kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kampuni ya ortello walipewa eneo la uwindaji loliondo mara ilipoingia awamu ya pili ya mzee ruksa.
Baada ya kupewa eneo hilo kampuni hiyo ya UAE yenye wamiliki toka familia ya kifalme tabia yao ikawa kama wamepata koloni.
Pamoja na kwamba wameweza kuepa kutajwa na vyombo vya habari kama zamani kuhusiana na migogoro yao na wenyeji lakini inawezekana ni namna yao kudhibiti mambo tu. Ukweli ni kwamba tangu wamekua hapo hakuna amani kwa wenyeji kuhusiana na maisha yao kama ilivyokua jadi. Kulikua na wakati ukiingia eneo la ortello la uwindaji ilikua kama unaingia katika nchi ya kigeni.
Kwa maoni binafsi naona kama hao waarabu wa UAE wanachukulia loliondo kama mali yao na wana tamaa kuongeza ukubwa kwa hivyo wanachochea chokochoko za kuhamisha wakazi wa jadi.
Kama kuna mtu au seriksli yenyewe ikiweza hebu watupe mapato yanayopatika kwa kitalu cha ortello kwa kila mwaka ili wananchi wapime kama kuna manufaa au kuna vigogo au kigogo anunufaika pekee.
Pia yafaa tujue kama ortello hua anashindanishwa kwa kila muda kwenye kitalu chake.
Itawezekanaje miongo zaidi ya 3 bado wanahodhi kitalu na mipango ya serikali ni kuwahifadhi wao tu?
Tunataka kujua mipango kuwahamisha wenyeji ni kwa ajili ya kuboresha mazingira kwa ustawi wa wanyama tu au ni kuongeza maeneo ya vitalu vya wawekezaji?
Je, ni haki kumuhamisha mtanzania toka eneo lake la asili ili kulitoa kwa biashara ya mgeni huku mapato kwa serikali au mkataba wa huyo mgeni kumiliki eneo hilo sio wazi?