Mkuu shukrani kwa kudadavua vizuri kabisa juu ya credibility ya vipimo vya kisayansi katika lugha inayoeleweka ningependa mkuu
mitale na midimu aione hii atupe maoni yake.
mkuu maelezo ya mkuu pale yako vizuri ila siungi mkono hoja ya dunia mamilioni kwa maelezo ya vipimo vyake.
Hija zangu kutoka katika maelezo ya mkuu
Kituko ni kama ifuatavyo:
1:anasema bibilia imekuwa coded, lkn katika decoding au kuzisimbua hoja zilizokuwa coded kwenye bibilia anatumia nadharia za kisayansi. Je Bibilia haina uwezo wa kujing'amua yenyewe?
Mfano hizo tunazoita codes za kitabu cha mwanzo na Torati, Yesu aliwalaumu marabbi na mafarisayo kwa kushindwa kuziona zikimuelezea yeye. Alipoquote Mwanzo na matukio yake Yesu alitafsiri literally. Je Yesu alitenda dhambi kwa kuwalaumu wale jamaa kushindwa kuelewa mambo ambayo kumbe yangesubiri sayansi ndio yaeleweke?
Nini nafasi ya Roho mtakatifu katika decoding maana inaonyesha hapo msaada wa sayansi ndio wenye nguvu.
2: Kuhus Galileo, Aliamini bibilia na aliamini uumbaji, hivyo anautofauti na wanasayansi wanaopinga uumbaji. Kanisa lilishikilia Bibilia lkn upande mwingine lilikumbatia philosophy za kigiriki. Na Galileo aliwashinda wanasayansi wa kigiriki na kuwadhalilisha kwa ushahidi kuwa mambo yao ni ya kutunga na hayana ushahidi. Kwa Sababu kanisa lilikuwa upande wao lilimshughulika ingawa viongozi wengine walikuwa marafiki zake, waliona anaweza kusababisha machafuko. Ila msingi wa hoja hapa, utetesi wa Galileo uliegemea Bibilia, Ufahamu wa kanisa ulichanganya bibilia na philosophia za kigiriki, Ufahamu wa wanasayansi wengi wa leo wanaanza kwa kumpinga Mungu na uwepo wao hivyo wengi hata kama watagundua kitu sahihi watalazimisha kitoke kwenye mtazamo wa Bibilia. Hii ni taadhari inayotakiwa kuchanganywa katika decoding zetu.
Kwenye MADA
* Sio wanasayansi wote wanakubaliana na hiyo miaka 4.5Mil. Kuna wanasayansi wacha Mungu, Wengine sio wacha Mungu lkn ni Pro -Creation wanakubaliana na 24Hrs Days za Kwenye Bibilia. Hitimisho la wanasaynsi la kuleta miaka hiyo halihusishi Bibilia na halikubaliani na Uumbaji wa Mungu Bali Cosmic Evolution na mambo ya Bing Bang Theory ambayo ni anti-Biblical.
Huoni kwamba tunahitaji kuchekecha akili zaidi ya kukubali kila kitu cha mwanasayansi hasa yeye anapokana Bibilia kufanya baadhi ya mahitimisho na sisi kuyatumia hayo unbiblical conclusions kuwa Biblical.?
* Kuhusu Miamba na Tafsri yake ya pili. Hili naomba nilifanyie kazi maana na kuona wanasayansi wanaoounga mkono bibilia wanalizungumziaje. Maana nimewahi kujifunza huko nyuma ila kwa sasa sikumbuki vizuri. Linamaelezo ya kutosha kupinga hizohizo miaka maelfu.
* Conclusion pia ya mkuu kituko inaacha ombwe la kibibilia. Maana anatushawishi kwa kutumia sayansi mambo ya kibibilia, ilanapozungumzia kwenye Bibilia anaishia kusema kule Kuna CODES. Nilidhani ni wakati wa Kuzitafuta ni zipi na kwa kutumia Bibiliq tuzidecode kwa pamoja. Mfano Kusema kulikuwa na watu wengine walioumbwa nje ya Adam na Hawa kama baadhi wanavyojenga hoja ni Kubishana na Bibilia Yenyewe. Vinginevyo dhambi ingewahusu adam na hawa na watoto wao, hao wengine wangeendelea kula raha. Ila kusema kuoana Ndugu kwa Ndugu au watoto wa Kike kitohesabiwa katika baadhi ya maeneo ya Bibilia ikiwemo mwanzo inaleta mantiki ya kibibilia maana ilibidi waoane ndugu ili kuiendeleza kizazi, Ila walipojaa katika uso wa Dunia, Mungu akasema kupitia Vitabu Vya Musa ni Laaana Mtu Kulala na mke wa Baba Yake au hata dada yake. Nasisitiza tusome bibilia kwa jicho linaloona nyuzi 360 zinazocover mwanzo hadi ufunuo sio kasehemu kamoja na kujenga hitimisho.
Maelezo haya sio Msaafu, yanaruhusiwa kukosolewa kupingwa, kubishiwa, hata kuboreshwa.
Ila kuhusu Mimi, Nasimama na wote wanaoamini siku saba na Young earth 6000 maana ndio maelezo ambayo kwa kutumia bibilia naweza kiyasimamia. Na naungana na wanasayansi wote wanaoyaamini haya kama Alivyoeleza Mungu katika Bibilia.