John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Nimepitia maoni ya watu lakini nimegundua kwamba watu wengi hawajui bayana nini au nani hasa mchawi wa kuwepo kwa hali hii mbaya iliyopo hapa nchini?Hata kama staandika matarajio yenu, kifupi ni kwamba, Tanzania inahitaji tena na kwa haraka mno mtu mwenye mfanano na hayati JPM,
Watanzania acheni kuendekeza ujinga, uzembe na ulalamishi
Wengi wenu ni walalamishi na msiopenda kabisa kufanya kazi, (wavivu wa kupindukia) mnapenda starehe bila kujali mnachoingiza
Familia zote masikini chanzo ni baba legelege, baba asiyeweka mfumo na mwongozo thabiti juu ya watoto wake, ni kuandaa mababa wengine walioferi maisha tokea kwa makuzi yao
Nikikumbuka kipindi cha huyo mwamba, kila mtu alipenda kufanya kazi, maofisini nako vile vile kwa sababu baba alikuwa ni mchapa kazi, mkemea uzembe, mkemea wezi na kila maovu, JPM aliwakemea mpaka viongozi wastasfu kwa sababu alijua nini anafanya juu ya nchi hii yenye watu masikini na sio tu masini, bali pia ni nchi yenye wajinga wenge!
JPM alikuwa ni mwalimu mzuri wa mapato na matumizi pia, kila kilichokuwa kikipatikana, kilielekezwa sehemu hisika tu na kufuatiliwa kwa ukaribu
Na ndiyo maana karibu kila mradi ulikuwa ukienda vema kwa sababu shilingi ilikuwa haipotei ovyovyo,
Nikiangalia sasa tulipo na tunavyokwenda, tumekopa matrilioni ya shilingi, na bado miradi ya kimkakati inasuasua, nani aseme tupo kwenye njia sahihi? Hivi ni nani mpaka muda huu kawajibishwa kwenye ripot ya CAG iliyovunja records ya upotevu wa mabilion ya shilingi, nani kajihudhuru walau tuweke imani kwa wanaotuongoza? Nani kafikishwa mahakamani ili tuseme tunatendea haki wananchi??
Mgogoro wa Wizara ya Nishati na wananchi, ni kama kumekosekana mtu wa kuutibu huu mgogoro, visingizio viingi na havijawahi kuisha, kwa nini tuwe na mgao wa umeme?? Tunakosa nini yaani, mwenye jibu wa swali hili nitamlipia ya bando la mwezi mzima, kwa nini kuwe na mgao wa umeme Tanzania kama siyo ulegelege na uzembe tu uliokubuhu??
Kama tunataka kuwa nchi inayopiga hatua kiuchumi na kuwa nchi inayoheshimika nje ndani, basi tunamhitaji mfano wa mtu aliyepita, yaani JPM asiyeogopa kufa kwa ajili ya maisha ya wengi ili akabiliane na wezi, mafisadi, wazembe na makuwadi wa kisiasa, wazembe na machawa yaliyokosa kazi za kufanya, yanaabudu watu ili yalipwe!
Wale kufokafoka karibuni mfoke, na sababu ni moja tu, maslahi yenu yaliyojengwa kwenye wizi na ujanjaunja, ndiyo huwa hamtakaki viongozi kama hao!
Tz tunahitaji taasisi imara na madhubuti kabisa ya kuweza kutuvusha hapa tulipo na kusonga mbele. Mahali pa kuanzia mabadiliko ni kupatikana kwa Katiba Mpya itakayotokana na Maoni, Mawazo na Fikra za Raia wote wa nchi hii.