Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

Mwanzoni mwa ungwe ya pili ya yule mwenyekiti mwenye kibwagizo cha "Weka manenoo"
 
Mwaka ambao virusi vya uviko-19 viligunduliwa huko china
 
Mwaka ambao mwalimu Nyerere alihudhuria sherehe ya wafanya kazi Mbeya na kutangaza nyufa kadhaa katika nchi yetu na baadaye mwaka huo kulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi kwa mara ya kwanza nchini.
 
Mimi nilimaliza mwaka ambao mitihani ilifutwa tukarudia tena. Wakongwe najua watakuwa wameng'amua...

Kwa upande wako, ulimaliza mwaka gani bila kututajia mwaka?
1998 mtihani ukarudiwa 1999
Salimia wakubwa zako dogo....
 
Mimi nilimaliza mwaka ambao Deogratius Rweyunga alifukuzwa kazi IPP Media kwa kutapikia makaratasi ya taarifa ya habari kwa kuwa alikuwa amelewa
 
Nilimaliza form 4 wakati ambapo mwaka uliofuata nilitangazwa kua Tanzania One(TO)

Waziri wa wizara husika akanitangaza kua, na alietuongozea kitaifa anatoka shule ya sekondari Mbwindeng'e nae ni Vishu Mtata .
 
Back
Top Bottom