Sijajua kama wengine wameuliza,ila mtumishi kama nitapata kibari rohoni mwako,nielezee Nini maana ya nafsi na roho,vinanipa shida kuelewa ,naona ni kama ni kitu kilekile
Mi naomba nikueleweshe kwa urahisi.
Mwamba amesema kuna mwili, nafsi na roho.
Mwili ni jumba (body) ambalo linaishi katika dunia hii, Biblia inasema neno Vazi.
Hii kwanza ili uelewe, ni kuwa kwenye kila ulimwengu kuna vazi lake.
Ukiwa unaishi duniani, au kwenye ulimwengu huu tunaoishi ni lazima utatumia vazi la mwili.
Hapa kwanza tupo pamoja. Si ndio?
Haya twende sasa...
Kuna nafsi,
Hii ndio identity yako wewe, yaani hii ndio wewe. Nafsi ndipo inakaa id yako kuwa wewe ni nani.
Kwenye mwili huu wa ulimwengu wetu nafsi hatuioni, ila inajificha ndani yetu inabeba vitu vyake kadhaa, mf. Self (inner conscience); hii ni ile hali yako ya kutambua mema na mabaya, kufanya maamuzi binafsi, ni ile sauti flani unaisikiaga au inakuambiaga wakati mwingine unapotaka kufanya maamuzi ya hiari au ya lazima (hatari), na kadhalika.
Nikiielezea hizo sauti za ndani zinaweza kukuchanganya ukaamini ubonho ndio unafanya kazi zote, ila ni hapana, ubongo ni kama computer system tuu ya body zima la mwili, au kama unajua computer, brain ni kama CPU au processor kwenye computer.
Lakini kwenye nafsi hakuna kitu kimoja tuu, kuna vingine ambavyo kuvifahamu ni mpaka uwe na full access ya ulimwengu wa roho, namaanisha, uweze kuwa umefunguka zile SENSES zako zilizofungwa, zikiwemo THIRD EYE na zinginezo. Zinafika hata saba au zaidi, ndio Zile Higher dimensions. Usijali sana kama huzijui maana bado hazijagundulika vizuri kwenye ulimwengu wa mwili, so..yah.
Ila kwa ufupi, nafsi ni identity yako wewe.
Sawa. Mpaka hapo nadhani tupo pamoja.
roho sasa....
Roho ni power grid, light au energy source ya kila kitu chako. Maana rahisi ni chanzo cha nishati ambacho Mungu kakupa. Na hiki anakiona yeye mwenyewe. Na kikizima hiki, anajua, kikiendelea kuwaka anajua.
Kumbuka kuwa wewe ni system, so kila system ni lazima iwe na power source/ chanzo cha nishati, ndio roho sasa.
Watu wa dini na imani wanasemaga roho imetoka kwa baba, maana yake ni roho ni ya Mungu mwenyewe, ndio maana ukisali au usiposali, Mungu anakusikia, anakuona, na anakujua popote pale ulipo.
Wengine hufika mbali zaidi kuwa hii ndio inayompelekea taarifa Mungu kuwa unafanya mema au mabaya, well, kwa hilo sina uhakika...ila najua tuu NAFSI ndio itakayohukumiwa siku ya mwisho coz ina matendo yako yote, tangu kuzaliwa mpaka kuda kwako duniani, na itaendelea kurekodi maisha yako yote ya milele.
Anyway, tusipotelee huko, turudi kwenye reli.
So, Hauwezi kutengeneza roho, wala kuiona, wala kujua inavyofanya kazi...sanasana utasoma na kuelewa, lakini ni tech ya Mungu mwenyewe, hauwezi uifanyia manouver, kwa sababu roho ni ya milele.
Mnaosoma biblia mlionaga lines zinasema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, maana yake mtu amepewa roho. Ndicho pekee kinachokufananisha na Mungu, na si kingine. So hapa kwa wengine majibu wamepata, kuwa mwanadamu amefananaje na Mungu.
Mpaka hapo sasa umeelewa?
SASA INAKUWAJE MTU ANA VYOTE HIVI KWA PAMOJA???
Nafsi na roho zinaweza kushikamana na kukaa pamoja, lakini mwili hauwezi kushikamana na vyote hivi kwa muda mrefu, kwa sababu mwili ni wa muda, mpito, unaishia kwenye ulimwengu huu pale unapokufa (iwe duniani au mars au hata sayari yoyote ile, au galaxy gani sijui ukiweza kuishi huko)
Lakini Nafsi ni ya milele, na roho ni ya milele. Havifi, havipotei na wala havichakai.
NINI KUHUSU STORI ZA KWENDA MBINGUNI?
Kwa watu wa dini na imani mbalimbali wanaamini kuhusu kwenda mbinguni, ila endapo wakibahatika kwenda huko ni kuwa wataenda na NAFSI (mwili utauacha) na wakifika kwenye ulimwengu husika, watakuta au kupewa vazi jipya la ulimwengu huo, ili waishi maisha ya huko.
Sasa kama umeenda Mbinguni utapewa vazi la huko ambalo naskia ni zuri ajabu, lipo so pure, so real, na soo perfect, (kama ambavyo Zumaridi amejaribu kuelezea kwenye interview yake na MillardAYO na akashindwa[emoji23][emoji23])
Na kama ukibahatika kwenda motoni, basi utapewa vazi la huko ambalo limejaa mateso, taabu, funza, wadudu, moto na maumivu ya milele.
Mpaka hapo sijui kama umenielewa??
Na haya hadi zumaridi amejaribu kuelezea pia, ila inabidi umsikilize kwa makini sana ili upatepate idea.