zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,661
- 40,890
Mkuu jibu swali mbona ni rahisi tu, wapi sabato ni jumamosi au mlijitungia wenyewe tu??unasema “Wapi wamesema ni Jumamosi?” Haya angalia Biblia yenyewe inavyosema:
📖 Luka 23:54–56:
“Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na Sabato ikaanza kuangaza. Wakamrudishia mwili wa Yesu, wakarudi, wakatengeneza manukato na marhamu; na siku ya Sabato walistarehe sawasawa na ile amri.”
📖 Luka 24:1:
“Hata siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, walikwenda kaburini…”
Na sisi wote tunajua siku ya kwanza ya juma ni Jumapili (ninyi wenyewe FPTC mnasheherekea Easter Jumapili kwa sababu ya ufufuo,sijui Nan kawaambia hili😂😂😂)
Kwa hiyo Sabato ipo wazi = siku ya saba = Jumamosi.
Kama Biblia inasema Siku ya kwanza ya juma = Nyie FPTC mnasherekea Easter kila jumapili eti ufufuko wa Yesu ,, basi siku ya saba ni lini? 😂ukijibu nakupa Laki 3
FPTC mnasheherekea Jumapili kama siku ya ufufuo hiyo ni kweli??bisaha kama kweli unajiweza, lakini Biblia haijasema badilisheni Sabato muifanye Jumapili. Hii ni mapokeo ya wanadamu.
Hata Yesu mwenyewe alikufa Ijumaa (siku ya maandalio), akalala kaburini Jumamosi (Sabato), na akafufuka Jumapili (siku ya kwanza ya juma). Sasa kama hiyo si ushahidi wa moja kwa moja, unataka andiko gani tena?
Punguza maelezo marefu na toa tu specific answer kuwa ni biblia au ni nyie wafuasi wa Hellen ndio mlichagua.