Habari za mchana wakuu kama kawaida huwa nakuja na mada za kuchokoza fikra zetu hasa kwenye mambo ya kiimani hivyo mada hizi sio za kukosoa dini fulani au vitabu vya imani ila ni kuhoji tu ili tupanue fikra zetu kwenye masuala haya kwa faida yetu sote so sitegemei iibue mijadala ya kidini bali kuelimishana juu ya mambo haya baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye mada husika ya leo.
View attachment 948749
Biblia na umri wa Dunia
Mwaka 1650 professor wa masuala ya theologia na Askofu wa makanisa ya protestant wa Ireland John Ussher aliandaa maandiko yake kupitia mfululizo wa vitabu vyake kuanzia cha Annals of the Old Testament: Origins of the world ambacho ndani yake aliibua mjadala mpana sana wa karne nyingi sana. Ussher alipiga hesabu ya muda ulivyopita kati ya Adam kuumbwa hadi Yesu kuzaliwa na kugundua kwamba ni miaka 4000 imepita tokea Adam aumbwe hadi Yesu kuzaliwa hivyo kufanya dunia yetu ikiwa na wanadamu kuwa na miaka elfu 6 pekee mpaka sasa!!. Ussher alitumia maandiko kama chanzo cha nadharia yake alitumia nyaraka za masoretic zilizotumika kuandaa Biblia za agano la kale ili kuweza hesabu umri wa Adam hadi vizazi vya Abraham hadi kufikia Yesu na baada ya mnyambuliko huo alifanikiwa kugundua kwamba dunia iliumbwa usiku wa October 23 4004 kabla ya kristo.
Young Earth Creationists
Vuguvugu hili la YEC lilianza miaka ya 1960 ambapo iliasisiwa na wasomi 9 chini ya PhD wa theolojia na uhandisi Bwana Henry Morris wakijikita kwenye utafiti wa uhalisia wa umri wa dunia na uumbaji na wakahitimisha rasmi kuwa dunia tunayoishi iliumbwa ndani ya miaka elfu 10 pekee na sio zaidi ya hapo na wao pia walitumia maandiko ya Biblia ya kiebrania ili kufikia hitimisho hilo hivyo na wao wakaunga mkono hoja za hapo nyuma za Professor John Ussher na hata leo hii wameweza shawishi zaidi ya 40% ya wakazi wa marekani kwa takwimu za 2017 wanaamini nadharia hii kwamba uumbaji wa dunia ni kwa mujibu wa Biblia hauzidi miaka 10,000 iliopita.
View attachment 948751
SAYANSI inasemaje??
Baada ya sayansi na teknolojia kukua na kuongezeka vifaa vya kupima umri wa miamba,mazao na mifupa ya wanyama wakaibuka wasomi wa sayansi waliohoji kuhusu uhalali wa nadharia hizi na imeleta utata na mjadala mzito kwa miaka mingi sasa. Mwanasayansi wa karne ya 20 Clair Cameron Patterson baada ya tafiti kadhaa juu ya miamba akagundua ulimwengu toka uanze una miaka billion 4.5 na baadae wanasayansi mbalimbali wakaja na tafiti mbalimbali zikidai kwa usahidi wa kisayansi na kiacholojia kwamba uhai duniani umekuwepo miaka takriban 3.8 Billion iliopita hivyo kukinzana kabisa na nadharia hizo mbili za juu kuwa Biblia
Jinsi ya kupima
Kwa upande wa Young Earth wao wanalalia maandiko kwa kiasi kikubwa na kupiga hesabu miaka ya kibiblia tokea Adam hadi Yesu lakini wanasayansi wamepiga hesabu zao kwa ushahidi wa kushikika wakitumia mfumo unaitwa radiometric dating ambacho kinapima miamba hasa stage tofauti za jinsi miamba inavyooza na ambapo kila stage ina umri wake yake yaani miaka kadhaa ili ifike stage nyingine ya kuoza hivyo wanapiga hesabu kuanzia layer ya mwisho mpaka ya kwanza na kufikia hitimisho la umri wa mwamba huo na wakafanikiwa kugundua mwamba wa kwanza ulitokea miaka 3.8 Billioni iliyopita.
View attachment 948748
Utafiti wangu (Primary)
Binafsi nilichukua hatua kuonana na wanatheolojia kadhaa kutoka chuo fulani cha Biblia wenye ngazi ya PhD na wamenijuza kwamba Biblia haikuandikwa kwa maneno bali mafumbo hivyo isitafsiriwe kwa maana zetu bali kwa mafunuo na maana zilizo kwa Biblia... Mfano wanadai Dunia haikuumbwa kwa siku 7 kama zetu hizi bali miaka mamilion na wakaenda mbali kusema Biblia haikuanza kuandika matukio yote bali imeandika matukio juu ya watu waliochaguliwa tu hivyo wanakiri kuwa kweli dunia ina miaka mabillion na sio miaka elfu 6 pekee bali wanaotafsiri maandiko kwa akili zao ndio wanapotosha sababu wameitafsiri maneno kama yalivyo badala ya kutafuta maana ya hayo mafumbo na wakanipa mistari michache.
Yohana 16:25
25
Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.
Na wakaenda mbali kusema hata hayo mafumbo walioambiwa kuandika Biblia hawakuyaelewa sababu ni siri imewekewa hadi wakati muafaka yaani mwisho wa dunia ufike soma hapa kisa cha Daniel
Daniel 12:4
4
Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Hapa tunaona kuna maandiko na nabii zimefichwa kwa uelewa wetu kabisa hata Daniel hakuelewa!!
Daniel 12:8-9
8
Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?
9 Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho.
Hivyo kama hata Daniel kuna baadhi ya vitu alifichwa na mpaka anaandika hakuvijua basi hata sisi hatuwezi vijua mpaka siku ya mwisho hivyo wakahitimisha mjadala kwa kusema huenda ni kweli dunia ina 4.5 Billion years ila sio 6000 kama YEC inavyosema maana Biblia haielezi hicho kuwa ni miaka 6000 bali watu wanatafsiri maandiko kwa akili zao ilihali YAMEFICHWA!!
View attachment 948750
Hitimisho
Ukinzano huu kati ya maandiko na sayansi juu ya asili ya umri wa ulimwengu umezua mjadala mpana sana huku kila upande ukivutia kwake nikaona kwa kuwa JF ni kisima cha maarifa nilete hii mada ili tuweze kufikiria pamoja je umri wa dunia upi ni halisi
4.5 Billion ama 6000?
Naomba kuwasilisha
Fungu la kwanza hapo chini linalotoka kitabu cha Mwanzo 1, linasema wazi kabisa kuwa Mungu alianza akaumba Mbingu na Nchi kwanza halafu ukapita muda ambao hatujaelezwa ni muda gani, halafu ndiyo akafanya yale yote yanayoelezwa kuanzia fungu la 3.
Kwa hiyo ieleweke wazi kuwa
MOJA Alichofanya Mungu kinachoelezwa kuanzia Mwanzo 1:3 na kuendelea si uumbaji bali ilikuwa ni urekebishaji, nyongeza vikiambatana na upambaji wa kile ambacho tayari alikuwa aameshaumba huko nyuma.
MBILI Mungu huwa hahitaji kitu phsical katika uumbaji, huwa anatamka tu halafu kilichokuwa hakipo kinakuwepo. Ukiona anatamka kwa kitu kitu phsical, ujue hapo haumbi ila anafanya marekebisho, yaani modification.
TATU Aliwaumba Adam na Hawa kwa kutamka wakiwa ni roho zisizokuwa na mwili ndani ya NAFSI MOJA, baadaye tena akawafanyia marekebisho kwa kufinyanga udongo akawapa miili.Huu udongo ulikuwepo kabla ya watu hawa, Mungu alikuwa ameshauumba huko nyuma
NNE Kutokana na hoja hizo hapo juu,Mungu hakuumba ulimwengu kipindi anawaumba Adam na Eva ila ulimwengu ulikuwepo tangu kipindi kirefu huko nyuma. Hii inathibitishwa na hilo fungu la Mwanzo 1:1 na na mengine yote yanayofuata kwenye sura hiyo
TANO. Muumini yeyote wa dini anayeaamini kuwa ulimwengu una miaka 6000 hayuko sahihi, bali tangu kuumbwa Adam ndiyo miaka 6000. Ulimwengu ulikuwepo kabla ya Adam
SITA Wana Sayansi wanaofanya tafiti kwa mfano za miamba na kugundua kuwa kuna miamba ina miaka mabillion tangu kuwepo kwake, WAKO SAHIHI NA HAWAPINGANI NA BIBLIA, kwa sababu Biblia yenyewe inathibitisha kuwepo kwa ulimwengu kabla ya Adam, kwenye hilo fungu la Mwanzo 1:1
SABA Muumini yeyote ambaye alikuwa na taarifa zisizo sahihi kuwa ulimwengu uliumbwa miaka 6000 iliyopita, naomba arejee tena kusoma Mwanzo 1:1 na atusaidie kutoa tafsiri upya, kama pengine kama haya niliyoyasema hapo juu anadhani hayako sahihi
1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.