Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

Bila kututajia mwaka, tuambie ulimaliza form four mwaka gani?

nilimaliza form four pindi NCCR-MAEUZI kilikuwa chama kikuu cha upinzani kabla hata ya uchaguzi na Mrema alikuwa akipiga kampeni huku akitembea na Gazeti lililokuwa na ile habari aliyokataa Rushwa nono ya kitu kama Milioni 9 pindi akiwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Mwaka mmoja kabla Jakaya hajaingia awamu ya pili ya uongozi wake.

Chuo nikamaliza katika awamu ya kwanza ya Magufuli..

la saba nikamaliza kwenye awamu ya kwanza ya Kikwete.
 
Mimi nilimaliza mwaka ambao mitihani ilifutwa tukarudia tena. Wakongwe najua watakuwa wameng'amua...

Kwa upande wako, ulimaliza mwaka gani bila kututajia mwaka?
Mimi sijui nitamaliza F4 lini mana kila mwaka nasoma!
Kwako Jese Jonh...
 
Mwaka ambao matokeo ya mtihan yalitolewa mara mbili ya kwanza yakafutwa na yakatolewa tena
Nakumbuka mwaka huo kunamshkaj wangu alikuwa na four ya 30 mara ya pili akapata 3 ya 23
ule mwaka 😥
wengi walipoteza dira ya elimu
 
Mwaka wa CCM kuzaliwa au Jumuiya ya Africa Mashariki ilivunjika.
 
Nilimaliza mwaka ambae Ndalichako alimvimbia JK...[emoji28][emoji28][emoji28]Mama kauzu yule sijapataa onaaa ndo mwaka ambao taifa lilijua kuna Divsion 0.
 
Back
Top Bottom