Bifu ya hawa wawili Arusha bado mbichi

Bifu ya hawa wawili Arusha bado mbichi

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Katika siku za hiv karibuni jijini Arusha kumeibuka bifu Baina ya wafanyabiashara wawili ambao inaelezwa hapo awali walikuwa marafiki wa kufa na kupikana.

Wafanyabiashara hawa Elizabeth Mayani maarufu kama “Mama Shombee “ anayemiliki kampuni ya Newlook Bridal na Lilian Mosha mmiliki wa duka la Liliy Love Bridal.

Taarifa zinaeleza kuwa Wafanyabiashara hawa kabla ya kufarakana walikuwa wakifanya biashara kwa pamoja lakini inaelezwa mmoja (Lilian)alimzidi kete mwenzake na kuvuta mpunga na kisha kwenda kufungua biashara zake.

Taarifa hizo za ndani zinaeleza kuwa Mama Shombee ndiye aliyemkaribisha Lilian kwenye biashara lakini baada ya kujanjaruka na kuvuta pesa dukani kwake alitemana nae na kisha kwenda kufungua duka lake kitendo ambacho kilimkasirisha mwenzake na kujenga chuki baina yao.

Itakumbukwa ya kwamba mwanzoni mwa mwaka huu kwenye tuzo za wanawake Arusha zilizoandaliwa na mwanama Fide Mwakitelema Wafanyabiashara hawa wote walijinyakulia tuzo lakini yaliibuka maneno kwamba Mama Shombee alimwaga rushwa kwa waandaaji ili aonekane kinara kuliko wenzake kitendo kilichomuudhi Lilian Mosha.

Inaelezwa katika tuzo hizo Mama Shombee alimwaga fedha kwa MC Dk Kumbuka ili amfagilie katika tuzo hizo kitendo kilichomuudhi Lilian na kundi lake.

Kumekuwa na maneno ya kurushiana mitandaoni baina ya Wafanyabiashara hawa ambao wana ukwasi hali ambayo imepelekea kila mmoja kutengeneza kambi ya kushambulia mwenzake.

Tunaomba watu walio karibu na hawa Wafanyabiashara wawashauri kwamba bifu hazina maana walio karibu wawaweke kitako na wawashauri kwamba maisha sio kugombana wafanye kazi waingize vipato.

Kazi iendeleeee

EEDA769E-FD96-4DB2-8BD7-93AFACE71E26.jpeg
35DD5DAB-F224-4E28-8FD0-C3A627898FD0.jpeg
 
Back
Top Bottom