BIKO inapiga goli la mkono, ni mchezo wa kamari na utapeli tupu

NIMEKULA ZANGU MIA MBILI GAME ZA JANA UEFA,HAPA NIMEAMKA TAJIRI LEO,MZIGO UMETEMA FULL SHANGWE😀😀😀 MUHINDI NIMEMTIA DOLE LA JICHO LEO😉
 
Mkuu tatizo hata serikali imeingilia kati utasikia mkuu wa mkoa anatuambia eti ni fursa kwa hiyo wananchi waendelee kuucheza huo mchezo,,
Hapo jua TRA nao wanakula ela kubwa ya Kodi ndo maana.
 
Mtu mwenye akili zinazofanya kazi vizuri na utashi wa kungamua mambo hawezi poteza muda wake kwenye bahati nasibu na kamari.we hujiulizi wao hawana shida na hela mpaka wakupe wewe?.Katika pronciple za kamari wanakwambia "the house always win".
 
Mkuu tatizo hata serikali imeingilia kati utasikia mkuu wa mkoa anatuambia eti ni fursa kwa hiyo wananchi waendelee kuucheza huo mchezo,,
Hapo jua TRA nao wanakula ela kubwa ya Kodi ndo maana.

nimewasikia kwenye news leo wakitetea kuwa kuna mifumo sijui wame rithi wapi, sijui wamepata asilimia ngapi...
ila kiukweli ni kwamba kwa kutegemea hizi bahati nasibu hakuta kuja na tanzania ya viwanda kamwe....zaidi ya tz ya wsiojulikana kukithiri...
wito wangu ni kwamba bila kujali tiharahei wanapata kiasi gani lakini kama itakuwa ni kwa ajili ya dhuluma.

ndani ya hii michezo kuna uoshwaji wa fedha haramu umejificha humo..tena kwa njia rahisi mno..
 
Hili naona ni tatizo la Dunia wadau maana hizi kampuni hazipo Tanzania tu.

Ni Dunia nzima,Nchi zilizoendelea kama UINGEREZA,marekani na zingine nyingi ndo kuna makampuni mengi zaidi.

Hata Africa mataifa kama SOUTH AFRICA na NIGERIA ndo yanaongoza kuwa na hizi kampuni za betting.

Nafikiri ni upepo ndo unaelekea huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora betting ambazo unacheza mwenyewe na Kuamua wapi unaweka pesa, Ila hii ya BIKO na Tatu mzuka ni wizi wa wazi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uongo mtupu mnadanganywa. mimi kuna kaka yangu alishinda gari airtel lakini jamaa wakatuambia ili ashinde toeni helatukatoa. akachukua garikiufupi ni kama tuliinunua kwa bei ya kutupa.nyie mnadanganywa kwenye tv
 
Imani yangu ni kuwa mnaocheza mnaingiza million 600 zawadi inayotolewa ni Million 20 kuna utapeli gani hapo?

Sema uwongo nimeugundua pale wanaposema watakua live saa tatu usiku Itv,Tbc,Etv na Startv ukifuatilia utagundua sio live ni recorded sababu kila kituo wanarusha kwa time yake
 
Mimi nimewapigia simu karibu siku tano mfululizo wanasema tu "MTUMIAJI WA SIMU UNAYEMPIGIA ANAONGEA NA SIMU NYINGINE " nikagundua kuwa huu ni usanii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Betting nzuri ni ya michezo tu km football betting, lakini hiyo michezo mpaka itumike mitambo ndio mshindi apatikane. Kuna mtu aliniambia inawezekana mashine zimesetiwa kutafuta non or low frequency number.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…