Biharamulo, Kagera: Ajali ya basi la KABCO yaua watu 11 eneo la mlima Simba

Biharamulo, Kagera: Ajali ya basi la KABCO yaua watu 11 eneo la mlima Simba

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Ni ajali kubwa sana kwa takribani miaka 10 haijawahi kutokea ajali kama hii ambapo watu kadhaa wanadiwa kufa nita update taarifa, baada ya kufika hospitalini

FB_IMG_1734804796052.jpg

Ni basi la kampuni Kabco ambayo hufanya safari zake kati ya kigoma na bukoba

Inadaiwa sababu mwendo kasi na dereva kushindwa kulimudu kwenye kona yenye mteremko mkali liliacha njia na kupinduka mara kadhaa hadi kipande cha juu cha bus kuondoka

FB_IMG_1734804791766.jpg

Updates

Watu kumi na moja wamefariki na zaidi ya 20 ni majeruhi taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Biharamulo

USSR

======

UPDATES

=====

Watu 11 wamefariki dunia huku 16 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea katika Kijiji cha Kabukome Kata ya Nyarubungo kwenye mlima wa kuanzia pori la Kasindaga lililopo Wilaya ya Biharamulo na Muleba Mkoani Kagera

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amelitaja gari hilo kuwa lina namba za usajili T 857 DHW linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Bukoba ambapo liliacha njia na kupinduka na hatimaye kusababisha vifo vya Watu 11 kati ya hao Wanaume ni wanne Watu wazima na Wanawake watano, Mtoto wa kiume mmoja na Mtoto wa kike mmoja na miili yote ipo Hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo huku kati ya 16 waliojeruhiwa baadhi yao wanaendelea vizuri na muda wowote wataruhusiwa.

IMG_20241222_090053_856.jpg

IMG_20241222_090537_874.jpg

IMG_20241222_090524_982.jpg
 
Ni ajali kubwa sana kwa takribani miaka 10 ambapo wait kadhaa wanadiwa kufa mita update taarifa.

K
Gari la Kabco hufanya safari zake kati ya kigoma na bukoba

Inadaiwa ni mwendo mkali na dereva kushindwa kulimudu kwenye kona yenye mteremko mkali

USSR
View attachment 3181876View attachment 3181877
Oooh my God ooh my God. This is so sad.
 
Back
Top Bottom