Ughonile..
Huu mtandao pamoja na kuwa naupenda ila kuna baadhi ya members wanaboa sana, unaweza kuingia humu kwa bashasha ila ukatoka na huzuni sababu ya members wachache vichwa panzi siku yako ikaharibika.
Kuna hawa chawa wa Bi Tozo wakiongozwa na
Lucas Mwashambwa &
Tlaatlaah , itoshe kusema nyie vima mnanikera sana na mada zenu za kichoko.
binafsi nakupenda mno gentleman, pamoja na wadau wengine wote muhimu sana wa humu JF, kwenye majukwaa mbalimbali hususani hili ambalo umetumia kutoa hoja na dukuduku lako la moyoni dhidi yangu na wengine ulowatag..
umechukua uamuzi muhimu sana wa kujitibu kijiba cha Roho, kongole sana aise, I hope utapata relief ya kipekee sana leo.....
ile ya muhimu zaidi ni kuheshimu haki na uhuru wa mawazo, maoni na mtazamo wa wengine. Na njia pekee kumudu mambo haya ni kuvumiliana, kustahimiliana na kua na subra ..
ni vizur kua na uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya dhana ya kukukubaliana kutokukubaliana...
hata hivyo ile jamii yako ya mihemko, ghadhabu na saa zingine waparomosha matusi hawajakuelekeza namna ya kuignore wanaokukwaza, ili usibabaike nao zaidi?🐒
hata hivyo ukifanya hivyo utajinyima na kujikosesha elimu, uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala mbalimbali, Lakini pia sio mbaya na sio lazima ufahamu kila kitu humu JF...
by the way,
amani, utulivu na utangamano miongoni mwa waTanzania, bila kujali dini, rangi, ukabila wala mirengo ya kisiasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu shupavu, Dr Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha tunaipenda nchi yetu na tunaishi kwa upendo, umoja na mshikamano...
Tutaendelea kusema ukweli daima upende, usipende 🐒
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake 🐒