Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Hizo bikra zinapigiwa kelele tu huku mtandaoni..

Lakini ukiingia kitaa hao hao wapiga kelele za bikra wanapita na chochote kinachopatikana iwe un bikra single maza , mishangaza yenye mapengo yani ni tafrani tu.
na kiuhalisia mwanaume huwa hapati mwanamke mwenye vigezo anavyotaka yeye bali hufikiq hatua anachuakua anayepatikana kwa wakati huo
Hapo ni pale mwanaume ana shida ya mwanamke atafanya chochote, na mwanamke yeyote atakaye katiza kwenye 18 anapita naye, ndio maana utaona hata vichaa wanabeba mimba.

Tukubaliane tu ukiwa nayo bikra umshukuru Mungu umekwepa mishale mingi, au Lah hauna jipige moyo konde sogea mbele lakini asibebeshwe lawama mwanaume eti alinitoa, au alinirubuni sijui kwa maneno yoyote, kama ni issue ya kutongozwa hata raisi anatongozwa kipindi cha sodoma hata wale malaika vijeba waliwatamani wapite nao
 
Mimi nitawatetea waliobakwa nyie wa chips mayai mtajua wenyewe! Pongezi ziende kwa muumba hapa kweli kawashughulikia wanawake! Ukitaka wanawake watokwe na mishipa ya shingo we leta mada ya bikra. Na mwisho kama bikra si chochote kwanini ulete mada kama hii?
Jifunze kusoma nakuelewa
Kama hujaelewa usichangie kabisa fatilia comment

NB : huna hoja ya kujibu bandiko langu ndio maana unaweweseka
 
Kwani bikra tunazo jadili hapa si za watu kama ww ?
Mm nimekuuliza hivyo Nina maana yangu
Kama bikra yako ilitolewa kwa kubakwa na ukiwa mdogo hujielewi basi Uzi wako una hoja ,lakini kama ilitolewa ukiwa mkubwa hii mada yako ni takataka.
Mada yangu sio takataka
Imekuzidi uwezo ndio maana umeacha kuijadili unakimbilia kutaka kujadili maisha yangu binafsi

Kaa kwa utuo bro
Makasiriko hapa ni marfuku
 
Hapo ni pale mwanaume ana shida ya mwanamke atafanya chochote, na mwanamke yeyote atakaye katiza kwenye 18 anapita naye, ndio maana utaona hata vichaa wanabeba mimba.

Tukubaliane tu ukiwa nayo bikra umshukuru Mungu umekwepa mishale mingi, au Lah hauna jipige moyo konde sogea mbele lakini asibebeshwe lawama mwanaume eti alinitoa, au alinirubuni sijui kwa maneno yoyote, kama ni issue ya kutongozwa hata raisi anatongozwa kipindi cha sodoma hata wale malaika vijeba waliwatamani wapite nao
Sasa kumpata yoyote kumbe imekubali sasa unaweza pata aliyonayo au la!!!!

Kwangu mimi bikra sio inshu na katika maisha kiujumla bikra si chochote wala lolote ndio maana wavulana wako bize kulilia bikra na wanaume wako bize kusaka wanawake watakao wapa maana ya maisha
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?

Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao

Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?

Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?

Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia

Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌


Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi


Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?

Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?

Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?

Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?

MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️
Kama wewe unataka bikra, basi nawe jitunze uwe bikra, full stop.

Haiwezekani wewe una 5BC halafu unataka mwenye 0BC!!!
 
Mbona sasa wewe ni mpumbavu kuliko wao?
Bila shaka ww ni miongoni wa wapumbavu walio tolewa bikra kwa chips alafu unataka lawama abebe uliye mlia chips eti kwa nn akukataa kukutoa bikra😂😂😂😂😂.
Mwanaume na mwanamke wanapo fanya uzinzi %95 ya matokeo ya huo uzinzi utayabeba mwanamke na si mwanaume.

Hivyo wanaume wengi huwa hawajali kwa sababu wa sio waathirika.
 
Sasa kumpata yoyote kumbe imekubali sasa unaweza pata aliyonayo au la!!!!

Kwangu mimi bikra sio inshu na katika maisha kiujumla bikra si chochote wala lolote ndio maana wavulana wako bize kulilia bikra na wanaume wako bize kusaka wanawake watakao wapa maana ya maisha
Suala la Bikra libaki kwa mwanamke mwenyewe, akiipoteza akiitunza asilaumiwe mtu maana imewekwa katika kiungo chake cha uzazi, ni sawa na swala la ushoga anayelaumika ni mwanaume mwenyewe, ndio maana kuna kauli mbiu ya kulinda mgongo. Na wanawake kama mnaona suala la Bikra linawaumiza bado kuna wanaume wanahitaji bikra kutoka kwenu wenye nazo basi hiyo kauli pia ihamishwe kwenu mhamasishane na muhamasishe mabinti wafunike mapaja yao
 
Bila shaka ww ni miongoni wa wapumbavu walio tolewa bikra kwa chips alafu unataka lawama abebe uliye mlia chips eti kwa nn akukataa kukutoa bikra😂😂😂😂😂.
Mwanaume na mwanamke wanapo fanya uzinzi %95 ya matokeo ya huo uzinzi utayabeba mwanamke na si mwanaume.

Hivyo wanaume wengi huwa hawajali kwa sababu wa sio waathirika.
Umeanza kunishambulia mie binafsi sasa?
😂😂😂 mbona siko huko kabisaa, Sex sio vitu vyangu mbona.
 
Umeanza kunishambulia mie binafsi sasa?
😂😂😂 mbona siko huko kabisaa, Sex sio vitu vyangu mbona.
Ww mbona umenushambulia kwa kunii ta mpumbavu?
Kwa hiyo tangu uzaliwe hujui dushe la mwanaume?acha zako ww.
 
Nadhani tatizo moja wapo ni kuacha kufuata mila na desturi zetu, pia misingi imara ya tamaduni zetu. Zamani msichana akijulikana sio bikra, familia au ukoo ulikaa na kujua nani aliyesababisha mtoto wao kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Faini zilitolewa au hata wengine kufukuzwa. Wanaume ambao walikuwa hawajaoa walifundishwa kuheshimu wanawake walioolewa na wasichana ambao bado.

Sasa dunia ya sasa, kwa watoto wanazaliwa nje ya ndoa, elimu ya kumheshimu na kumjali msichana/mwanamke haipo katika msisitizo imara na hata waliozaliwa katika ndoa nao pia wamekosa elimu hii.
 
Suala la Bikra libaki kwa mwanamke mwenyewe, akiipoteza akiitunza asilaumiwe mtu maana imewekwa katika kiungo chake cha uzazi, ni sawa na swala la ushoga anayelaumika ni mwanaume mwenyewe, ndio maana kuna kauli mbiu ya kulinda mgongo. Na wanawake kama mnaona suala la Bikra linawaumiza bado kuna wanaume wanahitaji bikra kutoka kwenu wenye nazo basi hiyo kauli pia ihamishwe kwenu mhamasishane na muhamasishe mabinti wafunike mapaja yao
Mbona wenzetu mnalilia vitu ambavyo viko kwa mwingine?¿???

Wewe zaa wako, hamasisha ukoo wako na familia yenu vijana wa kike wawe na bikra maana hiyo ndiyo kipaumbele chenu.

Mimi binti zangu na familia yangu nina vingi vya kuwahamasisha bikra sio kipaumbele chetu na haijawahi kuleta utajiri sehemu yoyote ile.
 
Dada mtoa mada ni kweli kuna wasichana wanapitia ukatili wa kingono lakini tuseme ukweli mabinti wengi wamekua wahuni kwaiyo kwa kiasi kikubwa bado mabinti wao ndio wenye changamoto wao ndio walitakiwa wawe na misimamo kujilinda zaidi usichana wao kwaajili ya heshima yao kwenye Ndoa endapo atakuja kupata mume.

Juzi tuh apa tumeona mabinti wa fomu4 wanatamba wamemaliza mitihani yao wanaenda mtaani kutembea na waume za watu pale huwezi kukuta Binti mwenye bikra na wanajivunia kabisa uhuni wao hiyo inaonyesha kabisa kwa asilimia kubwa mabinti wenyewe ndio tatizo zaidi ukiachana na hao wasichana kazaa wanapitia ukatili wa kingono.
 
Back
Top Bottom