Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

mkuu mimi ni muumini wa Young earth creation.
Pia ninaamini Bibilia iliumbwa kwa siku sita '' lateral days '' kwa ushahidi wa bibilia yenyewe, bila mafumbo, Maana Mungu mwenyewe aliyeumba aliweka clarification ya hilo.
Pia umefanya utafiti ambao umeacha mgogoro mkubwa hasa kwenye hitimisho lako la kuwahojinwanatheolojia maana umehojinwa upande mmoja.

Wapo wanatheolojia wengine ni maprofesa na phd na bado wanaamini Young earth creation, na 7 lateral days.
Wapo wanasayansi wengi wakristo wanaoamini dunia kuwa na miaka takribani elfu sita, na kuumbwa kwa siku saba za kila siku masaa 24.

Kwa nyongeza ili mada ijae vizuri. Kuna nadharia kama 9 juu ya uumbaji kutoka kwa wanavyuoni mbalimbali.
1: Theistic evolution
dunia iliumbwa kwa mchanganyiko wa evolution katika kutimiza uumbajinhuo.
2:GAP theory AU RESTORATION THeory
Hawa wanaamini dunia iliumbwa na baada ya kumalizika kukatokea vita kati ya shetani na Mungu, na baada ya vita Mungu ikabidi aumbe upya maana vitu vilikuwa vimeharibiwa na vita. Na kuumba huko upya ndio huko kwa mwanzo 1,2 na wwnamafungu mengine kuunga mkono hoja zao.

3Day AGE THEORY
Hawa wanaamini Mungu aliposema siku,hakumaanisha siku kama 24hrs hawa wanaamini alimaanisha zama, yaani mamilioni ya miaka.

4:Apparent Age Theory
Hawa wanaamini kama Mungu alimuumba adamu akiwa mtu mzima, basi atakuwa aliumba vitu vingine vyote vikiwa vizee kabisa sio vipya. Hawa wqnabase katika gramatical historical interpretation of the bible.

5Punctuated 24Hrs Theory
Hawa wanajaza mamilioni ya miaka katikati ya siku moja na siku moja. na nadhani wataungana na wqle uliowaelezea pale juu.

6:Scientific creationism
Hwa wanaamini kupitiq matokeo ya mafuriko ya nuhu kuwa dunia inamiaka kama 7000 -15000
wanaibuka kama wanasayansi wanaojaribu kuwapinga wanasayansi wenzao wanaoamini katika mamilioni ya miaka.
kwa kutumia system yao, wanaamini waumini wanapaswa kuamini mwanzo 1 ilikuwa ni matukio halisi sio fumbo.

7: 24 Hrs interpretation na Mimi naamini Hii.
Hawa wanaamini dunia imeumbwa kwa siku za kawaida sita tu, na kwa kuangalia vizazi vya bibilia na matukio ya kihistoria dunia inatrkribani miaka 6000 japo hatuwezi kujua tarehe na mwezi kama huyo mdau.
Ile ilikuwa ni wiki mojanya kawaida, na sisi watafrisi wa bibilia kiubichiubichi bila kuchakachua kwa mgongo wa kusingizia mafumbo tunarudi kwenye amri za Mungu miaka baadae, Mungu anasema na Kuandika alifanya Yote kwa SIKU SITA. Hakukuwa na fumbo wala kujificha na akawapa formula ya maisha ya kufanya kazi siku sita na kupumzika moja.

8:Historical Creationism
Hawa wanaamininDunia na maambo yote yaliumbwa na kumalizwa Mwanzo1:1 , hayo mambo mengine yote ya siku zita yalikuwa ni maandalizi tu ya bustani ya edeni.

9: Evolutionists
hawa wanapinga uumbaji wanakwenda kwenye mabing bang theory na mengine. nao wamegawanyikq makundi kama sita hivi.

Hivyo mkuu kwa mtazamo wangi mjadala huu ni mpana na mzito.

Ila kwa Bibilia kujitafsiri yenyewe. Binafi naamini ni siku wiki ya kawaida tu. Na Nadharia nyingine zote ni watu wa bibilia kuamua kujiunga na Evolutionists moja kwa moja bila kujua au kwa kujua. Kabla ya miaka kadhaa zote hizo zilikuwa hazipo. Wiki imekuwepo kihistoria kabla ya watu wengi kuvurugwa na evolution na baada ya kuibuka imani kwamba bibilia haijaandikwa moja kwa moja bali kuna siri ndani yake. Mfano Jamaa mmoja wa alexandira alichanganya imani ya bibilia na philosophy za kigiriki na kuja na theory kwamba kila kitu cha bibilia kina maana karibu sita za kina sana ambazo wajuzi wachachet tu ndio wanaweza kuzing'amua, ila hoehae hatutaweza. Hizi dhana zimeendelea kudumu hata leo na kuwafanya wasomi na wachimbuzi wa maandiko kinadharia kujikuta wanayapinga nankutafuta vitu vigumu huku wakipishana na mampo mepesi yaliyo wazi.
 
Hoja ya kuwa dunia ina miaka takribani 6000 sio kweli kwasababu kuna baadhi ya maandiko yanasema kuna viumbe walipata kuishi duniani kabla ya Adam kuumbwa.Mungu aliwaondoa viumbe hao baada ya kuleta machafuko ikapita million years ndo akaja kuumbwa Adam.
Nadhani kutumia bible pekee ili kuelezea umri sahihi wa dunia ni kutokuvitendea haki vitabu vingine
Ni kweli Adam ndiye mwenye umri wa miaka 6,000, na tukumbuke kuwa aliumbwa baada ya viumbe wote wengine kuwa wameumbwa baada ya miaka mingi...
 
Ni kweli Adam ndiye mwenye umri wa miaka 6,000, na tukumbuke kuwa aliumbwa baada ya viumbe wote wengine kuwa wameumbwa baada ya miaka mingi...
dunia iliumbwa siku sita. hizo miaka mingi tunazitolea wapi mkuu.
au tunataka kuwa evolutionist christians
 
dunia iliumbwa siku zita. hizo miaka mingi tunazitolewa wapi mkuu.
au tunataka kuwa evolutionist christians
Rudia kusoma maandiko (Biblia) pengine utaelewa. 2 Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu...
Je, unadhani siku saba zinazotajwa zilikuwa na saa 24 kama siku tuzijuazo leo?...
 
Alikuwa anazungumzia kwa Bwana " Mbinguni", Ila yeye aliyeiumba dunia, alifafanua wazi kuwa aliiumba siku sita mkuu.

'' Kwa kuwa kwa siku sita, Mungu alizifanya mbingu na dunianna vyote vilivyomo'' Mungu (kutoka 20)
sioni sababu ya kufafanua jambo ambalo muhusika alishalifafanua.
Vinginevyo unataka kumsuta Mungu na kumfanya Muongo kadanganya mara Mbili, kwenye uumbaji na Kwenye mbao za Mawe kitu ambacho sio kweli.
 
Pia jiulize kuhusu andiko hili: Mwanzo 1:2 “nayo nchi ilikuwa tupu tena ukiwa”. Hapa hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Sura hii, kwamba Mungu alikusudia kufanya jambo duniani. Alikusudia kuitengeneza tena ili kusudi ikaliwe na watu iweze kuleta sifa na utukufu kwake...
 
Pia tafakari mstari huu: Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima."...
Mathayo 6:34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”
Hilo mkuu mbona halina uhusiano na uumbaji na Yesu alilifafanua tunaoaswa kuishi kwa siku moja, hata kama unamipango ya miaka mia.

Kuhusu Uumbaji Mungu alilifafanua kwa watu wake wa agano waisrael sio kwa maneno bali kwa maandishi kuwa Dunia iliumbwa kwa Siku sita za kawaida. na akwapa maelekezo kwa mujibu wa jinsi alivyoumba.
Mimi nqqmininkufuta hii amri imepelekea wanadamu kupeperushwa na kila upepo wa maarifa na hadithi za wanaojiita wasomi. Sasa kuna theory zaidi ya kumi kuhusu haya mbili tu za mwanzo.
 
Pia jiulize kuhusu andiko hili: Mwanzo 1:2 “nayo nchi ilikuwa tupu tena ukiwa”. Hapa hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Sura hii, kwamba Mungu alikusudia kufanya jambo duniani. Alikusudia kuitengeneza tena ili kusudi ikaliwe na watu iweze kuleta sifa na utukufu kwake...
Yeye aliyeumba na kufanya yote hayo na huo utupu na ukiwa alisema vyote vilifanyika kwa siku sita. Hekima yoyote nje ya Kauli za Mungu zilizo wazi lazima zitufikirishe ili turejee kauli za Mungu mwenyewe.
Mungu alikuwa na kusudi kubwa sana kutaka wanadamu wakumbuke uumbaji. Leo wanaibuka watu wanahamisha magoli wanajikumbusha mambo yao na kujikuta wakisombwa na kila nadharia zisizo na nanga katika bibilia.
 
Mathayo 6:34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”
Hilo mkuu mbona halina uhusiano na uumbaji na Yesu alilifafanua tunaoaswa kuishi kwa siku moja, hata kama unamipango ya miaka mia.

Kuhusu Uumbaji Mungu alilifafanua kwa watu wake wa agano waisrael sio kwa maneno bali kwa maandishi kuwa Dunia iliumbwa kwa Siku sita za kawaida. na akwapa maelekezo kwa mujibu wa jinsi alivyoumba.
Mimi nqqmininkufuta hii amri imepelekea wanadamu kupeperushwa na kila upepo wa maarifa na hadithi za wanaojiita wasomi. Sasa kuna theory zaidi ya kumi kuhusu haya mbili tu za mwanzo.
Haya mkuu, lakini siku zote mimi ni mwanafunzi, nitaendelea kujifunza kwa kuwa sitaki kukaririshwa...
 
Yeye aliyeumba na kufanya yote hayo na huo utupu na ukiwa alisema vyote vilifanyika kwa siku sita. Hekima yoyote nje ya Kauli za Mungu zilizo wazi lazima zitufikirishe ili turejee kauli za Mungu mwenyewe.
Mungu alikuwa na kusudi kubwa sana kutaka wanadamu wakumbuke uumbaji. Leo wanaibuka watu wanahamisha magoli wanajikumbusha mambo yao na kujikuta wakisombwa na kila nadharia zisizo na nanga katika bibilia.
Inawezekana, lakini hatukuambiwa tukariri kila kilichoandikwa (maana kila wanavyozidi kutafsiri kuna maana zinapotea au maneno mengine kuachwa), bali tunatakiwa tutafakari neno ili kuiona kweli: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana"...
 
Asante tena kwa chakula hiki kitamu cha ubongo
Kabla ya kufikia kufanya ulinganifu na sayansi.. Kibiblia yenyewe naweza kusema umri (kwa tafsiri ya miaka) wa dunia una siri, fumbo ama mkanganyiko wa kipekee mno
1.kabla ya Kristo hesabu ya namba ilianza 0 kurudi nyuma, na baada ya hapo ndio tukawa tunaanzia 0 kwenda mbele 9876543210123456789..... Hapa huwezi kupata jibu halisi kwakuwa utatumia formula gani kazi ya hizo mbili?

2. Tunaambiwa kibiblia kwamba miaka 1000 kwa Mungu ni sawa na siku moja kwa mwanadamu na kinyume chake.... Sasa tafsiri sahihi ya muda kwa Mungu ni ipi?
 
Haya mkuu, lakini siku zote mimi ni mwanafunzi, nitaendelea kujifunza kwa kuwa sitaki kukaririshwa...
sawa mkuu. katika nadharia za kisomi kuhusu bibilia sisi wengine tumeamua kusimamia maneno mepesi tu yasiyohitaji phd kung'amua.
Mfano, Mungu anasema aliumba mtu mme na mke, Adam Na hawa. Miaka mingine mingi ndani ya bibilia hiyohiyo Yesu akarudia msisitizo huo, Mitume akiwemo paulo akarudia kauli hiyohiyo.
Leo wanaibuka mitume wa kisasa na wasomi wanakambia Mungu aliumba watu wengi mno sio wawili tu.
Sasa tuwaamini wao au Yesu (Pasipo yeye hakikufanyika kitu) au Paulo (Nilifundishwa moja kwa moja na Yesu Kwa Ufunuo).

Pamoja na kuchangamsha bongo na kufikiri kwa njia ya bibilia, umakini unahitajika hasa tunapojadili mambo ambayo Mungu ameshayafafanua kwenye bibilia hiyohiyo. Tunakuwa tumetua mizigo mingi mno. Pia kumbuka pHDs ndio waliomkataa Yesu aliyekuwa kwenye magombo waliyoyashika, hakuna muujiza kuona PhD anapotosha kwa jina la bibilia.

Sibezi ila nasisitiza umakini katika kupokea kila jambo.
 
Kumbuka asilimia kubwa ya Agano Jipya zikiwemo nyaraka na Injili imeandikwa na PhDs (Paulo na Luka), sasa sijui hapa unasemaje?...
 
Inawezekana, lakini hatukuambiwa tukariri kila kilichoandikwa (maana kila wanavyozidi kutafsiri kuna maana zinapotea au maneno mengine kuachwa), bali tunatakiwa tutafakari neno ili kuiona kweli: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawa sawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana"...
naunga mkono hoja. hatuoaswi kukariri.
hatupaswi kutokutafakari maana ni agizo la Mungu.
Lkn tafakari zote zinapaswa kuturudisha katika Bibilia sio kutuondoa katika bibilia.
na njia pekee ya kurudishwa katika bibilia ni kutafakari wazo la kitabu kimoja kwa kushirikisha mafungu ya vitabu vingine na waandishi wengine wanaofafanua jambo hilohilo.

Kutafakari kafungu kamoja bila kuheshimu fafanuzi nyingine kumepelekea askofu msomi wa theolojia wa kanisa Moja huko US kusema, Mungu aliwaumba adam na hawq kwq mfano wake, na kwa sababu Mungu hana jinsia hivyo mwanamke anaweza kuwa mwanamke na wakati huohuo akawa mwanaume. au mwanaume kuwa mwanaume na wakati huohuo anaweza kuwa mwqnamke maana alisema atamtaftia msaidizi wa kufanana nae.
na hilo fungu la mwqzo na uumbaji limegeuzwa kuwa geti la kuhalalishia ushoga na usagaji makanisani.
Pioneers wake ni wasomi na wanatheolijia hao hao wanaotafuta maana ambazo eti sisi tusiobobea hatufahamu.

nasisitiza taadhari ili kutafakari huko kusije kutupotosha, bali kutufanye tumuamini Mungu na maneno yake kwa kina.
 
It sound to me, vyote (Biblia na sayansi ) vipo swa, sijaizungumzia Kurani kwasababu sina ujuzi nayo. Nitafafanua. Kama ukisoma Biblia kwa haraka haraka utagundua dunia (kwa mujibu wa Biblia) ina umri wa miaka 6000 kama ulivyo onesha hapo mkuu Zitto Jr, but twendeni taratibu kwenye Biblia hiyo hiyo, Hivi ni lini Mungu alimtupa shetani duniani? Kabla au baada ya kumuumba Adamu na Hawa!? The Bible doesn't say anything about it, ingawa ukisoma kwa utulivu sana utagundua shetani alitupwa even before Adam and Eve, why, yule shetani aliyeingia ndani ya nyoka how did he know kwamba Mungu aliweka marufuku ya wao kula TUNDA la UJUZI wa mema na mabaya!? Hilo moja, lakini jambo la pili ni hili, ndani ya Biblia hasa wakati ule wa gharika la Nuhu (hilo pia mleta UZI umeligusia) kuna viumbe wanaitwa Wanefiri, tena Biblia inasema "...nao wanefiri walikuwepo wakati huo". Swali, hao wenefiri walitokana na nini? Lini waliumbwa au wanatokana na mzazi yupi kati ya wale watoto 2 wa Adam? Again the Bible is silence about it? Hope Mungu aliiadhibu dunia kabla ya kizazi cha Adam na Hawa and then akaamua kuumba upya,uthibitisho mwingine wa hilo ni hu, baada ya Mungu kuiadhibu dunia kwa maji/gharika; inaonekana Mungu ni kama aliona huruma with what he has did, akasema hivi, "....sitaiangamiza dunia tena kwa maji" na akaweka agano ambalo hadi leo tunaliona, ule UPINDE wa mvua!
 
Tukizungumzia nadharia ya kidini.....Dunia ilikwepo miaka mingi hats kabla ya Adam.
Pale mwanzo Dunia ilikuwa kiwa tena tupu Na roho ya Bwana ilitulia juu yake..
Hapa tunapata wazo Dunia haikuwnza immediately Na Adam..nooooo. Ilikuwepo miaka kadhaa ndo Mungu akaona aweke viummbe
 
naunga mkono hoja. hatuoaswi kukariri.
hatupaswi kutokutafakari maana ni agizo la Mungu.
Lkn tafakari zote zinapaswa kuturudisha katika Bibilia sio kutuondoa katika bibilia.
na njia pekee ya kurudishwa katika bibilia ni kutafakari wazo la kitabu kimoja kwa kushirikisha mafungu ya vitabu vingine na waandishi wengine wanaofafanua jambo hilohilo.

Kutafakari kafungu kamoja bila kuheshimu fafanuzi nyingine kumepelekea askofu msomi wa theolojia wa kanisa Moja huko US kusema, Mungu aliwaumba adam na hawq kwq mfano wake, na kwa sababu Mungu hana jinsia hivyo mwanamke anaweza kuwa mwanamke na wakati huohuo akawa mwanaume. au mwanaume kuwa mwanaume na wakati huohuo anaweza kuwa mwqnamke maana alisema atamtaftia msaidizi wa kufanana nae.
na hilo fungu la mwqzo na uumbaji limegeuzwa kuwa geti la kuhalalishia ushoga na usagaji makanisani.
Pioneers wake ni wasomi na wanatheolijia hao hao wanaotafuta maana ambazo eti sisi tusiobobea hatufahamu.

nasisitiza taadhari ili kutafakari huko kusije kutupotosha, bali kutufanye tumuamini Mungu na maneno yake kwa kina.
Askofu huyo anaweza kuwa sahihi lakini hapo hapo asiwe sahihi, kama jambo la uumbaji amelichukulia kimwili basi kakosea sana, lakini kama kiroho yupo sahihi. Maana wakati Mungu anamuumba mtu (mwanamke na mwanaume) kama ilivyoandikwa kwenye Mwanzo 1:26-27 hakuwa akiumba mwili bali roho (Uungu ulio ndani yetu ambao hauna jinsia). Mwanzo 1:26-27 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba...

Uumbaji wa mwili umefafanuliwa kwenye Mwanzo 2:7 "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."... Hapa aliyeumbwa ni Adam pekee (mwanamume), na baadaye akapatikana Hawa: Mwanzo 2:21 "Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu."...
 
Back
Top Bottom