Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

ubunifu wa miaka mamilioni ni tafrisi za kisasa za mamno ya Mungu, hasa watu wa dini walipojilazimisha kujipendekeza kwenye kila sayansi bila kujua pamoja na uzuri wake wote wanasayansi wanaoaminini hayo mamiaka milioni wanawachukia kabisa na kuwatenga wenzao wanasayansi wanaoamini uumbaji wa siku sita tu.
mmoja wao ni mvumbuzi wa MRI scanner, alinyimwa hadi tuzo ya nobel 2003 na akapewa jamaa mwingine.

Kuna watu wa dini nao wameingia kwenye huu mtego. Dunia inahamishwa kwa kasi kutoka katika original creation na kwa ujanja wa hali ya juu tunafanywa kuamini evolution theory.

Kama Kitabu Quran kimesema jambo ambalo Kaka yake Bibilia imeliweka sawa miaka mingi kabla yake. Basi pia ni habari njema katika hilo.

Hata kwenye sayansi tunapaswa kujua kuna mgawanyiko, wapo wanaoamini creation ya siku sita, na mainstream wanaoamini mamilioni.
 
"Hakika sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika"
Samahani Kiongozi,hiyo SISI inasimama kuwawakilisha wakina nani?
Mungu alishirikiana na nani kwenye uumbaji wa binadamu?
Nahitaji kuelewa,nitashukuru kama utanielewesha.
 
mkuu zitto junior
mada yako inazungumzia birthday ya dunia.
Radiometric dating haijawahi kutoa usahihi wa umri wa kitu based on its birthday.
hata kama ipo hapo UDSM tunaweza kuomba experiment hata moja inayoongesha hata mtoto wa Mbuzi kazaliwa leo, akawekwa kwenye cage baada ya mwaka akapimwa ikathibitika anamwaka hata mmoja.

Tukikimbilia kwenye mamilioni ambayo hayana ushahidi, wala hakuna wa kuulizwa ambaye atatumika kama ushahidi wa jibu kuna uwezekano kudanganywa.
Labda kama wapo maarchealogists, Paleantologists na geologists humu waje watusaidie.
 
Dunia ina umri 0.00000000000000000000000000000000001microtrilosecond
Yap wewe ndio kila kitu

Waumini wa Mungu kitabu wanaamini kwenye time travel mwenye upako na aende arudi na majawabu
 
mkuu wanasayansi umetumia kama kokoro.
unaweza kuchanganua wanasayansi gani, maana sio wote wanaoamini hayo.
wapo creation scientist mamia ulimwenguni wanaamini katika 24 hrs day creation.
Newton aliamini.
Galileo aliamini.
Johan Kepler, Boyle, M. Faradays etc
na wengine wengi wa kisasa wanaamini.
Wapo wa creationscience UK wanahadi Lab ya kuthibitisha kuwa dunia ni changa kabisa kwa mujibunwa bibilia.

changanua vizuri mkuu ili uelewa uwe sawia
Pia kama Muumini wa Neno la Mungu, Unapaswa kuwa makini na kila kinachotoka kwa wanasayansi sio kila wanachosema ni sahihi kulingana na biblical basis. Mfano leo wanasema Ushoga ni matokeo ya Vinasaba. Watu wa Mungu wanaoamini kila kitu cha mwanasayansi wajiandae kuhalalisha ushoga kwa vizazi vyao maana umehalalishwa maabara ya wanasayansi wanaowapenda na kuamini kila wanachosema.
Basisi ya Research nyingi ninabsence ya Mungu, hivyo sio tusiamini bali wanaweza kuja na conclusion inayopromote upingwaji wa Mungu. Hivyo wanadini wanaouwaunga mkono itabidi wakubaliane nao ili kudumisha upenzi wao.

Haya Yote yanatutaka tuwe makini siontupuuzekila kitu, ila pembeni Bibilia pembeni science as a tool of exploring creation.
Ndivyo alivyoamini Galileo, corpenicos na wakagundua mambo makubwa ya ukweli kutoka katika uumbaji wa Mungu.

Pia kama mkuu Sala na Kazi alivyotoa hoja, kwa sababu science ni progressive kila siku wanavumbua mapya wanaweza kuvumbua kile ambacho tunakisema pia, ingawa trend haionyeshi hilo.
 

Fungu la kwanza hapo chini linalotoka kitabu cha Mwanzo 1, linasema wazi kabisa kuwa Mungu alianza akaumba Mbingu na Nchi kwanza halafu ukapita muda ambao hatujaelezwa ni muda gani, halafu ndiyo akafanya yale yote yanayoelezwa kuanzia fungu la 3.

Kwa hiyo ieleweke wazi kuwa
MOJA Alichofanya Mungu kinachoelezwa kuanzia Mwanzo 1:3 na kuendelea si uumbaji bali ilikuwa ni urekebishaji, nyongeza vikiambatana na upambaji wa kile ambacho tayari alikuwa aameshaumba huko nyuma.
MBILI Mungu huwa hahitaji kitu phsical katika uumbaji, huwa anatamka tu halafu kilichokuwa hakipo kinakuwepo. Ukiona anatamka kwa kitu kitu phsical, ujue hapo haumbi ila anafanya marekebisho, yaani modification.
TATU Aliwaumba Adam na Hawa kwa kutamka wakiwa ni roho zisizokuwa na mwili ndani ya NAFSI MOJA, baadaye tena akawafanyia marekebisho kwa kufinyanga udongo akawapa miili.Huu udongo ulikuwepo kabla ya watu hawa, Mungu alikuwa ameshauumba huko nyuma
NNE Kutokana na hoja hizo hapo juu,Mungu hakuumba ulimwengu kipindi anawaumba Adam na Eva ila ulimwengu ulikuwepo tangu kipindi kirefu huko nyuma. Hii inathibitishwa na hilo fungu la Mwanzo 1:1 na na mengine yote yanayofuata kwenye sura hiyo
TANO. Muumini yeyote wa dini anayeaamini kuwa ulimwengu una miaka 6000 hayuko sahihi, bali tangu kuumbwa Adam ndiyo miaka 6000. Ulimwengu ulikuwepo kabla ya Adam
SITA Wana Sayansi wanaofanya tafiti kwa mfano za miamba na kugundua kuwa kuna miamba ina miaka mabillion tangu kuwepo kwake, WAKO SAHIHI NA HAWAPINGANI NA BIBLIA, kwa sababu Biblia yenyewe inathibitisha kuwepo kwa ulimwengu kabla ya Adam, kwenye hilo fungu la Mwanzo 1:1
SABA Muumini yeyote ambaye alikuwa na taarifa zisizo sahihi kuwa ulimwengu uliumbwa miaka 6000 iliyopita, naomba arejee tena kusoma Mwanzo 1:1 na atusaidie kutoa tafsiri upya, kama pengine kama haya niliyoyasema hapo juu anadhani hayako sahihi

1Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.
6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.
7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;
15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo.
16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.
17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
23 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
 
Mbona sekta nyingi tu biblia na Quran vinafanana, hasa visa. Sema mjinga aliyekuja kututofautisha ndiyo kazingua Tungekuwa wamoja.
 
Ngumu kupata jawabu halisi wengi wanakadiria na hata makadirio yenyewe tu yanautata
 
Mkuu asante kwa hoja.
hoja hii aliyoleta mkuu inachangamoto kubwa sana na inaleta uelewa mpya na migogoro hata kwa waumini wa bibilia.
wengi hata wa imani moja wanaibuka na kutofautiana pia.

Makasisi/wachungaji na wanatheolojia wengi wa kisasa wanabishana na kutofautiana katika hili wengine wakiungana na wanasayansi wanaoamini miyo miaka mamilioni wengine wakiungana na wanasayansi wanaosema ni miaka kama 6000 tu.

Msingi wa hoja yangu katika hili. Hatujui ilichukua muda gani kwenye mwanzo 1:1 au Mwanzo 1:3
Ila kabla hatujaruka bibilia na kuwauliza wanasayansi tukiiuliza bibilia inasema wazi kupitia Mungu huyohuyo aliyehusika kuumba kuwa yote yalifanyika kwa siku sita. Na Kumbukumbu ya siku hizo sita ilimtofautisha Mungu wa waisrael na Miungu mingine yoyote iliyokuwepo enzi zile. Na wakristo wanamuamini Yesu, Na Bibilia Inasema Hakuna kilichofanyika pasipo yeye Yesu, Basi naamini hata Yesu anatutaka Turudi kuheshimu Ufafanuzi wa Bibiliq kqbla ya sayansi.

Kwa nini?
Sayansi Inabadilika, na Bado inagap Kubwa la ufahamu kuliko ilivyovifahamu, Haina Vifaa reliable undebatable vya kutatua utata huu bila shida.
Ila Bibilia Inatutaka tuiamini kama Ultimate truth na ukweli usiobadilika hadi mwisho hivyo inatoa mwanya mpana wa kujadili pia. Ndio maana naamini mada hizi zote zinaibuka na zitaendelea kuibuka kwa sababu tuliutupilia mbali ule mpango wa Ile amri Ya sabato ambayo inawataka wanadamu wakumbuke 6 literal days of creation na sio mamilioni.

maoni mkuu, tunaweza kupingana bila kukwanguana piq. Maana haya mambo sio yetu ni Ya yeye aliyeumba.
 
"Hakika sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika"
Samahani Kiongozi,hiyo SISI inasimama kuwawakilisha wakina nani?
Mungu alishirikiana na nani kwenye uumbaji wa binadamu?
Nahitaji kuelewa,nitashukuru kama utanielewesha.

Ahsante kwa swali lako zuri: Nina lako linasadifu vizuri - Ngumbaru.
Ngoja tumuulize Mwenyezi Mungu mwenyewe aliye Mtaalamu na mwanzilishi wa Lugha:

"Na hatukumtuma kabla yako mtume yeyote Ila tulimfunulia ya kwamba Hapana mungu Ila MIMI. Basi niabuduni MIMI tu". (Qur'an 21:25)

"Hakika MIMI ndiye Mwenyezi Mungu, Hapana mungu ila MIMI tu. Basi niabuduni MIMI na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka MIMI." (Qur'an 69:14).

Naamini umeelewa vizuri kakangu. Kama hujaelewa naomba karibu uulize tena.

NB: Kwa msaada Zaidi kama wewe ni Mkristo nenda kasome mwanzo pale Mungu anaposema "Natufanye MTU kwa mfano WETU. ……..Kisha Mungu akamuumba MTU kwa mfano WAKE.
SIYO KWA MFANO WAO.
 
Wamepima kuanzia Adam alipoumbwa!
Mbona tunasoma humu ndani Kuwa Dunia ilikuwa ina watu kabla ya Ujio wa Adamu?

Samahani kama nitakuwa sijaeleweka maana sipo vizuri kwenye hizi mambo.
Adam ni mapokeo ya Wayahudi tu.

Zamani, watu walikuwa wanaishi tofauti tofauti. Hawachangamani sana.

Katika kuishi tofauti huko, hawakuwahesabu watu walioishi mbali nao kama watu.

Wayahudi wakajitungia hadithi yao ya mtu wa jwanza. Ndiyo huyo Adam.

Adam hawezi kuwa mtu wa kwanza, kwa sababu hata hadithi ya mtoto wake Cain alipofukuzwa Eden, alikimbia pembe i akakutana na watu.

Sasa kama Adam alikuwa mtu wa kwanza, huko nje ya bustani ya Eden watu walifikaje?

Pia, kisayansi, watu walitokea Africa maelfu na maelfu ya miaka kabla ya habari za Adam miaka 6000 iliyopita.

Sasa unakuwaje watu watoke Afrika maelfu na maelfu ya miaka iliyooita, halafu Adam awe mtu wa kwanza kaumbwa miaka 6000 iliyopita?

Kama dunia imeumbwa miaka 6000 iliyopita, mbona ina mawe yenye mamilioni ya miaka?

Mbona ina milima iliyofanyika mamilioni ya miaka?
 
sio kweli
Ukweli ni upi kaka. He, Dunia kama part and parcel ya solar system sio zao la Big Bang?

"Have those who disbelieved not considered that the heavens and the earth were a joined entity, and We separated them and made from water every living thing? Then will they not believe?" (Qur'an 21:30)
 
Hivi umeelewa kweli swali langu?
Au username yangu imekuzuzua,kiasi kwamba ukashindwa kabisa kusoma swali vizuri?
 
Mbona sekta nyingi tu biblia na Quran vinafanana, hasa visa. Sema mjinga aliyekuja kututofautisha ndiyo kazingua Tungekuwa wamoja.
Yanayofanana na Bibilia huwa nayakubali, yanayotofautiana ,Bibilia ni Sahihi kuliko hiyo quran. Maana Bibilia imeanza kuyaandika kabla ya quran.
Binafsi huo ndio ufahamu wangu, unaweza usiwe mzuri sana.
 
Hivi umeelewa kweli swali langu?
Au username yangu imekuzuzua,kiasi kwamba ukashindwa kabisa kusoma swali vizuri?
Na Je, umesoma post yangu ukaielewa vizuri kabla ya kua-assume kuwa nimezuzuliwa na jina lako??.
Hebu some vizuri kisha utafakari halafu onyesha ni wapi hujaelewa. Nimekuelimisha kama mwanafunzi usiyejua taawili ya maana ya Lugha.
 
Mkuu shukrani kwa kudadavua vizuri kabisa juu ya credibility ya vipimo vya kisayansi katika lugha inayoeleweka ningependa mkuu mitale na midimu aione hii atupe maoni yake.
 
Yanayofanana na Bibilia huwa nayakubali, yanayotofautiana ,Bibilia ni Sahihi kuliko hiyo quran. Maana Bibilia imeanza kuyaandika kabla ya quran.
Binafsi huo ndio ufahamu wangu, unaweza usiwe mzuri sana.

Unaweza kuwa sahihi lakini Jeremia 8:8 inaweza kukufundisha kinyume cha ukweli. Na hapo ndipo huyo au hao wajinga walianza kupotoa na kukoroga mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…