecond ijayo hutaelewa umeandika ninmi?
 
Mkuu ndio maana nimeuliza je ni wakati gani ambapo unagundua ni lateral au figurative language ndio imetumika.... Mfano Yesu kasema kuhusu hao waisrael 144000 na malaika wapo 10,000×10,000 je na sisi tuisome hiyo lateral kisa tu Yesu ndio kafafanua?? Ama unakubaliana na mimi kuwa zote ni parables zenye mafumbo ikiwemo creation process???

Kuhusu kutoka 20 pia ni fumbo mkuu ikimaanisha kwa VIPINDI vyote Mungu alifanya kazi ila kuna siku aliitenga akapumzika sasa akaitranslate kwa hali ya binadamu maana kama angesema achukue siku zake saba ina maana sabato ingekuwa let's say kila baada ya miaka kadhaa sio siku!!! Ni sawa tu na ufunuo wa Yohana aliandika mambo ya siku za mwisho lakini kutumia maelezo na uelewa wa enzi zake mfano vita kupiganwa kwenye farasi na mapanga ilihali leo hii vita zinapiganwa na bunduki sasa mtu akitafsiri lateral si atadhani vita za siku za mwisho ni mpaka watu washike mapanga tena sio bunduki!!

Je kwakuwa ufunuo wa Yohana ulielezewa na Yesu kupitia Yohana je na sisi tusubiri vita za mapanga ???
 
Nani kwanini hizo siku zingine hakuumba kwa microsecond wakati yeye ni Mungu mwenye uwezo?
 

Hakuna ukidhani wowote kwani bibilia inatoa majibu kwa kuanza na neno hapo mwanzo Dunia ilikuwa utupu ikionyesha kuna jambo nyuma hapo ,lakini vile vile umeeleza vyema biblia imaanzia history kuanzia kwa adamu ambapo dunia kwa maana ya sayari ilikuwepo miaka mingi kabla ya adamu na tena sijaona popote ambapo biblia inataja umri wa dunia ili kuweka ukidhani bali umri na calenda kuanza kwa adamu
 
nimekupa option mbili ila umechagua Moja. kwa hii uliyoichagua nimesema microsecond kwa sababu hajasema ila anasema yeye mwenyewe aliyeumba kasema siku sita alimaliza kila kitu, na akasema alifanya yote siku sita.
Ila sio ugomvi mkuu, Huu unqodhani ni upumbavu na ufinyu wa uelewa wa maandiko ya siri yalifichwa sana na Mungu ambao unapelekea niamini SIKU SITA LATERAL mimi kwangu naona ni hekima. Unaweza kuendelea na hekima ya Wanadunia na wanasayannsibibilia wanaosema ulimwengu uliumbwa kwa miaka milioni nne.
 
Jambo jingine la kutia changamoto watafsiri wa bible ni kwenye zile siku 6
Biblia inasema Mungu alifanya kazi siku sita na siku ya saba akapumzika
Swali je siku ya nane Mungu aliendelea kufanya kazi?
Na siku zingine je ukiondoa siku ya saba?
Tunaposema hizi siku ni siku katika format ya Mungu mnatubishia
Kwa Mungu hakuna siku ya nane na kuendelea, Maana yake ni nini?
Mungu anaposema siku ya kwanza, ya pili mpaka ya saba kila siku ina maana yake katika mahesabu ya Mungu

Kwa haraka tu
3 ina maana ya ukamilifu
7 ina maana ya undefine au indefinitely au eternity au milele
Maana ya Mungu kufanya kazi siku sita nitaeleza baadaye lakini kumpunzika siku ya saba maana yake amepumzika milele, kazi Mungu alishafanya yooote na hana kazi tena ya kufanya, Ukinibishia hii nitakuja na maandiko punde
so 7 means eternity rest na origin ya sabato ndio huyo
 
Umri wa vyote sio mmoja.Ulimwengu uliumbwa takribani miaka bilioni 13.5 kisha baadaye zikaja kutokea galaxy mbalimbali na baadaye sana dunia pamoja na solar system katika ukanda wa milky way ziliumbwa pamoja na sayari zingine takribani miaka bilioni 3.5 iliyopita
Tofauti ni sizes lakini vyote vimepatikana pamoja kama zao la Big Bang (a.k.a Big explosion). Umri wa vyote ni mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…