Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

Nilimaliza mwaka ambao mpiga picha wa rais mwinyi mkubwa alifariki baada ya kukatwa koromeo na panga la helicopter alipowahi kushuka kutoka kwenye helicopter ili ampige picha mheshimiwa.
 
R.Kelly alipotoa wimbo wa The storm is over, The storm ilikuwa ni kumaliza form four salama
 
Mimi naenda direct , ule mwaka NELSON MANDELA ALIPOFARIKI HUO HUO NDO CSEE IKAISHIA HIVOOOOOOOO
 
Nilimaliza mwaka ambao mpiga picha wa rais mwinyi mkubwa alifariki baada ya kukatwa koromeo na panga la helicopter alipowahi kushuka kutoka kwenye helicopter ili ampige picha mheshimiwa.
Sijawahi sikia hii. Nitaulizia kwa wakubwa
 
Nilimaliza wakati Mzee wa Uwazi na Ukweli (Mr. Clean -RIP)... Alipokuwa anaamaliza muhula wake wa mwisho Magogoni...
 
We mpumbavu kiongozi wao.
Kivipi usitaje mwaka uliomaliza alafu utaje ulimaliza mwaka gani?
Hivi wewe,nenda mkale matogo huko porini, na hatujui nani alikuleta JF.
 
Mwaka ambao kwa mara ya kwanza babu yangu alienda daslamu
 
Nimemaliza kidato cha nne kipindi waasi wa Banyamulenge wanasitisha mapigano huko Kivu DRC
 
Mwaka ambao Mwalimu Nyerere alikuwa anasubiri kijana aliyemkuza katika uongozi aje achukue fomu ya kugombea urais wa URT bahati mbaya kijana Huyo alisita na hakutaka kuachia nafasi yake huko OAU
 
mimi nilimaliza ule mwaka ambao darasa la 7 na la 8 walifanya mtihani pamoja...
 
Back
Top Bottom