Kujibu kile kinachojulikana kama "uzalishaji kupita kiasi wa China" ambacho kimechochewa hivi karibuni na baadhi ya nchi za Magharibi, Bw. Ayodeji Dawodu, ambaye anafanya kazi na kushughulikia mambo ya Afrika katika benki ya uwekezaji ya BancTrust yenye makao yake makuu mjini London alisema, hakuna “uzalishaji kupita kiasi wa China”, na kinyume chake, Afrika inahitaji China yenye maendeleo yenye nguvu.
Alielezea kuwa nchi za Afrika zinaagiza bidhaa nyingi kutoka China, zikiwemo mashine, nguo na vitu vya mahitaji mengine, na kudumisha uhusiano wa kunufaishana kiuchumi na kibiashara na China.
Kama Dawodu, kuna wanauchumi na wataalamu wengi ambao ni vigumu kwao kuelewa huo "uzalishaji kupita kiasi wa China ", na wengi wao wanatoka nchi za Magharibi ikiwemo Marekani. Hata hivyo, katika macho ya serikali za nchi hizi, kile kinachoitwa "uzalishaji kupita kiasi wa China" kinamaanisha kwamba China haipaswi kuzalisha bidhaa zaidi ya uwezo wa mauzo yake ya ndani.
Kwa mfano, kampuni ya magari ya umeme ya China inaweza kutengeneza magari kwa ajili ya soko la ndani tu, na haitakiwi kuuza magari katika nchi za nje. Lakini kulingana na mantiki hii, Kampuni ya Boeing ya Marekani inauza ndege duniani kote, je, inapaswa kupunguza uzalishaji?
Maharage ya soya yanayolimwa Marekani yanauzwa kote duniani, Je, mashamba nchini humo yanapaswa kupunguza uzalishaji? Ni wazi kuwa, nchi hizo za Magharibi zinatumia kisingizio hicho kupinga utandawazi na kujilinda kibiashara.
Tofauti na nchi hizo za Magharibi, China na Afrika ni waungaji mkono na wanufaika muhimu wa utandawazi, na katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano wa kibiashara wa pande mbili umekuwa karibu zaidi. Bidhaa za China zinazidi kuwa maarufu katika soko la Afrika.
Kama tunavyojua sote, vifaa vya umeme vyenye ubora wa juu na vya bei ya chini, simu, nguo na viatu vilivyovyotengenezwa nchini China vinapendwa sana na watu wa Afrika. Mfano mwingine, ni miradi ya miundombinu iliyotengenezwa na China, kama vile Reli ya SGR Kenya na Kituo cha Umeme wa Maji cha Kafue Gorge Lower Zambia pia imekuwa chachu katika kuboresha miundombinu barani Afrika, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watu.
Kama muungaji mkono mkubwa wa maendeleo endelevu ya Afrika, "Made in China" pia inasaidia mabadiliko ya nishati ya kijani barani Afrika. Afrika ina 60% ya rasilimali za jua duniani, lakini ina 1% tu ya vifaa vya kuzalisha umeme wa jua duniani, na kusaidia nchi za Afrika kutumia nishati hizo safi ni jukumu kwa bidhaa zinazozalishwa China.
Wakati huo huo, magari ya umeme ya China pia yanazidi kuwa maarufu katika nchi za Afrika, kubadilisha hali ya muda mrefu ya soko la magari la Afrika kudhibitiwa na magari ya Ulaya, Marekani na Japan.
Aidha, mashine za ujenzi za China na mashine za kilimo pia zimeshinda soko la Afrika kutokana na ubora mkubwa na bei nafuu... Kama jarida la "African Leadership" la Uingereza lilivyoeleza kuwa katika dunia ya sasa, uhusiano wa karibu wa kibiashara kati ya China na Afrika unaleta fursa mpya kwa pande zote mbili na kusaidia kujenga dunia kuwa na ustawi na maingiliano.
Ni wazi kwamba, kitu kinachoitwa "uzalishaji kupita kiasi wa China" ni njia ya kisiasa inayotumiwa na Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi kudhalilisha na kukandamiza uchumi wa China, na lengo halisi ni kutafuta ushindani kwa nchi hizo zenyewe, lakini kufanya hivyo ni hatari kwa uhusiano wa kawaida wa kibiashara wa kimataifa na kuharibu maslahi ya pamoja ya nchi zote duniani, hasa nchi za Afrika.