Bifu linaendelea, Mume wa Waziri Gwajima akana kumtambua Mathias Gwajima kama Baba yake

Bifu linaendelea, Mume wa Waziri Gwajima akana kumtambua Mathias Gwajima kama Baba yake

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Picha ya Marehemu Mzee Stiven Gwajima. Huyu ndiye alikuwa Mkwe wa Waziri wa Afya Dorothy Gwajima.

Mzee Stiven Gwajima alifariki dunia tarehe 30/9/2019 jijini Dar es Salaam. Mtoto wake Mwanasheria Msomi Methusela Gwajima amezungumza na #KitengeTV na kusema huyo ndio alikuwa Baba yake na Mkwe wa Waziri wa Afya na sio mwingine yeyote "Amesema jioni hii"

Hatua ya Mwanasheria huyo kuweka wazi hivyo imekuja baada ya leo Gwajima mwingine kuibuka na kusema yeye ndio mkwe wa Waziri huyo wa Afya.

#KitengeUpdates

FB_IMG_16296499607207149.jpg

Je, yule mzee Mathias Gwajima aliekuwa kanisa la ufufuo na uzima leo na akamtaka waziri aache kutumia jina la Gwajima alikuwa amesahau au alipangwa?

Mtazame mzee mathias Gwajima hapo chini👇👇
 
Gwajima askofu kwa tabia zake za uongo sitashangaa akifanya huo mchezo, yule ni msanii tu anaecheza na upepo kuwakamata wasiojua kufikiria vizuri, akiwaambia Corona haiji wanamshangilia, ikija anawadanganya na kingine sichanjwi wanamshangilia tena.
 
Askofu Hana Injili, Zaburi, Mithali,Agano la Kale,la kufundisha Waumini wake. Una Nguvu ya Mungu Ndani unapataje Ujasiri wa kumuabisha Mke wa Nduguyo? Huyu Askofu Hekima Hana. Endelea Tu kuwaongoza Vipofu Mwisho wake atauona.
 
Waziri Gwajima amesikika Mara kadhaa akisema mchungaji Gwajima Ni shemeji yake ..inaonekana baba yake mchungaji Gwajima na baba wa mume wa waziri wanaweza wakawa mtu na Kaka yake

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
gwajima askofu na gwajima mume wa waziri ni mtu na kaka yake kwa upande wa mama
 
Back
Top Bottom