Fursakibao
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 6,813
- 11,540
Umeharibu kufikiria kuwa wanaolipa kodi za majengo asilimia kubwa sio wahusika?Huo ni mtazamo mpya wa ukusanyanji wa kodi, kila mwananchi sasa anachangia pato la taifa maskini kwa tajiri, maskini sasa anaweza kusimama kifua mbele kwamba na yeye ni muhimu katika Taifa - anachangia ujenzi wa kituo cha afya, madarasa na barabara. Kodi za majengo zimekuwapo zaidi ya miaka 10, kama kuna watu wanashangaa mwaka huu- hii ni dhahiri kuwa watu wengi walikuwa wanakwepa kulipa. Hongera kwa awamu ya Sita kwa kungamua hayo.