Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Are you out of your mind? Kwani wewe mwanamke hujui kuwa mwanaume akikutongoza anataka nini mbali na hiyo kukuoa? Kaa chini ufikiri wanaume ni hawa hawa, na wanawake ni hawa hawa miaka ya nyuma wanawake waliwezaje kukaa na bikira zao? Wanaume wenye ushawishi hawakuwepo, wanaume wenye pesa hawakuwepo? Au tuseme wanaume wa zamani walikuwa hawana tamaa ya wanawake?

Ukweli ni huu wanawake walikuwa na misimamo hawakuwa easy going ilikuwa unatongoza mwanamke mwaka mzima, akikukubalia mnaanza safari nyingine ya kutongoza upate mbususu na tena ukianza hizo stori unapigwa Kibuti, vipi wanawake wa sasa? Hawa wanaoshindana tena wengine wanacheza kwa kuweka chupa inaingia kwa Bibi kule ndio uko kupeleka lawama kwa wanaume kuhusu kupoteza bikira zao?

Vitoto havina adabu siku hizi, vinajipeleka vyenyewe kwa boda boda kwa tamaa za lift, chips kavu na peps,

NARUDIA TENA ISSUE YA MWANAMKE KUTOKUWA NA BIKRA NI LA MWANAMKE MWENYEWE, NA LAWAMA ANAIBEBA MWENYEWE NA NDIO MAANA HATA MATOKEO YAKE ANAYAPATA MWENYEWE. FIKIRIA MWENYEWE ULIPOTEZAJE BIKRA YAKO?.
Mwenye uzi wake anawatetea under-age mkuu. Kwamba hawana uwezo wa kuhimili vishawishi vya Wanaume. Hapo vipi?
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?

Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao

Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?

Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?

Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia

Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌

Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi

Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?

Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?

Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?

Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?

MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️
Bikra ya mwanaume imekaaje! Ambae hajawahi ku -sex maishani nae ni bikra. Sasa huyu aungane na mwanamke bikra, ndio ndoa halisi na ya kudumu. Kila mtu anamjua mwenzake ndivyo alivyo. Kama ni bamia na wanaume wote ni bamia.
 
Mwanamke analaumiwa sababu yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho,(kukataa)
Mwanaume anapotongoza haweki ulazima wa kukubaliwa.
 
Mbona wenzetu mnalilia vitu ambavyo viko kwa mwingine?¿???

Wewe zaa wako, hamasisha ukoo wako na familia yenu vijana wa kike wawe na bikra maana hiyo ndiyo kipaumbele chenu.

Mimi binti zangu na familia yangu nina vingi vya kuwahamasisha bikra sio kipaumbele chetu na haijawahi kuleta utajiri sehemu yoyote ile.
Sisi tena ndio tunalilia? Kwa mujibu wa mtoa mada sisi ndio tunapaswa kulaumika kwa vitu ambavyo viko kwenye miliki ya wengine?

Ndio maana nimesimama upande wa opposer na kusema hapana habari ya bikra ya MWANAMKE alaumiwe mwenyewe anapoteza nje ya matarajio na akiitunza apongezwe na sio lawama za kupoteza bikira atwishwe mwanaume.

Na kama Bikra hazina umuhimu wowote na mjadala huu ufungwe
 
Mada yangu sio takataka
Imekuzidi uwezo ndio maana umeacha kuijadili unakimbilia kutaka kujadili maisha yangu binafsi

Kaa kwa utuo bro
Makasiriko hapa ni marfuku
Mbona kama ww ndo una makasiriko kwa sababu swali nililo kuuliza jibu lake ni rahisi sana tu sasa nashangaa unapaniki.
Kwani hizo bikra tunazo jadili hapa ni za mbwa au wanazo watu kama ambao pia na wao suala la bikra ni suala binafisi ?
Au ww ya kwako ni tofauti na ya wengine mpaka isijadiliwe kama unavyo jadili za wengine?
Nimekuuliza hili swali nikiwa na maana yangu ili nijue umesimamia engo gani katika mada yako,kama bikra yako ilitolewa kwa kubakwa,au ukiwa na umri mdogo sana usio jielewa basi una haki ya kuanzisha mada ya kuhoji uhalali wa madai ya wanaume kutaka bikra.
Lakini kama ilitolewa ukiwa mtu nzima unajielewa huna haki ya kuja kuhoji uhalali wa madai ya wanaume kutaka bikra.
 
Kwani bikra tunazo jadili hapa si za watu kama ww ?
Mm nimekuuliza hivyo Nina maana yangu
Kama bikra yako ilitolewa kwa kubakwa na ukiwa mdogo hujielewi basi Uzi wako una hoja ,lakini kama ilitolewa ukiwa mkubwa hii mada yako ni takataka.
Nimeona wengi hawajamuelewa mleta mada,

Issue ni kwamba,kwa kawaida,Mwanamke anatolewa bikra yake na mwanaume,haijalishi walipatana au hawakupatana mpaka ikapelekea huyo mwanamke kupoteza hiyo bikra yake,kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba,bikra hiyo imepotea kwa ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume,

Hoja ya mleta mada anauliza kwamba,sasa kwanini lawama ziende kwa mwanamke peke yake?
Nafikiri mjadala upo kwenye hiyo hoja.
 
Mwenye uzi wake anawatetea under-age mkuu. Kwamba hawana uwezo wa kuhimili vishawishi vya Wanaume. Hapo vipi?
Hapana wanauwezo Mkuu, sema tamaa zimewazidi, wanataka vitu vizuri bila kujua kuwa vitu vizuri ni gharama. Wanapenda mteremko wapelekwe shule na boda na kuchukuliwa na boda bure bure bila kujua hiyo boda inatumia mafuta. Hilo ni tatizo kubwa, na kama kweli tunakubaliana hawawezi kuhimili ushawishi basi lawama ziende kwa wazazi na walezi wao kuliko eti wao kupoteza bikira lawama ziende kwa wanaume hapo hapana
 
Mbona wenzetu mnalilia vitu ambavyo viko kwa mwingine?¿???

Wewe zaa wako, hamasisha ukoo wako na familia yenu vijana wa kike wawe na bikra maana hiyo ndiyo kipaumbele chenu.

Mimi binti zangu na familia yangu nina vingi vya kuwahamasisha bikra sio kipaumbele chetu na haijawahi kuleta utajiri sehemu yoyote ile.
Kwa hiyo ww kwako mabinti zako kutunza na kujua thamani ya miwili yao sio kipaumbele kwako?
Sasa mbona mlikuwa mnawashambulia wanafunzi walio kuwa wakijitapa kutembea na waume za watu kuwa hawana maadili?
 
Nimeona wengi hawajamuelewa mleta mada,

Issue ni kwamba,kwa kawaida,Mwanamke anatolewa bikra yake na mwanaume,haijalishi walipatana au hawakupatana mpaka ikapelekea huyo mwanamke kupoteza hiyo bikra yake,kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba,bikra hiyo imepotea kwa ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume,

Hoja ya mleta mada anauliza kwamba,sasa kwanini lawama ziende kwa mwanamke peke yake?
Nafikiri mjadala upo kwenye hiyo hoja.
Swali litabaki pale pale kati ya hao wawili mwenye mali ni yupi? Yaani mwenye Bikra ni yupi? Kama MWANAMKE alikubali bikra yake itoke na yeye ameshiriki basi lawama zinabaki kwake kwasababu yeye ndiye aliyepewa dhamana ya kuitunza
 
Nimeona wengi hawajamuelewa mleta mada,

Issue ni kwamba,kwa kawaida,Mwanamke anatolewa bikra yake na mwanaume,haijalishi walipatana au hawakupatana mpaka ikapelekea huyo mwanamke kupoteza hiyo bikra yake,kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba,bikra hiyo imepotea kwa ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume,

Hoja ya mleta mada anauliza kwamba,sasa kwanini lawama ziende kwa mwanamke peke yake?
Nafikiri mjadala upo kwenye hiyo hoja.
Mkuu ww ukiacha mlango wazi wezi wakaingia wakaiba kati ya hao wezi na ww nani mpumbavu?
Mlango wa zinaa uko kwa mwanamke na ndio maana mwanamke halali na Kila anaye mtongoza bali analala na aliye mkubalia kulala naye.
Ni upumbavu kumtupia kipande cha nyama mbwa alafu utegemee eti atajizuia kukila eti kwa kuofia usiku mtakula ugali bila mboga.
Mwanaume atalaumiwa iwapo atakuwa amebaka,au amerubuni kibinti kidogo kisicho jielewa lakini kwa binti mkubwa huo ni upumbavu wake mwanaume hana lawama zozote.
 
Mada na iishie hapa, maana mtoa mada ameingia mitini
 
Et hata ukipata kibali hivi huoni aibu kwanini unaomba kibali cha kumtoa bikra msichana mdogo huku ukijua humuoi?

Unajiangalia unachoandika kweli?

Kwanini umshawishi mwanamke tena mdogo ambae bado hajakomaa kifkra

Kwanini usimlaumu huyu mwanaume mshenzi?

Akili gani hizi ?
Yani hapo tunatafuta kichaka cha kutafuta nani anasitahili kubebeshwa lawama,,, hatuwezi kupata suluhisho.

Asilimia kubwa sana ya mabinti iwe kwa kulazimishwa, kubakwa, au kushawishiwa kwa namna fulani huwa wanatoa green light indirect. Though naelewa kuna wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ni sawa kabisa.

Suala la mwili ni wajibu mama wa mwenye nao, wengine wote ni supporters.

Na hili suala la ukomavu wa kifikira ni kweli, ila mara nyingi linatumika kama excuse.
 
Nadhani tatizo moja wapo ni kuacha kufuata mila na desturi zetu, pia misingi imara ya tamaduni zetu. Zamani msichana akijulikana sio bikra, familia au ukoo ulikaa na kujua nani aliyesababisha mtoto wao kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Faini zilitolewa au hata wengine kufukuzwa. Wanaume ambao walikuwa hawajaoa walifundishwa kuheshimu wanawake walioolewa na wasichana ambao bado.

Sasa dunia ya sasa, kwa watoto wanazaliwa nje ya ndoa, elimu ya kumheshimu na kumjali msichana/mwanamke haipo katika msisitizo imara na hata waliozaliwa katika ndoa nao pia wamekosa elimu hii.
Hili wanaume wanalikwepa wala hawataki kulizungumzia wao wanadai mwanamke ndio mwenye tatizo
 
Dada mtoa mada ni kweli kuna wasichana wanapitia ukatili wa kingono lakini tuseme ukweli mabinti wengi wamekua wahuni kwaiyo kwa kiasi kikubwa bado mabinti wao ndio wenye changamoto wao ndio walitakiwa wawe na misimamo kujilinda zaidi usichana wao kwaajili ya heshima yao kwenye Ndoa endapo atakuja kupata mume.

Juzi tuh apa tumeona mabinti wa fomu4 wanatamba wamemaliza mitihani yao wanaenda mtaani kutembea na waume za watu pale huwezi kukuta Binti mwenye bikra na wanajivunia kabisa uhuni wao hiyo inaonyesha kabisa kwa asilimia kubwa mabinti wenyewe ndio tatizo zaidi ukiachana na hao wasichana kazaa wanapitia ukatili wa kingono.
Huo uhuni wanafanya na akina nani?
 
Yani hapo tunatafuta kichaka cha kutafuta nani anasitahili kubebeshwa lawama,,, hatuwezi kupata suluhisho.

Asilimia kubwa sana ya mabinti iwe kwa kulazimishwa, kubakwa, au kushawishiwa kwa namna fulani huwa wanatoa green light indirect. Though naelewa kuna wanaofanyiwa vitendo vya ukatili ni sawa kabisa.

Suala la mwili ni wajibu mama wa mwenye nao, wengine wote ni supporters.

Na hili suala la ukomavu wa kifikira ni kweli, ila mara nyingi linatumika kama excuse.
Hapa hakuna wakutipiwa lawama
Kinachoshangaza ni wanaume kujitoa kwenye hili swala kama vile vile hawahusiki
 
Back
Top Bottom