BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

Babu, ukishinda 50m utakuwa kweli na muda wa JF? Saa hizi uko na mawazo kshenz ununue vyerehani vi4 ufungue kiwanda
Chukulia kwamba kwa siku 7 wanacheza biko watu 10000 kila mmoja 1000. Chukua 10,000 x 1,000 x 7= 70,000,000. Na hiyo idadi ya watu 10000 ni kadirio la chini sana katika nchi yenye watu wanakadiriwa million hamsini. Pia mtu mmoja anaweza kucheza zaidi ya mara moja ndani ya hizo siku 7. Kwa ujimla ni kwamba hawa jamaa wanapiga hela sana kuliko hata hiyo wanayotoa. Na ndiyo maana wameweza kutoka sh. 20,000,000 mpaka 50,000,000
Biko hiyo jumatano na jumapili million 50 iv wao pesa wanapata WAP tena kwa 1000

Alafu ww ushinde kirahisi rahisi 2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uongo mtupu Mimi ndo maana sichezi Hiyo michezo

sent using TV ya chogo
Sasa wewe ndiye unataka kupanga nani apate au nani akose. Kitu kikishaitwa bahati nasibu maanake unaweza ukacheza hata mara elfu moja na usibahatike kushinda ndiyo maana ya bahati nasibu. Sasa wewe unataka kucheza leo na tu umeshashinda ! Off course unaweza kucheza kwa mara ya kwanza ukashinda lakini siyo formula na siyo lazima iwe hivyo
 
Shida iliopo kwenye hii nchi,michezo ya kubahatisha inapoanzishwa hakuna mamlaka zinazofuatilia uhalali wake na kama wanafuailia ni pale mwanzoni inapoanza,wakishatoa leseni zao basi wanawaacha wanajifanyia wanavyotaka ,mpaka wakija kushtuka,wananchi wameshaliwa vya kutosha na jamaa wameshatajirika.
 
Wana JF kutokana na akili zangu ndogo nimekuwa sana najiuliza huu mchezo jinsi unavyoendeshwa kama maigizo vile,

Kwanza washindi wote huwa lazima simu zao zinapatikana,
Halafu Kwa sababu wanarusha live mtazame kajala Kama huwa anapiga ile simu, kingine kila mshindi huwa sio mshiriki wa mara ya Kwanza Lazima akiulizwa atasema kishacheza mara nyingi, Halafu atasema kuwa alishashinda elfu 50 na laki,
Kama mchezo ni bahati nasibu na inaendeshwa Kwa namba Kwanini hakuna namba mpya hata moja kushinda? Yaani mshiriki wa mara ya Kwanza tu,halafu tazama mtu anaepigiwa Simu itaita mara mbili kapokea, yaani Kama mtu kaambiwa shikilia simu tutakucall,

Jamani mimi bado sijaamini huu mchezo kabisa haujanishawishi, Nina hayo Tu

Sent using Jamii Forums mobile app
umewaza ka mimi yn cm inapigwa Mara 1 haiiti ikakata halafu MTU akapigiwa tena wala micd call ka 2au 3 hv, halafu pia ile hamaki ya mpokeaji cm inakuwa kama ya kuigiza fulani hv, siyo ya ule mshangao wa kupata lbda 50 mln kwa bahat, kweli hata mimi cjailewa vzr hii bahatinasibu asee.
 
Nimekuwa nikicheza sana BIKO, nimetumia zaidi ya laki tatu sishindi, nimekuwa nikicheza kila baada ya robo saa au kila nikikumbuka nacheza. Lakini sijawahi kushinda hata hiyo milioni Moja. Naomba kufahamu kama kuna mtu aliwahi kushinda millioni Moja BIKO?
TAZAMA HAPA nikacheza elfu kumi, ila katika muda Huo huo niliocheza nikashinda elfu ishirini bado ile hela Yangu ikiendelea kucheza katikati round hiyo wakasema bado mshindi Mmoja nishinde millioni moja, ikaendelea kucheza kucheza hiyo hiyo elfu kumi Yangu nilo cheza, cha ajabu nikashinda elfu 50,000 badala ya 1 million.

KWANINI Baada ya kushinda 20,000 waliniambia bado mtu 1 nishinde 1 million then ile ile elfu kumi Yangu ilipokuwa inaendelea kucheza nilishinda 50,000 badala ya 1 million?


Naomba kufahamu mtu anaposhinda 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 1,000,000 na hiyo 50,000,000 ni vigezo gani huwa mnatumia kuupata huo ushindi??????


KINGINE, huo muda mnatafuta mshindi huwa ni live au huwa ni recorded mnatudanganya mnatafuta mshindi?!! Mnatafuta mshindi muda mchache huo?!! HIYO HUWA NI RECORDED NA SIO MUDA HUO HUWA MNAMTAFUTA NA KUMPIGIA MSHINDI.


OMBI LANGU KWA SERIKALI.

Naomba kampuni inayochezesha huu mchezo, hizo hela wanazozikusanya kutokana na watu kucheza asilimia 90% zitumike kuwa zawadia kwa wanaocheza na kushinda,

Hii kampuni ionyeshe jinsi inavyopata washindi na vigezo vya kushinda

Pia walipe Kodi kutokana na makusanyo wanayokusanya na sio kujitajirisha wao kwa kukusanya hela kwetu kwa njia zisizoeleweka vyema
 

Attachments

  • Screenshot_2017-09-20-19-32-30.png
    Screenshot_2017-09-20-19-32-30.png
    33 KB · Views: 97
Pole ndugu yangu.
Hivi wa tz kwanini mnapenda sana pesa za shortcut hivyo?
Hao ni wapigaji hebu tumieni akili bwana.
Mbona mnakuwa hivyo.
Tafuteni kwa jasho acheni kutaka maisha mazuri kwa njia za mkato.Kwani wao wanataka hasara.
Nan akupe mil 50 hakujui?
Wajinga ndio mliwao.
Siji fanya huo ujinga.
 
Wachezesha kamari/bahati nasibu hawaji kukupa hela bali wanakuja kuchukua hala zako!!
 
UZURI NI KWAMBA HAKUNA ANAYEKULAZIMISHA KUCHEZA.

Soko la wanaohitaji kutapeliwa bado ni kubwa sana, kikubwa weka bidii zaidi. Cheza bahati nasibu kisha nenda kasali kwenye makanisa ya biashara.Hakika mungu atatenda
 
Ndio maana inaitwa bahati nasibu, usilalamike sio bahati yako bro, next time think proper investing channel sio kwenye kamari. Wajinga ndio ...
 
Back
Top Bottom