Congo nafikiri unamaanisha DRC/RDC is a failed state kinachendelea kule ni looting, virtually sio uwekezaji - tangu enzi za mfalme Leopold II.
Huko kwingine ni suala la kuwa na kiongozi dikteta mwenye maono, utashi na uelewa wa mikakati thabiti ya kuiletea nchi yake maendeleo. Mfano mzuri kabisa ni wa Lee Kuan Yew wa Singapore. Bila shaka unajua habari yake. Ndiye aliyehamasisha usemi wa “benevolent dictator”. Kagame anajitahidi kufuata hilo. Tatizo la madikteta ni ile tamaa ya kutohojiwa wakijinufaisha kibinafsi.
Mexico ni demokrasia ingawa ieelemewa sana na wauza madawa ya kulevya.
China ni mfano wa kipekee wa utawala wa kundi la kidikteta lenye maono, mbinu na mikakati ya hali ya juu ya maendeleo na nguvu ya taifa. Heshima ya kipekee inamuendea Deng Xiaoping aliyepindua na kutawala China tangu 1978-1989 baada ya Mao. Huyu ndiye aliyeijenga China Mpya - the architect of Modern China kwa kuifungua na kuingiza uchumi wa soko. Ndio wakati mamia ya wawekezaji toka US na Ulaya walipovamia China na kusisimua utajiri tunaouona leo hii. Alitaka China iwe ya kidemokrasia kama Marekani na Ulaya. Lakini wahafidhina akina Xi wakaweka Breki na kurejesha enzi za kutukuza mtu mmoja - lakini bila kutibua mwelekeo wa uchumi.
TANZANIA SASA … Ni udikteta usio na vision wala utashi wa maendeleo ya nchi. Hakuna mikakati, miongozo wala taasisi imara za kuelekeza maendeleo. Mfumo wa uongozi umegubikwa na upendeleo (patronage), undugu (nepotism), uchawa (sycophancy), ufisadi (graft), wizi wa dola (kleptocracy) na kila takataka ya hujuma. Nchi imegeuzwa mgodi wa kujichotea. Hakuna mwenye uchungu na nchi. Kama vile sote ni wageni tunasaka fursa za kusanya na kusepa!
Kipaji kinachopewa uzito ni uchawa na na namna kupiga propaganda za hali ya juu kuhakikisha wananchi (mazuzu) wanatulia kwa amani huku mchezo ukiendelea.
US na Ulaya walijua kuwa hulka kuu ya binadamu ni UBINAFSI. Hivyo socialism haiwezekani (msome George Orwell katika Animal Farm) na udikteta hauna UTU. Hivyo walipambana kwa damu na jasho kutengua nguvu za wafalme na madikteta na kujiletea katiba imara zinazowahakikishia demokrasia ya kweli, haki za binadamu, uhuru wa mtu binafsi, fursa sawa, miongozo makini na uwezo wa kutekeleza mikakati thabiti ya maendeleo.
Hivyo mnapokana demokrasia na haki za binadamu na kutarajia maendeleo chini ya udikteta - eti kama China, Rwanda au Morocco jiulizeni kama kweli mnakielewa mnachojiombea. Bila kusahau kuwa kuna tyranny, despotism, dictatorship, benevolent dictatorship, petty dictatorship (udikteta uchwara), socialism, communism, democracy, socia democracy, liberal democracy, capitalism, etc. 😁 BE HONEST because only the truth will set you free.