Bila kujali kelele na yaliyosemwa juu ya Hayati Magufuli, kuna ulazima wa haraka sana kumpata mwingine wa aina yake



Spoken like a pure mwalimu wa darasa la 7A shule ya msingi Tanganyika.
 
Tunahitaji mabadiliko ya kimfumo kuliko mabadiliko ya watu.

Watu wanaweza kufariki baada ya miaka michache, mifumo inaweza kudumu miaka mingi zaidi, hata watu wakifariki.

Tatizo la Watanzania wengi kama wewe wanapenda sana kuangalia watu, badala ya kuangalia mifumo.

Huyo Magufuli unayemsifia, bila ya kuzama sana kwenye mazuri na mabaya yake, alishindwa kuweka mabadiliko ya kimfumo sehemu nyingi, aliongoza kwa kutegemea uwepo wake yeye mwenyewe.

Sasa amefariki, hawezi kuongiza tena.

Sasa wewe unamtafuta Magufuki mpya.

Hayo ni makosa unayotaka kuyarudia.
 
Mh Magu ameonekana ni Bora sana ukilinganisha na wana-CCM wenzake Chama kimoja ila mm nafikir tungekubali tukawa demokrasia vumilivu ikawa ni halali wapinzani wenye mawaza tofauti wakatawala inamaana makosa mengi yangekuwa yanarekebishwa sheria kali zingekuwa zinatungwa ili kulinda raslimali za nchi bila kubebana, leo ni ngumu ata akiingia Kasimu bado yuko mlemle kwenye tenga ile ile.. Chama mbadala ni muhim sana kuwa na taasisi imara na sheria imara za nchi sio mtu imara
 
Jpm alifanye sehemu yake ,ila Mama ameifungua nchi miradi ya maendeleo kila kona ya nchi kwaujumla Rais samia suluhu anatosha hadi 2030 kwamjibu wa katiba
 
Hachana na huyu mpuuzi. Inaonekana ni machinga ambae kipindi cha JPM aliruhusiwa kutembeza bidhaa zake sehemu yoyote kwa kitambulisho cha elfu 20. Ni mtu anaeamini kila mwenye pesa ni mwizi na haki ya kunyang'anywa.
 
Mkuu mawazo yako kama nayaona kwenye hiki kitabu kinachopigwa vita vya Wasomi Wajinga. Humu ndani kama mwandishi anatoa siri nyingi sana za CCM. Nafikiri ndiyo sababu hiki kitabu wamekipiga marufuku na mwandishi wake Dkt. Dyaboli hajulikani aliko mpaka sasa
 

Attachments

  • Wasomi Wajinga - Dkt. Dyaboli.png
    355.9 KB · Views: 3
Hachana na huyu mpuuzi. Inaonekana ni machinga ambae kipindi cha JPM aliruhusiwa kutembeza bidhaa zake sehemu yoyote kwa kitambulisho cha elfu 20. Ni mtu anaeamini kila mwenye pesa ni mwizi na haki ya kunyang'anywa.
Jielimishe kwanza ndio uanze kuchangia

Hachana= achana
 
Unazo siku kidogo sana kijana kwa hasira hizo za kijinga!
Hiyo takataka inaoza Chato, kama unaipenda nenda kazikwe naye. Usitujazie nzi hapa!!

Jitu limekataliwa na Mungu kuwa Rais bado mnaliota
 
CCM bwana ni wapumbavu sana yaani kwa sasa bunge ni lao watupu,Rais ni wao,mahakama ni yao,sasa mwakani wakati wa kampeni sijua watawaambia nn wananchi na Sijui watasema nani kawakwamisha.
 
Yaani zirudi zama zile za watu kupotezwa na wasiojulikana? Zama za ajira kugawiwa kwa ukabila? Zama za viongozi kukiuka haki za watumushi? Zama za wafanyabiashara kubambikwa Kodi? Daah ! tupumzishwe Kwanza kwa kweli
 
Yaani nchi itawaliwe na nduli tena??? Nooo, JPM alikuwa mtu wa hovyo kbs
 
Spoken like a pure mwalimu wa darasa la 7A shule ya msingi Tanganyika.
Kabisa mkuu. Huyu atakuwa mwalimu wa shule ya msingi. Hajajua bado mchezo wa siasa unavyochezwa. Pengine akisoma hiki kitabu hapa kinaweza kumsaidia kuelewa walau kidogo
 

Attachments

  • Wasomi Wajinga - Dkt. Dyaboli.png
    355.9 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…