Bila dhuluma wala kukimbiza wafanyabiashara, Rais Samia aweka rekodi ukusanyaji mapato

Ati watanzania tunakupenda sana, tumekutuma uwe msemaj wetu??
Wewe kama unampenda nenda kanywe nae urojo uko kisiwandui.
Kifupi hatujakutuma ivyo hacha ufala.
Huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

Nimnyenyekevu na mpole sana,

Hana majigambo kabisa,

Mungu akulinde Rais wetu

Watanzania tunakupenda sana,
 
Miamala na tozo za ktk umeme, hata mie ningekusanya hizo, tena zaidi maana ningeziba magepu ya ufisadi na upi

Mwacheni Magufuli apumzike uongozi wake bado wakumfikia msimlinganishe, fanyeni yenu, pia kipindi chake hizo tozo tunazokamuliwa mpaka damu hazikuwepo.
Kwakweli uongozi wa kikatili namna ile na asiwepo hata wa kufikia hata theluthi yake tu.
 
Kurudi kwa wafanyabiashara na Wawekezaji ambao walihamishia shughuli zao nchi jirani na compliance ya walipa kodi ni miongoni mwa sababu za kuongezeka mapato.

Sababu nyingine ni Utaratibu wa kulipia maduhuli yote ya serikali kuu kwa njia ya mitandao . Hatua inayofuata serikali ijielekeze kuhakikisha mapato yote ya serikali za mitaa yanakusanywa kwa njia ya stakabadhi za mitandao hata Kama huduma hiyo wame-contract out,hapo serikali ndiyo itapata mgao wake halisi.

Kuna maeneo bado wananchi wanaolipia gharama za huduma ya ubebaji taka au usafi kwa stakabadhi za mikono, utaratibu huu unakosesha mapato kwa mwenye kampuni na Serikali ya mtaa.
 
Makusanyo ya kodi kupanda au kushuka ni kawaida tu ila najua hata angekuwepo jiwe makusanyo yangependa sababu data nyingi zimeanza kupikwa .
Kwa muda huu ambao kuna mfumko wa bei mwezi September zikusanywe trioni 1.9 tumeanza kurudi kuleeeeeee kwa ( praise team).
Chief Hangaya mwenyewe alisema hii miezi mitatu najua mapato yatapungua
4,5,6 mbona hatukuona hizo takwimu
Alijua atakuja na takwimu za kupika huku mbeleni.
 

Bila dhuluma wala kukimbiza wafanyabiashara Rais Samia aweka rekodi mpya Ukusanyaji mapato | TRA yakusanya kodi ya TZS 1.9T mwezi Sept 2021,kazi iendelee kwa kasi & weledi zaidi,​

==================================
Kitu ambacho hujui ni kuwa kodi nyingi hukadiriwa na hugawanywa kwa robo mwaka. Ja- march, April_ June, July- Sept, na Oct- Dec. Kwa hiyo miezi ambayo kodi huwa juu ni March , June , Sept, na Dec. Kupata kiwango kikubwa Sept haina maana uchumi umekuwa sana na kodi hiyo ndiyo wastani wa makusanyo kwa mwezi.
 
Srma haikusaidia kuwashawishi NEC kumtangaza
NEC haiwezi kumtangaza mtu ambae hakuchaguliwa na wananchi. Ngoja nikupe orodha ya NEC inavyotangaza wale waliochaguliwa na wananchi... Mwaka 2005 Lisu, dr Slaa, Zito na wengine wengi wa upinzani walichaguliwa na wananchi kuwa wabunge wao. NEC ikawatangaza, mwaka 2010 Mbowe, Lisu, Zito nk walichaguliwa na wananchi NEC ikawatangaza, mwaka 2015 hivyo hivyo Mbowe, Lisu, Sugu, Zito, Pro Jay nk walichaguliwa na wananchi NEC ikawatangaza, mwaka. 2020 wagombea wao walikuwa wabovu akiwemo mwenyekiti wao Mbowe ambae alizomewa na kutupiwa chupa za maji na wapiga kura wake kule Hai.

Hii ni baada ya wapiga kura hao kushtukia ulaghai wake wa kwenda Hai unapokaribia uchaguzi afu baada ya uchaguzi anakimbia jimbo lake na kuja kuishi Dar, huku akifanya safari mbali mbali za kwenda kula bata na familia yake Dubai, Afrika kusini, kususia vikao vya bunge kwa sababu za kijinga nk, huku akiwatelekeza wapiga kura wake wapambane na hali zao. Kwahiyo style hiyo ya mwenyekiti na genge lake kina Sugu, Lema nk ndio lilifanya wawanyime kura.
 
2025 hakuna uchaguzi - kama mtachaguana wenyewe kwa wenyewe sawa!!
 
Huu ni ugonjwa mkubwa sana kwako kusifu makusanyo feki ya mapato wakati miradi mingi ya manufaa imesimamishwa, hakuna ununuzi mpya wa ndege, hakuna ujenzi mpya wa madaraja na miundo mbinu mingine ikiwemo stendi ya Magufuli kumalizia imekuwa shida, hakuna ujenzi mpya wa meli na ukarabati, wafanya biashara wanatoa risiti feki au kadirio la chini ya thamani halisi ya manunuzi.

Hapo inathibitisha kwamba wananchi wa kawaida ndio wajenzi wa uchumi bila kunufaika maana kodi zote zimeelekezwa kwao .

Kwa kifupi mapato yako zaidi ya hapo ila yalikoelekea haijulikani.

Haiwezekani mfanyabiashara anaandika risiti ya thamani ya chini na ukihoji anakwambia rudisha biadhaa yangu ukatafute atakaye kupa risiti ya thamani halisi.

Kwa kulinganisha na namba ulizoweka ilitarajiwa kuwianisha na kitu gani kifanyika kipya cha maana na kinaonekana kwa watu waone na kukiri kwamba ni kweli inastahili lakini hakuna lolote

*Sifa sifa sifa zisizo na tija kwa taifa na watu wake
 
Mungu aende na Mama mpaka 2030 kwa ksihindo kikuu, kama alivyowahi kwenda na watu wanne waliosababisha kukimbia majeshi ya washami, maadui ambao nchi yao iliyokuwa na chakula tele wakati wa njaa kali. 2025-2030 NjIA ni SamIA
 

Bila dhuluma wala kukimbiza wafanyabiashara Rais Samia aweka rekodi mpya Ukusanyaji mapato |​

Mama ni kiboko yao na hapo TRA wamelega Sana watu hawadai risiti na wafanyabiashara hawatoi risiti yaani makusanyo yangevuka malengo ya serikali..

Ila kwa kasi ya uwekezaji unaoongezeka next year makusanyo yatakuwa makubwa Sana.

Chief Hangaya anaendelea kuupiga mwingi 👇



 
Miradi gani iliyosimama? Miaka 6 yote kwa nini hamkumaliza hiyo miradi?
 
Humo humo kuna tozo za simu humo humo kuna tozo za Luku
Harafu unaleta unafiki


magufuli hakutoza hizo
Kikwete hakutoza hizo
Mkapa hakutoza hizo


Kimberembere kibaya Sana

Chawa kama chawa
Hueleweki kitu we mburula tozo hazihusiki hapa..

Ukute hujawahi fanya hata muamala ukaangalia mchanganuo wake ndio maana unaongea pumba.Tozo haziendi TRA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…