Bila dhuluma wala kukimbiza wafanyabiashara Rais Samia aweka rekodi mpya Ukusanyaji mapato | TRA yakusanya kodi ya TZS 1.9T mwezi Sept 2021,kazi iendelee kwa kasi & weledi zaidi,
==================================
Wakati Hayati Rais Mkapa anaondoka madarakani serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs 322BL kwa mwezi,Wakati Mzee Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka madarakani serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs 850BL kwa mwezi na Wakati Hayati Rais Magufuli anaaga dunia Serikali yake ilikusanya wastani wa Tshs 1.4trl kwa Mwezi,
Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuapishwa kuiongoza Serikali kwa awamu ya Sita aliapa kamwe hatokubali serikali kukusanya Kodi ya dhuluma namnukuu "Niheri tukusanye kidogo lakini kiwe cha halali kitatufaa " alisikika kwa Upole na unyenyekevu akiwaasa wateule wake,Rais Samia alishangaa watu kudaiwa kodi za nyuma "Presumptive Tax accessment " wakati wanazo tayari "Tax Clearance " toka kwa haohao wanaowadai tena,Kitendo hiki Rais Samia alikiita kuwa kwa Mujibu wa Mungu na dini huo ni "udhulumati "
Wakati Serikali ya Rais Samia imepanga kutumia Jumla Tshs 36.33trl kwa Mwaka wa fedha 2021|2022 mwaka ulioanza tarehe 01|07|2021 ambapo mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa
Tshs 26.03trl, sawa na 71.7% ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, mapato ya kodi ni Tshs 22.18trl, sawa na 13.5% ya Pato la Taifa. Aidha, Serikali inalenga kukusanya
mapato yasiyo ya kodi ya Tshs 2.99trl na mapato kutoka
vyanzo vya Halmashauri ni Tshs 863.9BL,
Mungu ni mwema,kama kasi yetu ni Tshs 1.9trl kwa mwezi,Chukuaa 1.9trl zidisha kwa miezi 12 utapata jumla ya Tshs 22.8 tutavuka lengo kwa 3% naomba mfahamu tangu uhuru hakuna Rais aliwahi kutenga Tshs 36.33trilioni kwa aajili ya bajeti ni Samia and only Samia,
Tuendelee kulipa kodi kwa hiari kwaajili ya maendeleo yetu na ya watoto wetu na yawatoto wao,Tanzania tuko vizuri Sana kwa sasa pengine tangu uhuru japo ni niukweli mchungu kwa wengine.
#Kazi iendelee kwa kasi & nguvu zaidi
Be blessed & Happy Sunday
=============================
VIVA SAMIA VIVA || VIVA TANZANIA VIVA
View attachment 1961007