Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli Adam ndiye mwenye umri wa miaka 6,000, na tukumbuke kuwa aliumbwa baada ya viumbe wote wengine kuwa wameumbwa baada ya miaka mingi...Hoja ya kuwa dunia ina miaka takribani 6000 sio kweli kwasababu kuna baadhi ya maandiko yanasema kuna viumbe walipata kuishi duniani kabla ya Adam kuumbwa.Mungu aliwaondoa viumbe hao baada ya kuleta machafuko ikapita million years ndo akaja kuumbwa Adam.
Nadhani kutumia bible pekee ili kuelezea umri sahihi wa dunia ni kutokuvitendea haki vitabu vingine
dunia iliumbwa siku sita. hizo miaka mingi tunazitolea wapi mkuu.Ni kweli Adam ndiye mwenye umri wa miaka 6,000, na tukumbuke kuwa aliumbwa baada ya viumbe wote wengine kuwa wameumbwa baada ya miaka mingi...
Rudia kusoma maandiko (Biblia) pengine utaelewa. 2 Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu...dunia iliumbwa siku zita. hizo miaka mingi tunazitolewa wapi mkuu.
au tunataka kuwa evolutionist christians
Alikuwa anazungumzia kwa Bwana " Mbinguni", Ila yeye aliyeiumba dunia, alifafanua wazi kuwa aliiumba siku sita mkuu.Rudia kusoma maandiko (Biblia) pengine utaelewa. 2 Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu...
Je, unadhani siku saba zinazotajwa zilikuwa na saa 24 kama siku tuzijuazo leo?...
Pia tafakari mstari huu: Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima."...dunia iliumbwa siku sita. hizo miaka mingi tunazitolea wapi mkuu.
au tunataka kuwa evolutionist christians
Pia jiulize kuhusu andiko hili: Mwanzo 1:2 “nayo nchi ilikuwa tupu tena ukiwa”. Hapa hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Sura hii, kwamba Mungu alikusudia kufanya jambo duniani. Alikusudia kuitengeneza tena ili kusudi ikaliwe na watu iweze kuleta sifa na utukufu kwake...Alikuwa anazungumzia kwa Bwana " Mbinguni", Ila yeye aliyeiumba dunia, alifafanua wazi kuwa aliiumba siku sita mkuu.
'' Kwa kuwa kwa siku sita, Mungu alizifanya mbingu na dunianna vyote vilivyomo'' Mungu (kutoka 20)
sioni sababu ya kufafanua jambo ambalo muhusika alishalifafanua.
Vinginevyo unataka kumsuta Mungu na kumfanya Muongo kadanganya mara Mbili, kwenye uumbaji na Kwenye mbao za Mawe kitu ambacho sio kweli.
Mathayo 6:34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”Pia tafakari mstari huu: Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima."...
Yeye aliyeumba na kufanya yote hayo na huo utupu na ukiwa alisema vyote vilifanyika kwa siku sita. Hekima yoyote nje ya Kauli za Mungu zilizo wazi lazima zitufikirishe ili turejee kauli za Mungu mwenyewe.Pia jiulize kuhusu andiko hili: Mwanzo 1:2 “nayo nchi ilikuwa tupu tena ukiwa”. Hapa hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Sura hii, kwamba Mungu alikusudia kufanya jambo duniani. Alikusudia kuitengeneza tena ili kusudi ikaliwe na watu iweze kuleta sifa na utukufu kwake...
Haya mkuu, lakini siku zote mimi ni mwanafunzi, nitaendelea kujifunza kwa kuwa sitaki kukaririshwa...Mathayo 6:34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”
Hilo mkuu mbona halina uhusiano na uumbaji na Yesu alilifafanua tunaoaswa kuishi kwa siku moja, hata kama unamipango ya miaka mia.
Kuhusu Uumbaji Mungu alilifafanua kwa watu wake wa agano waisrael sio kwa maneno bali kwa maandishi kuwa Dunia iliumbwa kwa Siku sita za kawaida. na akwapa maelekezo kwa mujibu wa jinsi alivyoumba.
Mimi nqqmininkufuta hii amri imepelekea wanadamu kupeperushwa na kila upepo wa maarifa na hadithi za wanaojiita wasomi. Sasa kuna theory zaidi ya kumi kuhusu haya mbili tu za mwanzo.
Inawezekana, lakini hatukuambiwa tukariri kila kilichoandikwa (maana kila wanavyozidi kutafsiri kuna maana zinapotea au maneno mengine kuachwa), bali tunatakiwa tutafakari neno ili kuiona kweli: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana"...Yeye aliyeumba na kufanya yote hayo na huo utupu na ukiwa alisema vyote vilifanyika kwa siku sita. Hekima yoyote nje ya Kauli za Mungu zilizo wazi lazima zitufikirishe ili turejee kauli za Mungu mwenyewe.
Mungu alikuwa na kusudi kubwa sana kutaka wanadamu wakumbuke uumbaji. Leo wanaibuka watu wanahamisha magoli wanajikumbusha mambo yao na kujikuta wakisombwa na kila nadharia zisizo na nanga katika bibilia.
sawa mkuu. katika nadharia za kisomi kuhusu bibilia sisi wengine tumeamua kusimamia maneno mepesi tu yasiyohitaji phd kung'amua.Haya mkuu, lakini siku zote mimi ni mwanafunzi, nitaendelea kujifunza kwa kuwa sitaki kukaririshwa...
Kumbuka asilimia kubwa ya Agano Jipya zikiwemo nyaraka na Injili imeandikwa na PhDs (Paulo na Luka), sasa sijui hapa unasemaje?...Pamoja na kuchangamsha bongo na kufikiri kwa njia ya bibilia, umakini unahitajika hasa tunapojadili mambo ambayo Mungu ameshayafafanua kwenye bibilia hiyohiyo. Tunakuwa tumetua mizigo mingi mno. Pia kumbuka pHDs ndio waliomkataa Yesu aliyekuwa kwenye magombo waliyoyashika, hakuna muujiza kuona PhD anapotosha kwa jina la bibilia.
Sibezi ila nasisitiza umakini katika kupokea kila jambo.
naunga mkono hoja. hatuoaswi kukariri.Inawezekana, lakini hatukuambiwa tukariri kila kilichoandikwa (maana kila wanavyozidi kutafsiri kuna maana zinapotea au maneno mengine kuachwa), bali tunatakiwa tutafakari neno ili kuiona kweli: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana"...
Askofu huyo anaweza kuwa sahihi lakini hapo hapo asiwe sahihi, kama jambo la uumbaji amelichukulia kimwili basi kakosea sana, lakini kama kiroho yupo sahihi. Maana wakati Mungu anamuumba mtu (mwanamke na mwanaume) kama ilivyoandikwa kwenye Mwanzo 1:26-27 hakuwa akiumba mwili bali roho (Uungu ulio ndani yetu ambao hauna jinsia). Mwanzo 1:26-27 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba...naunga mkono hoja. hatuoaswi kukariri.
hatupaswi kutokutafakari maana ni agizo la Mungu.
Lkn tafakari zote zinapaswa kuturudisha katika Bibilia sio kutuondoa katika bibilia.
na njia pekee ya kurudishwa katika bibilia ni kutafakari wazo la kitabu kimoja kwa kushirikisha mafungu ya vitabu vingine na waandishi wengine wanaofafanua jambo hilohilo.
Kutafakari kafungu kamoja bila kuheshimu fafanuzi nyingine kumepelekea askofu msomi wa theolojia wa kanisa Moja huko US kusema, Mungu aliwaumba adam na hawq kwq mfano wake, na kwa sababu Mungu hana jinsia hivyo mwanamke anaweza kuwa mwanamke na wakati huohuo akawa mwanaume. au mwanaume kuwa mwanaume na wakati huohuo anaweza kuwa mwqnamke maana alisema atamtaftia msaidizi wa kufanana nae.
na hilo fungu la mwqzo na uumbaji limegeuzwa kuwa geti la kuhalalishia ushoga na usagaji makanisani.
Pioneers wake ni wasomi na wanatheolijia hao hao wanaotafuta maana ambazo eti sisi tusiobobea hatufahamu.
nasisitiza taadhari ili kutafakari huko kusije kutupotosha, bali kutufanye tumuamini Mungu na maneno yake kwa kina.