BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

Wana JF kutokana na akili zangu ndogo nimekuwa sana najiuliza huu mchezo jinsi unavyoendeshwa kama maigizo vile,

Kwanza washindi wote huwa lazima simu zao zinapatikana,
Halafu Kwa sababu wanarusha live mtazame kajala Kama huwa anapiga ile simu, kingine kila mshindi huwa sio mshiriki wa mara ya Kwanza Lazima akiulizwa atasema kishacheza mara nyingi, Halafu atasema kuwa alishashinda elfu 50 na laki,
Kama mchezo ni bahati nasibu na inaendeshwa Kwa namba Kwanini hakuna namba mpya hata moja kushinda? Yaani mshiriki wa mara ya Kwanza tu,halafu tazama mtu anaepigiwa Simu itaita mara mbili kapokea, yaani Kama mtu kaambiwa shikilia simu tutakucall,

Jamani mimi bado sijaamini huu mchezo kabisa haujanishawishi, Nina hayo Tu

Sent using Jamii Forums mobile app
NIMEKULA ZANGU MIA MBILI GAME ZA JANA UEFA,HAPA NIMEAMKA TAJIRI LEO,MZIGO UMETEMA FULL SHANGWE😀😀😀 MUHINDI NIMEMTIA DOLE LA JICHO LEO😉
 
speaking from experience ...
hii michezo musijaribu kabisa kwani madhara yake ni makubwa mno, kwanza huleta umaskini, huchangia umaskini, na pia huweza kupelekea watu kupoteza hata maisha...na nk..

hio biko, au tatu mzuka etc kuna wizi mkubwa mnoo ambao wanao faidika ni wachache mno...

kwa ushauri wangu kama kweli hii inchi ni ya uadilifu na wapo kwa ajili ya maslahi ya umma washuke pale chini kwenye ile board ya bahat nasibu ichunguzwe kitaalamu uone jinsi formula kandamizi zinavyowa dhulumu wananchi kwa maslahi ya wachache...

wafute tu hio michezo, tutafute njia nyingine za kuwekeza...sasa hivi 80% ya wasio na ajira na wale wenye vijimishahara wanateteza fedha zao huko.

serikali adilifu ifanye ya fuatayo.

kwanza wa review software inatumika kwa tatu mzuka..na hizo biko..hapa sitaandika mno kuna mlolongo ambao najua kwa siasa zetu wakifuatilia watazifunga..

wachezeshaji wachunguzwe kwa kila kitu kuanzia mawasiliano yao maisha yao etc...

washindi wale wakuchaguliwa pia wachunguzwe..na kufuatiliwa...

kingine na cha mwisho... kwa wale wadadisi wapenda ku penetrate na kupiga huku ndo kwenye fursa..
Mkuu tatizo hata serikali imeingilia kati utasikia mkuu wa mkoa anatuambia eti ni fursa kwa hiyo wananchi waendelee kuucheza huo mchezo,,
Hapo jua TRA nao wanakula ela kubwa ya Kodi ndo maana.
 
Mtu mwenye akili zinazofanya kazi vizuri na utashi wa kungamua mambo hawezi poteza muda wake kwenye bahati nasibu na kamari.we hujiulizi wao hawana shida na hela mpaka wakupe wewe?.Katika pronciple za kamari wanakwambia "the house always win".
 
Mkuu tatizo hata serikali imeingilia kati utasikia mkuu wa mkoa anatuambia eti ni fursa kwa hiyo wananchi waendelee kuucheza huo mchezo,,
Hapo jua TRA nao wanakula ela kubwa ya Kodi ndo maana.

nimewasikia kwenye news leo wakitetea kuwa kuna mifumo sijui wame rithi wapi, sijui wamepata asilimia ngapi...
ila kiukweli ni kwamba kwa kutegemea hizi bahati nasibu hakuta kuja na tanzania ya viwanda kamwe....zaidi ya tz ya wsiojulikana kukithiri...
wito wangu ni kwamba bila kujali tiharahei wanapata kiasi gani lakini kama itakuwa ni kwa ajili ya dhuluma.

ndani ya hii michezo kuna uoshwaji wa fedha haramu umejificha humo..tena kwa njia rahisi mno..
 
Hili naona ni tatizo la Dunia wadau maana hizi kampuni hazipo Tanzania tu.

Ni Dunia nzima,Nchi zilizoendelea kama UINGEREZA,marekani na zingine nyingi ndo kuna makampuni mengi zaidi.

Hata Africa mataifa kama SOUTH AFRICA na NIGERIA ndo yanaongoza kuwa na hizi kampuni za betting.

Nafikiri ni upepo ndo unaelekea huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili naona ni tatizo la Dunia wadau maana hizi kampuni hazipo Tanzania tu.

Ni Dunia nzima,Nchi zilizoendelea kama UINGEREZA,marekani na zingine nyingi ndo kuna makampuni mengi zaidi.

Hata Africa mataifa kama SOUTH AFRICA na NIGERIA ndo yanaongoza kuwa na hizi kampuni za betting.

Nafikiri ni upepo ndo unaelekea huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni bora betting ambazo unacheza mwenyewe na Kuamua wapi unaweka pesa, Ila hii ya BIKO na Tatu mzuka ni wizi wa wazi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uongo mtupu mnadanganywa. mimi kuna kaka yangu alishinda gari airtel lakini jamaa wakatuambia ili ashinde toeni helatukatoa. akachukua garikiufupi ni kama tuliinunua kwa bei ya kutupa.nyie mnadanganywa kwenye tv
 
Imani yangu ni kuwa mnaocheza mnaingiza million 600 zawadi inayotolewa ni Million 20 kuna utapeli gani hapo?

Sema uwongo nimeugundua pale wanaposema watakua live saa tatu usiku Itv,Tbc,Etv na Startv ukifuatilia utagundua sio live ni recorded sababu kila kituo wanarusha kwa time yake
 
Mimi nimewapigia simu karibu siku tano mfululizo wanasema tu "MTUMIAJI WA SIMU UNAYEMPIGIA ANAONGEA NA SIMU NYINGINE " nikagundua kuwa huu ni usanii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Betting nzuri ni ya michezo tu km football betting, lakini hiyo michezo mpaka itumike mitambo ndio mshindi apatikane. Kuna mtu aliniambia inawezekana mashine zimesetiwa kutafuta non or low frequency number.
 
Back
Top Bottom