Wana JF kutokana na akili zangu ndogo nimekuwa sana najiuliza huu mchezo jinsi unavyoendeshwa kama maigizo vile,
Kwanza washindi wote huwa lazima simu zao zinapatikana,
Halafu Kwa sababu wanarusha live mtazame kajala Kama huwa anapiga ile simu, kingine kila mshindi huwa sio mshiriki wa mara ya Kwanza Lazima akiulizwa atasema kishacheza mara nyingi, Halafu atasema kuwa alishashinda elfu 50 na laki,
Kama mchezo ni bahati nasibu na inaendeshwa Kwa namba Kwanini hakuna namba mpya hata moja kushinda? Yaani mshiriki wa mara ya Kwanza tu,halafu tazama mtu anaepigiwa Simu itaita mara mbili kapokea, yaani Kama mtu kaambiwa shikilia simu tutakucall,
Jamani mimi bado sijaamini huu mchezo kabisa haujanishawishi, Nina hayo Tu
Sent using
Jamii Forums mobile app