ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI
ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako
UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?
Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?
Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?
Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya
Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao
Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo
Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?
Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?
Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo
Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18
Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia
Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌
Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!
Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi
Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana
Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?
Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?
Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?
Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?
Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?
Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?
MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?
ShesRise_1 ✋️