Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Mkuu mitale na midimu kama unashikilia msimamo wa Young Earth creationists kuwa dunia ina umri wa miaka 6000 pekee labda niulize je accuracy yao ipoje?? Mfano calendar ya kiyahudi na wakati mwingine walitumia tarehe za kibabylon kuhesabu miaka yao na inajulikana kabisa kuwa tarehe zao hazilingani kabisa na gregorian calendar maana miaka yao ilikuwa mifupi kuliko yetu sasa huoni hata hiyo elfu 6 tayari ina kasoro kubwa?? How accurate can it be??

Nikupe mfano mwanzo 12:4 inasema Abraham alikuwa na umri wa 75 alipoondoka Nchini kwake lakini Biblia hiyo hiyo kupitia Matendo 7:4 inasema Abraham hakuondoka mpaka baba yao alipokufa hivyo kufanya aliondoka akiwa na miaka 135!!

Sasa errors kama hizi kwenye kuhesabu miaka zinawezaje kuleta credibility kwa mfumo waliotumia kina YEC kufikia conclusion yao kuwa dunia ina miaka 6000 pekee??
 
Mungu katika Uumbaji alifanya process ambayo kila kitu kimekuwa kiki-evolve chenyewe. Kwa lugha nyingine aliweka automatic mechanism ya vitu kutokea na kisha development kutokea au kuendelea. Mungu Mwenye uwezo hawezi kuwa Wa kuumba sisimizi au funza kwa kila alicho nacho. HE just created the Process.
ushahidi wa bibilia???
sio hekima zako mkuu.
Mungu aliumba vyote, Bibilia imeweka wazi hivyo mwanzo hadi ufunuo.
Mechanism ya evolution ndani ya Biblical creation unaisupport na andiko gani?
 
Chief,mimi nafikiri Mwalimu Nyerere alitumia maneno ya "uwezo tunao,sababu tunayo na nia tunayo" akiwa na maana ya kuwawakilisha Watanzania wote katika tamko lake hilo. Sidhani kama alikua na maana nyingine zaidi ya hiyo.
Hata magufuli anaposema MIMI anamaanisha Mamlaka yake tuliyompa! Ndiyo watanzania hao. Keanu Nyerere angesema uwezo ninayo, sababu ninayo na nia ninayo ingebadilisha chochote?? So bado anawakilisha watanzania???

Jaribu kusimama katika Lugha na majazi yake. Usisimame katika mafundisho yaliyopotolewa. Jaribu some yuda 1:4 utaelewa maana kwa undani kama mwanzo hujaielewa.

Katika Yohana 17:3 Yesu anasema; "Na uzima wa milele ndiyo huu, Wakujue ewe Mungu wa pekee na wa kweli! Na Yesu kristo uliyemtuma. Unahitaji mwalimu hapo???.

Achana na kasumba! Mungu ni mmoja asiye na mshirika!

"Na hatukumtuma kabla yako mtume yeyote Ila tulimfunulia ya kwamba Hapana mungu Ila MIMI. Basi niabuduni MIMI tu". (Qur'an 21:25)
 
Bible vs quran vyote matango pori mnazidiana ujinga tu.

Hata Kule wewe na wenzio kuamini kwamba hakuna tofauti kati ya Biblia na Kurani na kwamba hakuna kilicho chenye maudhui ya kusadikika kati vya hivyo viwili nayo ni imani matangopori.
 
Ninyi ndio basi wagonjwa mliofukamia uji na mkavimbewa. Biblia waachieni wenye nayo. Ninyi endeleeni tu na matangopori ya Muhammad madhali wanaume wazima mliamua kudanganywa kiasi kile.Ukitaka kufahamu Muhammad alikuwa hajitambui au anaongea nonsense na bado hajui kama ametapika ujinga,fikiria eti kuna wakati Jibrili aliacha kushusha Wahyi kwa wiki kadhaa na baada ya kujiuliza imekuwaje ndio akagundua Mbwa amefia chini ya Kitanda!

1. Hivi Malaika na Allah wanamuogopa Mbwa?

2. Hivi na Khadija walikuwa na Pua za aina gani hata Mbwa afie chini ya Kitanda na wasiweze kugundua kwa wiki zote zile?
Sanctus, utakuwa umechimba kweli au umepotoshwa kweli. Hebu naomba rejea ya hayo mafunzo. Usije kuwa umelishwa matango pori na walimu wako.
 
Nafikiria unapaswa pia unaposoma Biblia uelewe Lugha inayotumika na aina ya speeches walizotumia waandishi kufikisha maudhui kwa Hadhira husika. Kusema "Mimi Mwenyezimungu niliziumba...", sio kauli ya Mungu moja kwa moja. Hivi kwa mfano Leo kuna watu wanasema: " Mungu ameniambia" au "Bwana amesema nami..." au alivyokuwa akisema Ellen White " ...Naliona..." Mungu alinionesha...", ina maana hapo ni kweli wahusika huwa wameambiwa na Mungu moja kwa moja au Ellen alikuwa amemuona Mungu kweli?

Nakusihi sana ujitahidi kusoma historia ya Kila kitabu katika Biblia, Historia ya kila mwandishi na Staili ya Uandishi Wa kila kitabu. Vitabu vingine katika Biblia ni Hadithi, Sala, Mambo ya Hekima, Apocalyptics na kadhalika. Unasoma sana Biblia ila nimegundua tatizo kubwa ni msingi Wa Biblia uliojengewa toka Mwanzo.
mkuu jifunze kujibu, hata ikibidi utoe basi hizo tafsiri kificho za kauli za Mungu au bibilia ulizo nazo sio maelezo yenye sura ya kulaumu badala kujibu au kukosoa hoja kwa ufahamu unaodhani ni sahihi.

Kumbukumbu la Torati 9
Iko wazi Mungu na Musa wako Mlimani Siku 40.
Musa anasema Zile amri Mungu ameziandika kwa Chanda chake kama alivyowaeleza Verbally pale mlimani.
Akaandika (sio Musa Bali Musa anasema Mungu ndiye Kaandika).
Sasa nimuamini nani mkuu Wewe au Musa.
Kama unatafsiri ziweke ili tuone kama zinamashiko, kama tafsiri hizo ni siri pia useme.
 
ushahidi wa bibilia???

1. Biblia sio kituo kiimani Bali mwanzo tu Wa mambo ya kiimani. Unapoiona Biblia kama ukamilifu Wa kila kitu kiimani ndipo hapo unapoachwa hapo hapo huku wenzio wakizidi kukata mbuga katika mambo mazuri zaidi ya kiimani.

2. Unaponidai reference ya Biblia kwa kila jambo naomba unidai na andiko linaonyesha kwamba Mama yake Yesu alishakufa. Niulize Pilato, Paulo, Petro, Yusufu Wa Arimathaya, Magdalena, Maria Wa Cleopa imeandikwa wapi kwamba hao wote walishakufa.
 
Mungu katika Uumbaji alifanya process ambayo kila kitu kimekuwa kiki-evolve chenyewe. Kwa lugha nyingine aliweka automatic mechanism ya vitu kutokea na kisha development kutokea au kuendelea. Mungu Mwenye uwezo hawezi kuwa Wa kuumba sisimizi au funza kwa kila alicho nacho. HE just created the Process.
HE just created the Process.

Kulingana na andiko lako hapo hiyo process bado inaendelea? Yaani Kuna Wanyama wapya wanaendelea kuzaliwa? au funza aina tofauti au watu au ndege au nk, nk, nk???.

I ought question your understanding!
 
Hata magufuli anaposema MIMI anamaanisha Mamlaka yake tuliyompa! Ndiyo watanzania hao. Keanu Nyerere angesema uwezo ninayo, sababu ninayo na nia ninayo ingebadilisha chochote?? So bado anawakilisha watanzania???

Jaribu kusimama katika Lugha na majazi yake. Usisimame katika mafundisho yaliyopotolewa. Jaribu some yuda 1:4 utaelewa maana kwa undani kama mwanzo hujaielewa.

Katika Yohana 17:3 Yesu anasema; "Na uzima wa milele ndiyo huu, Wakujue ewe Mungu wa pekee na wa kweli! Na Yesu kristo uliyemtuma. Unahitaji mwalimu hapo???.

Achana na kasumba! Mungu ni mmoja asiye na mshirika!

"Na hatukumtuma kabla yako mtume yeyote Ila tulimfunulia ya kwamba Hapana mungu Ila MIMI. Basi niabuduni MIMI tu". (Qur'an 21:25)
Aisee!
Mbona unanilisha maneno ambayo sijayaandika!?
Wapi nimesema kuna Mungu zaidi ya mmoja?
Naona umeshindwa kunijibu swali langu mzee,au huenda swali langu kwako halieleweki,nikiendelea kung'ang'ania kukuuliza itakua ni kero,ikishakuwa kero mwisho wa majadiriano/majibizano yetu hautakua mzuri.
Ahsante kwa ushirikiano wako Kiongozi,watu wenye majibu na ambao watafanikiwa kuliona na kulielewa swali langu watanijibu.
 
Swali langu limetoka katika maneno haya kutoka katika kitabu cha Qur'an:
"Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika"
Hiyo SISI katika lugha ya Kiswahili inawakilisha nafsi ya tatu katika wingi, ina maana inatumika kuelezea mtu/nafsi zaidi ya mmoja. Hivyo basi kauli hiyo inaonesha Mungu hakua peke yake kipindi anafanya uumbaji wa binadamu.
Ndio mimi nimekuuliza, Mungu alikua na nani wakati wa uumbaji wa binadamu mpaka akalazimika kutumia neno SISI?
Mistari uliyonitumia inaonesha Mungu ni mmoja,mimi sijapinga hilo,pia swali langu halihitaji kujua kuwa kuna Mungu zaidi ya mmoja au la,nachohitaji kujua mimi ni kwanini limetumika neno SISI?
Sidhani kama neno SISI limetumika bahati mbaya,lazima lina maana yake.
Sidhani kama neno SISI limetumika bahati mbaya,lazima lina maana yake:

Njoo ukae kwenye Zulia ufundishwe Nahau.
 
Sanctus, utakuwa umechimba kweli au umepotoshwa kweli.

Tuombe uzima Mkuu. Sina haja ya kuwa Gnostic hata siku moja. Gnostic ni hao akina John Ussher wanaotafsiri Biblia kinyumenyume.

Mambo haya nitayaeleza kadri muda utakavyo rafiki kwangu. Kwa sasa niko na series ya mambo ya kizushi katika Imani nayaonesha ili watu wafumbuliwe macho. Kisha sasa tutaanza kueleza hatua kwa hatua jinsi Biblia ilivyopatikana.
 
Aisee!
Mbona unanilisha maneno ambayo sijayaandika!?
Wapi nimesema kuna Mungu zaidi ya mmoja?
Naona umeshindwa kunijibu swali langu mzee,au huenda swali langu kwako halieleweki,nikiendelea kung'ang'ania kukuuliza itakua ni kero,ikishakuwa kero mwisho wa majadiriano/majibizano yetu hautakua mzuri.
Ahsante kwa ushirikiano wako Kiongozi,watu wenye majibu na ambao watafanikiwa kuliona na kulielewa swali langu watanijibu.
Nashukuru Pia kwa uelewa wako! Ataayesoma posts zangu atakuwa ameelewa utetezi wangu kwa tafsiri ya neno Sisi au hatu au Tuli au natu ambayo yote yanaamnisha wingi katika maana nyepesi.
Na Maneno ila mimi, niabudu, kwa mfano wake nk kwa Tafsiri ya maana ya Tafsiri ya Maandiko ya Kimungu.

Kusema Mungu ni zaidi ya mmoja ni kumshirikisha na ni dhambi. Na hii ndiyo inayotofautisha kati ya Imani ya Kiislamu na Imani zingine.
Ukitulia ukatafakari utanielewa. Usiponielewa lakini wasomaji wengine wameelewa vizuri.
Namuomba Allah akupe fahamu nzuri ya mafundisho yake. Amiin!
 
Tuombe uzima Mkuu. Sina haja ya kuwa Gnostic hata siku moja. Gnostic ni hao akina John Ussher wanaotafsiri Biblia kinyumenyume.

Mambo haya nitayaeleza kadri muda utakavyo rafiki kwangu. Kwa sasa niko na series ya mambo ya kizushi katika Imani nayaonesha ili watu wafumbuliwe macho. Kisha sasa tutaanza kueleza hatua kwa hatua jinsi Biblia ilivyopatikana.
Nami naendelea kuchimba!
 
Mkuu mitale na midimu kama unashikilia msimamo wa Young Earth creationists kuwa dunia ina umri wa miaka 6000 pekee labda niulize je accuracy yao ipoje?? Mfano calendar ya kiyahudi na wakati mwingine walitumia tarehe za kibabylon kuhesabu miaka yao na inajulikana kabisa kuwa tarehe zao hazilingani kabisa na gregorian calendar maana miaka yao ilikuwa mifupi kuliko yetu sasa huoni hata hiyo elfu 6 tayari ina kasoro kubwa?? How accurate can it be??

Nikupe mfano mwanzo 12:4 inasema Abraham alikuwa na umri wa 75 alipoondoka Nchini kwake lakini Biblia hiyo hiyo kupitia Matendo 7:4 inasema Abraham hakuondoka mpaka baba yao alipokufa hivyo kufanya aliondoka akiwa na miaka 135!!

Sasa errors kama hizi kwenye kuhesabu miaka zinawezaje kuleta credibility kwa mfumo waliotumia kina YEC kufikia conclusion yao kuwa dunia ina miaka 6000 pekee??
Ungeonyesha utofauti wa Kalenda ya Kiyahudi kule Babiloni na Baaada ya kurudi na Je Uliathili Mfumo wa Siku sita fanya kazi siku ya saba Pumzika kama walivyoishi kule jangwani?
Je unakubaliana na mimi hawakwenda utumwani taifa lote kabisa kuna masalia walibaki?
Lkin licha ya kalenda kubadilika Mfano Mwezi Habib kuitwa Nissan, unakubaliana kuwa kwa sababu walikaa miaka 70 tu huko na walikuwepo wacha Mungu huko na manabii pia kama Ezekiel, Daniel na wakina ezra kumbukumbu hazikupotezwa hasa kwa maana ya week days seven?

Ndio maana tunasema ni makadilio ila makadilio hayo hayawezi kuturudisha katika miaka milioni.
Ukokotozi wa miaka hiyo unabase katika uzao wa Adam wa kitabu cha mwazo sio Ibrahim. Kama Adam aliishi miaka 900 mfano, Mwaka moja wake utaanza siku aliyoumbwa, dunia ikiwa na umri wa siku tano.
Ungejenga hoja kuanziq hapo sio Ibrahim.

Kuhusu Matendo na Mwanzo nq ukanganyaji wa Umri.
1: Ikiwa kweli kuna huo mkanganyiko, Bado creationist wako sahihi maana hauna range ya malaki au mamilioni bali makumi.
2:Lkn matendo sioni kama imekosea maana imetaja vituo Viwili. Alipotoka kwa wakaldayo (ur ya wakaldayo) hakwenda kaananinmoja kwa Moja, Alienda Harani, Baadae akatoka harani akaenda Kaanani.
Sasa Yeye hasemi alipotoka kwa baba Yake kule Ur (75Years), Bali aalitoka harani sio kwa wakaldayo baada ya kufa kwa baba Yake. Umejumlisha miaka ambayo haina uhusiano, labda kama kuna sehemu hatujelewana mkuu wangu.
 
1. Biblia sio kituo kiimani Bali mwanzo tu Wa mambo ya kiimani. Unapoiona Biblia kama ukamilifu Wa kila kitu kiimani ndipo hapo unapoachwa hapo hapo huku wenzio wakizidi kukata mbuga katika mambo mazuri zaidi ya kiimani.

2. Unaponidai reference ya Biblia kwa kila jambo naomba unidai na andiko linaonyesha kwamba Mama Yesu alishakufa. Niulize Pilato, Paulo, Petro, Yusufu Wa Arimathaya, Magdalena, Maria Wa Cleopa imeandikwa wapi kwamba hao wote walishakufa.
Nimekuomba ufafanuzi kwa mambo ambayo Yamo kwenye Bibilia. Wewe unaniuliza ufafanuzi wa mambo ambayo hayamo kwenye bibilia.
Mfano Kufa au wasife hawabadilishi Fundisho kwamba Mwanadamu atakufa,
Hakubatilishi fundisho kwamba Mungu anaouwezo wa Kufufua.
Hakubatilishi fundisho kwamba Yesu akija atakuta watu wengine wakiwa hai.
Hakubatilishi fundisho kwamba Mungu anaweza kumchukua mtu kwa sababu zake mwenyewe.
Hakubatilishi ukweli kwamba Wanadamu wanaweza kujitungia mapokeo na kuyapa hadhi sawa na bibilia ila ni uongo tu .
sasa tunajadili ya Bibilia, unayodai unasiri zake kuwa Mungu alidanganya aliposema alifanya Yote kwa siku sita na Ya saba akapumzika au alikuwa anawarubuni waisrael ili wasijue siri zake, naomba kwa unyenyekevu mwingi hizo siri.

usitake kujitaabisha kwa kujihalalishia mambo yaliyonje ya bibilia huku bibilia imesheheni majibu na formula za kila kitu.
 
Kusema Mungu ni zaidi ya mmoja ni kumshirikisha na ni dhambi. Na hii ndiyo inayotofautisha kati ya Imani ya Kiislamu na Imani zingine.
Ahahaaah.
Aisee!!!
Nafikiri leo kuna mtu humu jukwaani amekuambia kuna Mungu zaidi ya mmoja,lakini huyo mtu sio mimi Chief.
Usinichanganyie habari,mimi naamini Mungu ni mmoja tu.
 
Kwani uumbaji ni lazima viumbe vipya vipatikane? Hivi kwa mfano Genetic changes sio uumbaji? Evolution sio uumbaji?
unachanganya bibilia na makorokoro nje ya Bibilia mkuu. Ukiendelea hivyo utapoteza mwelekeo.
Mungu alimuumba Viumbe na Bwawa lililojaa genes ambazo zinaweza kutumika wakati wowote popote ili kiumbe kipambane na mazingira. Hakiwi Kiumbe kipya bali ni kiumbe hicho kubadilika tu. Hiyo jamaa wa evolution watasema ni evolution lkn sisi wa Uumbqji tutasema ni Uwezo wa Mungu wa Kuumbq kiumbe kikiwa na kila kitu, Kila tool ya kukisaidia kuexist.
Ukiona askari Jeshi wanatembea bila Bunduki mitaani haimaanishi hazipo, bali Mazingira yakihitaji Ziwepo utaziona kutoka kwenye maghara yao ya silaha. Haimaanishi zimeumbwa baada ya kusikika taharuki za Vita, ila zipo miqka yote.
Mkuu ukiendelea hivyo muda mchache ujao na wewe utakuwa team kiranga.
hahaha
 
Back
Top Bottom