The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,006
- 3,275
Ndio kawaida yao hao washari sana. Muda umeisha lakini wana lazimisha kuendelea na kampeni ili sheria ichukue mkondo wake halafu waanze kulalama.
Wamebanwa mbavu na wataangukia pua kesho wanacho tafuta sasa ni kuanzisha fuso na kuharibu uchaguzi.
Hivi hawawezi kujifunza japo kidogo kutoka kwa CCM? wao wamemaliza kampeni zao ndani muda na kutawanyika
CCM si wana uwanja wao kule juu karibia na shule ya msingi Umoja? hako kastendi kanabana sana au walijua hawataujaza ule uwanja?Kampeni za mwisho za CCM zinafanyikia uwanja wa Stendi Kuu ulipofanyikia mkutano wa TLP jana.
Hapa umechonganisha lolote baya tutakulaumu wewe. Ulikuwa na maana gani kumkumbusha RPC kazi yake?Nimerejea mkutano wa CCM, saa 12 imepita, Makamba ndie anazungumza. Mgombea wao ameshazungumza.
Wakati naondoka mkutano wa Chadema, nimemuona RPC wa Kagera, Afande Salema akiwa na CO, FFU, afande Aneclet, nikasimamisha gari, na kushuka kuwasalimia, nikalipongeza jeshi la polisi kwa uvumilivu wa uvunjifu wa sheria ya uchaguzi kwa kuwastahimilia Chadema wakiendelea na kampeni huku saa kumi na mbili imepita.
RPC akasema ni kweli wameivumilia sana Chadema, ili ifikapo 12 na Nusu, uvumilivu, utawashinda.
CCM WAMEMALIZA KAMPENI 12:30 JUU YA ALAMA. Narejea Chadema kushuhudia Tifu!.
wNdio kawaida yao hao washari sana. Muda umeisha lakini wana lazimisha kuendelea na kampeni ili sheria ichukue mkondo wake halafu waanze kulalama.
Wamebanwa mbavu na wataangukia pua kesho wanacho tafuta sasa ni kuanzisha fuso na kuharibu uchaguzi.
Hivi hawawezi kujifunza japo kidogo kutoka kwa CCM? wao wamemaliza kampeni zao ndani muda na kutawanyika
CCM ni wazuri kwenye mass mobilization, wangeweza kuujaza uwanja wao, tatizo wana B'iMulo, hawatabiriki.CCM si wana uwanja wao kule juu karibia na shule ya msingi Umoja? hako kastendi kanabana sana au walijua hawataujaza ule uwanja?
Hao polisi waangalie huo ustahimilivu wao usije ukawa ndio chanzo cha machafuko maana wanawalemaza watu. Kwa kuwaachia wavunje sheria wanaweza kudhani kuwa ni haki yao kuvunja sheriaNimerudi Chadema, mkutano ndio unaisha 12:45 bila polisi kuingilia kati. Kama kawaida yao wanaondoka kwa maandamano yasiyo yakiongozwa na Mbowe, Polisi wanaendeleza ustahimilivu wao kwa kutoyatawanya maandamano.
Hata wana CCM wanazunguka mitaani wakiongozwa na gari zao za PA. Nawashuhudia makamanda wale wawili wamesimama njia panda kushuhudia maandamano yasiyo rasmi bila kuamrisha visago.
Tunataka kujua kuwa nani atakuwa mshinda kutokana na kura za maoni za CCM au vipi??
Sasa Nani Atashinda uchaguzi wa Kesho??
Inawezekana kabisa kuwa CCM wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi wanakuwa wanabaka Demokrasia na hivyo kuna uwezekano yale ya busanda kujirudia tena Biharamulo
WanaBimulo wengi ni kabila la Wasubi, hawa ni jamii ya Wahaya wenye sura za majonzi, miili ya shidashida na mtazamo wa humble na down to earth, Wahaya wakawaida walio wengi, wana sura laini laini na miili ya neema inayoashiria wanakula vizuri, ila pia kwenye mazungumzo yao, kuna elements za kujisikia, nshomile mentality na majigambo mengi.
WanaBimulo ni wakimya sio kwa sababu hawa la kusema, bali ni wakya waliomua kukaa kimya lakini wanaonekana kujua vizuri kila kinachoendelea, yaani wakmya huku wanafikiri na kutafakari, Wahaya wa kawaida waliowengi ni boastiful na very vocal.
Hii maana yake, kama Wasubi, wanaukabila wa ndani ya damu, watanchagua mgombea wa Chadema ambaye ni Msubi mwenzao. CCM imemsimamisha Mhaya, kama Wasubi, wanawazimia Wahaya, basi watamtosa Msubi mwenzao wa Chadema na kumchagua Mhaya wa CCM.
Kutokana na tabia ya ukimya wa Wasubi, ni wagumu kutabirika, hata huyo Msubi mwenzao hawajamuonyesha matumaini ya kumpatia upendeleo wa ukabila. Hivyo kwa ukimya huo, kama wanaukabila mioyoni mwao, mgombea wa CCM hawezi kupita hata wamtakatisha kwa kumuogesha kwa pumba, na kumpaka manukato ya manemane ili aonekane vizuri machoni mwa Wasubi, na anukie vizuri puani mwao, kwao bado watasikia harufu ya uvundo, kwa sababu la kuvunda, halihitaji ubani.
.Si bora wangemsimamisha mhaya? mganda?
Anyway asante Pasco kwa info, majambazi wa kura tumeisha wazoea, Wenye mamlaka yaliyo tukuka walisha acha maagizo nani atangazwe mshindi, tunasubili saa na dakika itimie atangazwe!