Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Kumbuka asilimia kubwa ya Agano Jipya zikiwemo nyaraka na Injili imeandikwa na PhDs (Paulo na Luka), sasa sijui hapa unasemaje?...
Luka hakuwa PHD bali Tabibu au medical doctor.
Kweli Paulo alikuwa PHD lkn katika kitabu cha 1 wakorintho 2 anasema Hekima anazofundisha sio za dunia hii, maana wenye hekima za dunia hii (PHDs) zingekuwa na maana wasingemsurubisha Yesu.

Sipingi wasomi maana wamesaidia mengi, Ila msomi ambaye anategemea nadharia na hajawabadilika moyo wake. Strength ya hoja zake ni courses alizosoma sio Uweza wa Roho mtakatifu katika kunyumbua maandiko anaweza kuwa mtu hatari sana. Ndio maana Paulo anasema hekima za dunia hii ni UPUMBAVU.


Hekima na PHD sisitupelekee kupotosha na kujipotosha bali situpelekee kuwa wanyenyekevu kwa mambo ya Mungu kama alivyoyaeleza kwenye maandiko.
Mwenyewe natamani Baadae kusoma hata kuwa Prof wa chochote nitakachopenda lkn hekima hizo zijengwe juu ya hekima ya milele ya neno la Mungu.

Usiogope kumpinga mtu kwa sababu ni professor au PHD mkuu hata kama anapotosha.
 
Askofu huyo anaweza kuwa sahihi lakini hapo hapo asiwe sahihi, kama jambo la uumbaji amelichukulia kimwili. Maana wakati Mungu anamuumba mtu (mwanamke na mwanaume) hakuwa akiumba mwili bali roho (Uungu ulio ndani yetu ambao hauna jinsia). Mwanzo 1:26-27 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba...
sio huyo tu wako wengi wengi na kila siku wengi wanaongezeka. wengine wanaunga mkono nadharia za Evolution kwa kupitia bibiliq, wengine wanavuruga mfumo wa Mungu wa uimbaji makusudi ili ipatikane nafasi ya kuweka mfereji wa kupitisha mambo ya kijinga na kiovu katika makanisa, jamii na misikiti. Mbeleko inayosaidia ni kiwa jamii imeshakuwa programmed kuwa jambo likisemwa na PHD au PROF ni kweli. Ufafanuzi ukitolewa na PHD wa theology basi huo ji sahihi bila shida.
Unaweza kuwa sahihi ila sio siku zote utakuwa sahihi.
Hata Petro alikuwa sahihi aliposema Yesu ni nani, lkn baadae kidogo akaingiwa na shetani akataka kupingana na mpango wa kifo cha Yesu, Yesu akamkemea rudi Nyuma ewe shetani. Hata PHD au msomi wa theolojia akileta mambo ya ajabuajabu atakemewa tu bila shida mkuu. Maana wasomi na wasio wasomi wote wanajaribiwa na kupotoka wakati mwingine mkuu.
 
sio huyo tu wako wengi wengi na kila siku wengi wanaongezeka. wengine wanaunga mkono nadharia za Evolution kwa kupitia bibiliq, wengine wanavuruga mfumo wa Mungu wa uimbaji makusudi ili ipatikane nafasi ya kuweka mfereji wa kupitisha mambo ya kijinga na kiovu katika makanisa, jamii na misikiti. Mbeleko inayosaidia ni kiwa jamii imeshakuwa programmed kuwa jambo likisemwa na PHD au PROF ni kweli. Ufafanuzi ukitolewa na PHD wa theology basi huo ji sahihi bila shida.
Unaweza kuwa sahihi ila sio siku zote utakuwa sahihi.
Hata Petro alikuwa sahihi aliposema Yesu ni nani, lkn baadae kidogo akaingiwa na shetani akataka kupingana na mpango wa kifo cha Yesu, Yesu akamkemea rudi Nyuma ewe shetani. Hata PHD au msomi wa theolojia akileta mambo ya ajabuajabu atakemewa tu bila shida mkuu. Maana wasomi na wasio wasomi wote wanajaribiwa na kupotoka wakati mwingine mkuu.
Kumbuka hizi ni zama za mwisho na mpinga Kristo ambaye yuko kazini kwa kasi ya ajabu, halali. 1Yohana 4:1 "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani." na mstari wa tatu umepigilia msumali: "Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja, na sasa imekwisha kuwako duniani."...
 
Alikuwa anazungumzia kwa Bwana " Mbinguni", Ila yeye aliyeiumba dunia, alifafanua wazi kuwa aliiumba siku sita mkuu.

'' Kwa kuwa kwa siku sita, Mungu alizifanya mbingu na dunianna vyote vilivyomo'' Mungu (kutoka 20)
sioni sababu ya kufafanua jambo ambalo muhusika alishalifafanua.
Vinginevyo unataka kumsuta Mungu na kumfanya Muongo kadanganya mara Mbili, kwenye uumbaji na Kwenye mbao za Mawe kitu ambacho sio kweli.
Kalenda tunayotumia ilipangwa na Mungu au na Wa pagan
 
Mkuu mitale na midimu nashukuru kwa maoni yako ila nina swali dogo tu kwako je inapotokea Radiometric dating hiyo hiyo ikipima accurately umri wa layer ya miamba kwa miaka 10 tu iliyopita na ikatambua kwanini basi unapinga credibility yake

Yaani kama unajua kabisa ukipima mfupa wa mtu kuna tissues unaweza tumia kugundua age group yake na wote mtakubali lakini mfupa huo huo ukikaa miaka 100,000 alafu ukipimwa mnasema it's not accurate

Sasa nikuulize swali

1. je kwanini unapinga radiometric dating ilihali it's scientifically proven to be accurate??

2. Je unataka kuniambia miaka ilivyohesabiwa kibiblia ndio sawa na miaka yetu?? Na kama sio... how accurate can Young Earth Creationist be??

3. Pia kama dunia ina miaka 6000 kivipi kuna miamba yenye umri zaidi ya huo??

Ubarikiwe
 
Utafiti wangu (Primary)
Binafsi nilichukua hatua kuonana na wanatheolojia kadhaa kutoka chuo fulani cha Biblia wenye ngazi ya PhD na wamenijuza kwamba Biblia haikuandikwa kwa maneno bali mafumbo hivyo isitafsiriwe kwa maana zetu bali kwa mafunuo na maana zilizo kwa Biblia... Mfano wanadai Dunia haikuumbwa kwa siku 7 kama zetu hizi bali miaka mamilion na wakaenda mbali kusema Biblia haikuanza kuandika matukio yote bali imeandika matukio juu ya watu waliochaguliwa tu hivyo wanakiri kuwa kweli dunia ina miaka mabillion na sio miaka elfu 6 pekee bali wanaotafsiri maandiko kwa akili zao ndio wanapotosha sababu wameitafsiri maneno kama yalivyo badala ya kutafuta maana ya hayo mafum
mkuu pole na majukumu na hongera sana kwa mada

kuna mambo kadhaa nilitaka kuandika lakini niliposoma kwa makin huo utafiti wako ulioufanya nikaona haina haja ya kuandika kwani kifupi nilichotaka kuadika hakina tofauti sana na hayo maelezo machache ulioyaandika juu ya utafiti wako (labda ukipenda ninaweza kuyaongezea nyama zaidi)

2: binafsi sioni haja ya kupinga au kukubaliana na hizo nadharia (hypothesis) mbili za kwanza za miaka 6000 na zingine alizoonesha ndugu mitale na midimu huko juu. kwa sababu bado ni nadharia (hypothesis) tu na sio definitive truth. kwani sayansi inakua inaboreka na kugundua vitu vipya kila kukicha. hivyo naamini sababu ya maendeleo makubwa ya sayansi na techologia hata hiyo njia ya Radiometric dating au C14 dating zinaweza kuja kuboreshwa zaidi hapo baadae na kutoa matokeo yalioaccurate na yenye kuaminika zadi ya hivi sasa.

sio hilo tu la umri wa dunia pia kwa mfano ugunduzi na maboresho makubwa ya kisayansi ya upimaji wa umri wa kitu yaani C14 dating ulipinga na kuharibu kabisa nadharia za muda mrefu za kinawilson zilizodai kitambaa fulani (kilijulikana kama kitambaa cha EDESA) kuwa ni sanda halisi ya Yesu. ugunduzi wa C14 ulikuja kukataa kabisa japo ilikuwa ni kimizengwemizengwe.

mwisho mpendwa kumbuka kuwa biblia haikukusudiwa kuja kuwa kitabu cha kufundisha au kuelezea sayansi ila kweli za kiimani pekee zilizoandikwa na kuelezewa katika mazingira, lugha, tamaduni,maarifa, uelewa na sayansi ya watu wa miaka ya karne na karne tofauti kabisa na mazingira, tamaduni na sayansi yatu sisi watu wa karne ya 21.
 
Habari za mchana wakuu kama kawaida huwa nakuja na mada za kuchokoza fikra zetu hasa kwenye mambo ya kiimani hivyo mada hizi sio za kukosoa dini fulani au vitabu vya imani ila ni kuhoji tu ili tupanue fikra zetu kwenye masuala haya kwa faida yetu sote so sitegemei iibue mijadala ya kidini bali kuelimishana juu ya mambo haya baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye mada husika ya leo.
View attachment 948749
Biblia na umri wa Dunia
Mwaka 1650 professor wa masuala ya theologia na Askofu wa makanisa ya protestant wa Ireland John Ussher aliandaa maandiko yake kupitia mfululizo wa vitabu vyake kuanzia cha Annals of the Old Testament: Origins of the world ambacho ndani yake aliibua mjadala mpana sana wa karne nyingi sana. Ussher alipiga hesabu ya muda ulivyopita kati ya Adam kuumbwa hadi Yesu kuzaliwa na kugundua kwamba ni miaka 4000 imepita tokea Adam aumbwe hadi Yesu kuzaliwa hivyo kufanya dunia yetu ikiwa na wanadamu kuwa na miaka elfu 6 pekee mpaka sasa!!. Ussher alitumia maandiko kama chanzo cha nadharia yake alitumia nyaraka za masoretic zilizotumika kuandaa Biblia za agano la kale ili kuweza hesabu umri wa Adam hadi vizazi vya Abraham hadi kufikia Yesu na baada ya mnyambuliko huo alifanikiwa kugundua kwamba dunia iliumbwa usiku wa October 23 4004 kabla ya kristo.

Young Earth Creationists
Vuguvugu hili la YEC lilianza miaka ya 1960 ambapo iliasisiwa na wasomi 9 chini ya PhD wa theolojia na uhandisi Bwana Henry Morris wakijikita kwenye utafiti wa uhalisia wa umri wa dunia na uumbaji na wakahitimisha rasmi kuwa dunia tunayoishi iliumbwa ndani ya miaka elfu 10 pekee na sio zaidi ya hapo na wao pia walitumia maandiko ya Biblia ya kiebrania ili kufikia hitimisho hilo hivyo na wao wakaunga mkono hoja za hapo nyuma za Professor John Ussher na hata leo hii wameweza shawishi zaidi ya 40% ya wakazi wa marekani kwa takwimu za 2017 wanaamini nadharia hii kwamba uumbaji wa dunia ni kwa mujibu wa Biblia hauzidi miaka 10,000 iliopita.

View attachment 948751
SAYANSI inasemaje??
Baada ya sayansi na teknolojia kukua na kuongezeka vifaa vya kupima umri wa miamba,mazao na mifupa ya wanyama wakaibuka wasomi wa sayansi waliohoji kuhusu uhalali wa nadharia hizi na imeleta utata na mjadala mzito kwa miaka mingi sasa. Mwanasayansi wa karne ya 20 Clair Cameron Patterson baada ya tafiti kadhaa juu ya miamba akagundua ulimwengu toka uanze una miaka billion 4.5 na baadae wanasayansi mbalimbali wakaja na tafiti mbalimbali zikidai kwa usahidi wa kisayansi na kiacholojia kwamba uhai duniani umekuwepo miaka takriban 3.8 Billion iliopita hivyo kukinzana kabisa na nadharia hizo mbili za juu kuwa Biblia

Jinsi ya kupima
Kwa upande wa Young Earth wao wanalalia maandiko kwa kiasi kikubwa na kupiga hesabu miaka ya kibiblia tokea Adam hadi Yesu lakini wanasayansi wamepiga hesabu zao kwa ushahidi wa kushikika wakitumia mfumo unaitwa radiometric dating ambacho kinapima miamba hasa stage tofauti za jinsi miamba inavyooza na ambapo kila stage ina umri wake yake yaani miaka kadhaa ili ifike stage nyingine ya kuoza hivyo wanapiga hesabu kuanzia layer ya mwisho mpaka ya kwanza na kufikia hitimisho la umri wa mwamba huo na wakafanikiwa kugundua mwamba wa kwanza ulitokea miaka 3.8 Billioni iliyopita.
View attachment 948748
Utafiti wangu (Primary)
Binafsi nilichukua hatua kuonana na wanatheolojia kadhaa kutoka chuo fulani cha Biblia wenye ngazi ya PhD na wamenijuza kwamba Biblia haikuandikwa kwa maneno bali mafumbo hivyo isitafsiriwe kwa maana zetu bali kwa mafunuo na maana zilizo kwa Biblia... Mfano wanadai Dunia haikuumbwa kwa siku 7 kama zetu hizi bali miaka mamilion na wakaenda mbali kusema Biblia haikuanza kuandika matukio yote bali imeandika matukio juu ya watu waliochaguliwa tu hivyo wanakiri kuwa kweli dunia ina miaka mabillion na sio miaka elfu 6 pekee bali wanaotafsiri maandiko kwa akili zao ndio wanapotosha sababu wameitafsiri maneno kama yalivyo badala ya kutafuta maana ya hayo mafumbo na wakanipa mistari michache.

Yohana 16:25
25 Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.

Na wakaenda mbali kusema hata hayo mafumbo walioambiwa kuandika Biblia hawakuyaelewa sababu ni siri imewekewa hadi wakati muafaka yaani mwisho wa dunia ufike soma hapa kisa cha Daniel

Daniel 12:4
4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

Hapa tunaona kuna maandiko na nabii zimefichwa kwa uelewa wetu kabisa hata Daniel hakuelewa!!

Daniel 12:8-9
8 Nami nikasikia, lakini sikuelewa; ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, mwisho wa mambo haya utakuwaje?
9 Akasema, Enenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa
mwisho.

Hivyo kama hata Daniel kuna baadhi ya vitu alifichwa na mpaka anaandika hakuvijua basi hata sisi hatuwezi vijua mpaka siku ya mwisho hivyo wakahitimisha mjadala kwa kusema huenda ni kweli dunia ina 4.5 Billion years ila sio 6000 kama YEC inavyosema maana Biblia haielezi hicho kuwa ni miaka 6000 bali watu wanatafsiri maandiko kwa akili zao ilihali YAMEFICHWA!!
View attachment 948750
Hitimisho
Ukinzano huu kati ya maandiko na sayansi juu ya asili ya umri wa ulimwengu umezua mjadala mpana sana huku kila upande ukivutia kwake nikaona kwa kuwa JF ni kisima cha maarifa nilete hii mada ili tuweze kufikiria pamoja je umri wa dunia upi ni halisi

4.5 Billion ama 6000?

Naomba kuwasilisha

Nakuja ......!
 
Mkuu hiyo ya Adam kuwa wa kwanza au lah ni mada pana sana inayostahili uzi wake na ntakuja kuielezea siku nyingine ila kwa sasa tunajikita umri wa Dunia iwe na wanadamu ama lah kupitia hoja za hao YEC/Ussher Vs wanasayansi je nani mkweli juu ya umri wa dunia??

kwa kifupi Biblia hipo kwenye code au tuseme fumbo/mafumbo sana, unapoisoma unatakiwa uwe na uelewa mpana sana wa vitu vingi na uwe na busara ya kutafakari kwa kina, mfano operation ya kutoa kiungo (mfano figo) kwa mtu mmoja na kupandikiza kwa mtu mwingine ni ugunduzi wa miaka ya 1900, lakini ukisoma Biblia tunaona uwezekano huo ulikuwepo tangu MWANZO, kwani hata Adam alipigwa nusu kaputi na kiungo kikatolewa kwenye mwili wake na kupandikizwa mtu mwingine (Hawa), kwa mtu anayesoma Biblia kwa tafakari hawezi kushangaa mtu kupandikizwa Figo. Mfano mwingine ni jinsi Galileo alipokuwa akipingwa na Makasisi wa pale Vatican aliposema Dunia ni duara, alipingwa sana na wanasayansi wa Kikakotliki lakini ukisoma kitabu cha isaya 40:22 kinasema "Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya Dunia" sasa Biblia inasema Dunia ni Duara mbona wao walikuwa wanAmpimga mtu aliyekuja kuthibitisha maneno ya Biblia?

tukirudi kwenye maada, mimi naamini siku zote sayansi inayozungumwa ukiitafuta utaipata kwenye Biblia kwa uwiano wenye kuingiliana/Kufanana, kwa hoja iliyotolewa na hao makasisi kuwa Dunia ina miaka 6,000 tu sio sahihi nakubaliana na wana sayansi kuwa dunia ni nzee kufikia umri huo wa miaka 4.5bil.

zitto junior umeelezea njia moja ya kisayansi ya kuweza kutambua umri wa Dunia kwa kutumia Radiometric, lakini pia kuna njia ya pili ya kuweza kutambua umri wa Dunia kwa njia ya kulinganisha matukio (Correlations) hapa kuna kanuni moja inasema 'vitu vinvyofanyika leo na kuviona basi ni somo la kutuelezea vitu vilivyofanyika kipindi cha nyuma' (The Present is the key to the Past),

Tunafahamu mwamba wa asili kabisa ni mwamba moto (igneous rock), huu mwamba ukimegekamegeka vipande vyake vinaweza kujiunga tena kwa uwezo wa kukusanywa aidha na maji, upepo au barafu na kutengeneza mwamba mwingine wa kitabaka (Sedimentary Rock) hili tukio la kutengenezwa kwa mwamba wa kitabaka bado linaendelea lakini ni zoezi la taratibu mno (miaka mingi), so wataalamu wa miamba wanachunguza na kuona kwa hali ya kikawaida kabisa tabaka dogo tu la mwamba huo say mita 10 x10 na kina cha mita 1(100 Cibic Mita) linaweza kutengenezwa kwa miaka zaidi ya 100, swali wanalojiuliza je tabaka la 1kmx1kmx1km (1km Cubic mita) litatengenezwa kwa muda gani? obvious ni muda mrefu sana.

Mfano wa pili tunaona Bonde la ufa la Africa Mashariki (East Africa lift Valley) linapanuka, na miaka ya mbele kuna kipande kitatenganishwa na maji, utafiti uliofanywa maeneo ya Arusha unaonyesha kuwa bonde hilo linapanuka kwa 10-14cm kwa mwaka, Bahari Nyekundu (Red Sea) ni sehemu ya ufa huo na ilitokea kwa utaratibu unaofanyika huku East Africa, na sehemu pana kabisa ya bahari hiyo ina upana wa 355Km, sasa tukirudi kwenye ile kanuni yetu kuwa The Present is the key to the past, yaani tunachokiona sasa Arusha ndicho kilichotokea Red sea basi hiyo Red sea ilipanuka mpaka kufikia ilipo sasa kwa muda gani?
1Km =100,000cm
355Km=35,500,000cm
Bonde la ufa linapanuka kwa rate ya 10cm kwa mwaka kwa hiyo 35,500,000cm zitapanuka kwa muda wa miaka 3,550,000, so kama Bahari Nyekundu imepanuka na kufikia ilipofika sasa kwa muda wa miaka 3.5mil iweje dunia iwe na miaka 6000 tu?

kifupi, Dunia ni nzee sana na ukifumbua code za Biblia utaona uzee wa Dunia
 
Ni kweli Adam ndiye mwenye umri wa miaka 6,000, na tukumbuke kuwa aliumbwa baada ya viumbe wote wengine kuwa wameumbwa baada ya miaka mingi...

Kaka Bishop Hiluka , mitale na midimu , mshana jr naona mnaitendea haki sana Maada iliyopo Mezani,
Mimi naamini kuwa Sayansi inaconfirm kilichopo kwenye Bible, Fungu la kwanza la kitabu cha Mwanzo kinasema,
Mwanzi 1:1-2 Hapo Mwanzo Mungu aliziumba mbingu na Nchi, 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; roho ya mungu ikatua juu ya uso wa Maji. UKIANGALIA NA KUTAFAKARI HAYO MANENO YA MWANZO 1:1-2 UTAONA KUWA MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI NA MAJI SIKU NYINGI KABLA YA ZILE SIKU SABA, HATUNA UHAKIKA NI SIKU AU MIAKA MINGAPI, LAKINI MUNGU ALIUMBA MBINGU NA NCHI NA MAJI KWANZA

ukija kwenye Mwanzo 1:3 ndio zile siku saba zinapoanza, je kabla ya siku saba kuanza Dunia ilikuwa na miaka mingapi?, kwa uwezo tuliopewa na Mungu kwa kutumia sayansi ndio tunaweza kung'amua hiyo code kuwa Dunia ni nzee sana Probably 4.5 bil yrs, miaka 6000 wanayoizungumza hao makasisi ni kuanzia zile siku saba, je kabla ya hapo?

CC: zitto junior
 
Mfano mwingine ni jinsi Galileo alipokuwa akipingwa na Makasisi wa pale Vatican aliposema Dunia ni duara, alipingwa sana na wanasayansi wa Kikakotliki lakini ukisoma kitabu cha isaya 40:22 kinasema "Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya Dunia" sasa Biblia inasema Dunia ni Duara mbona wao walikuwa wanAmpimga mtu aliyekuja kuthibitisha maneno ya Biblia?
pia kabla ya 1586 dunia nzima iliamini katika geocentricism/geo-system. soma yoshua 10:13 "Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao."

lakini leo iko kabisa proved kisayansi (definitive truth) kwamba ni dunia na sayari zingine ndizo zinazozunguka jua. heliocentricism/solar-system na inapingana kabisa na yoshua 10:13.

biblia haikukusudiwa kuja kufundisha sayansi au kuwa kitabu cha sayansi au kufafanua masuala ya sayansi.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya ulimwengu (universe) na dunia (world), ukiyaelewa haya maneno mawili huwezi kupata shida kujiuliza maswali kama haya...
Ila dunia siipo kwenye ulimwengu. May be tu judge umri Wa ulimwengu. But dunia ni ya mda sana.
 
Mwanateolojia SANCTUS ANACLETUS unahitajika huku.

Asante Makosa kwa kuniita! Mjadala huu ni mzuri sana. Na ningependa niutendee haki. Kwa harakaharaka tu ni kwamba Wanasayansi wameshathibitisha kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa kwamba dunia na ulimwengu vimekuwepo kwa zaidi ya miaka 4.5 bilioni iliyopita. Na mimi nasema,matokeo ya utafiti ya hawa jamaa yanatupatia ile picha kwamba Uumbaji Ulimwengu ulitokea muda mrefu sana uliopita.

Ukokotoaji uliofanywa na Mprotestanti Ussher una mapungufu kwa sababu yeye amekaba kanuni yake kwa kuangalia miaka wanayotajwa watu muhimu katika historia ya Wayahudi kuishi. Sasa kanuni hiyo ina makengeza kwa sababu dunia hii haikuwa na watu wanaotokana na Lineage ya Kiyahudi tu. Dunia imekuwa na watu wengi tu waliokuwa wakihama kutoka sehemu moja hadi nyingine ambako walianzisha Jumuia zingine au Mataifa mbalimbali. Kwa hiyo ukitumia Umri Wa watu wanaotokana na Taifa moja tu unakuwa umeingia katika upotoshaji.

Sababu ya pili ya upungufu katika kanuni hiyo ni kwamba namba zinazotajwa katika Biblia hazina maana ya moja kwa moja katika uhesabuji namba(Literal meaning). Kwa mfano,Yesu alipofunga kwa siku 40 Arobaini haina maana ya siku 40 kweli Bali kwamba mfungo wake ulikuwa Wa muda mrefu na ulikamilika kama alivyokuwa amepanga. Yaani, Ratiba ya mfungo ilifika mwisho kabisa na haikukatishwa licha ya changamoto ya njaa iliyojitokeza.

Kwa hiyo, tutumie Sayansi katika kufahamu Umri Wa Ulimwengu na Dunia.
 
Rudia kusoma maandiko (Biblia) pengine utaelewa. 2 Petro 3:8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu...
Je, unadhani siku saba zinazotajwa zilikuwa na saa 24 kama siku tuzijuazo leo?...
Sahihi.


( يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ )

السجدة (5) As-Sajda

Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi.

Kwa hiyo muda wa kuumbwa mbingu na Ardhi na vilivyomo umechukua miaka elfu sita kwa hesabu zetu sisi.
 
Mkuu mitale na midimu nashukuru kwa maoni yako ila nina swali dogo tu kwako je inapotokea Radiometric dating hiyo hiyo ikipima accurately umri wa layer ya miamba kwa miaka 10 tu iliyopita na ikatambua kwanini basi unapinga credibility yake

Yaani kama unajua kabisa ukipima mfupa wa mtu kuna tissues unaweza tumia kugundua age group yake na wote mtakubali lakini mfupa huo huo ukikaa miaka 100,000 alafu ukipimwa mnasema it's not accurate

Sasa nikuulize swali

1. je kwanini unapinga radiometric dating ilihali it's scientifically proven to be accurate??

2. Je unataka kuniambia miaka ilivyohesabiwa kibiblia ndio sawa na miaka yetu?? Na kama sio... how accurate can Young Earth Creationist be??

3. Pia kama dunia ina miaka 6000 kivipi kuna miamba yenye umri zaidi ya huo??

Ubarikiwe
Radiometric sioni kama ni scientific accurate, hasa inapotakiwa kipima umri wa kitu huku haijui birthday yake. mfano tukipima umri wako kwa kutumia radiometric tutagundua unamiaka zaidi ya milioni nne.

Kwa kuangalia genealogy ya watu watu wa bibilia au huyo mdau aliyegundua miaka 4000+ tunapata angalau approximation ambazo zitaifanya dunia kuwa na umri ambao ni around 6000 Years na sio laki wala mamilioni. Kama ujatumia bibilia lakni.

Suala la miamba linaturudisha kulekule. Huwezi kujua umri wa miamba kwa kitegemea isotropic au radiometric dating huku hujui birdhday ya miamba. Mfano wanasema inakuhitajia miaka malaki kutengeneza almasi, lkn leo unaweza kutengeneza almasi kwa lab kwa siku tatu au moja. Kuna vitu vingi vya kisasa ambavyo baada kukutwa katika miamba ambayo inasadikiwa kuwa na mamilioni ya miaka, swali likarudi kwa nini mwamba au jiwe uwe na miaka mamilioni wqkati sindano mfano uliomo umegunduliwa miaka ya juzijuzi. watasingizia ni matokeo ya contamination ila kwa kujifunzia radiometric sawa ila accuracy sioni kama ni reliable.
 
Alikuwa anazungumzia kwa Bwana " Mbinguni", Ila yeye aliyeiumba dunia, alifafanua wazi kuwa aliiumba siku sita mkuu.

'' Kwa kuwa kwa siku sita, Mungu alizifanya mbingu na dunianna vyote vilivyomo'' Mungu (kutoka 20)
sioni sababu ya kufafanua jambo ambalo muhusika alishalifafanua.
Vinginevyo unataka kumsuta Mungu na kumfanya Muongo kadanganya mara Mbili, kwenye uumbaji na Kwenye mbao za Mawe kitu ambacho sio kweli.
Ni sahihi mbingu,duniabna vilivyomo kuumbwa katika siku sita,. Ilaa hesabu hasa ya siku kwa mujibu Wa muumba ni miaka elfu kwaa masaa haya 24

Ata kwenye kitabu hichi kitukufu kimeeleza hivyo,



( الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا )

الفرقان (59) Al-Furqaan

Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye.
 
Mkuu,kasome upya maana ya kila namba katika Kiebrania. Namba sita au saba na nyinginezo hazikupewa literal meaning kama tunavyoelewa sisi Leo.
kuhusu Hilo Mungu amelifafanua kwenye bibilia humohumo literally akifafanua alichokifanya kuwa ni siku sita kamili haihitaji kigiriki wala kiebrania.

Ushahidi.
'' Kwa siku sita (sio mamilioninya miaka) mimi mwenyezi Mungu niliziumba Mbingu na Dunia Bahari na Vyote vilivyomo...'' Kutoka 20:11

akawapa maelekezo hao watu wake wa enzi hizo akisisitiza ni siku sita lateral 24Hrs, mavumbuzi ya tafsiri za mamilioni yamekuja hapo katikati ya safari
 
Back
Top Bottom