Bila Rakitic,Iniesta,Bosquet Hakuna Messi

Nakubiliana na Wewe ila Rakitic mwenyewe alikiri kucheza na wachezaji type iyo lazima uwe na extrapower
Xavi alikuwa mkabaji? Iniesta Mkabaji? Barca mkabaji ni Sergio na mabeki. Na hii ni kutokana na tiki taka.
 
Wewe dogo upo mtupu kabisa ktk suala la soka, hivi ushawahi kucheza mpira? Kama umewahi bila shaka umeishia cha ndimu tu na sio vinginevyo.

Ngoja nikupe fact uonde ujinga akili mwako. Mimi nimecheza mpira ila kutokana na sababu za hapa na pale ikabidi niache.

Umesema Sergio ndio mtibuaji mipango kwa Barca, na ukasema pia Pogba kutopewa jukumu la kukaba kumemfanya afanyw vyema.

Mdogo wangu, katika timu kuna watu WATATU (3).

1. Mkabaji
2. Mchezeshaji na
3. Mfungaji

Timu yoyote inapoingia uwanjani lazima hawa watu wawepo, kama una wakabaji wawili lazima mmoja ndo atakuwa master, na kwa mchezeshaji hivyo hivyo na kwa mfungaji hivyo hivyo.

Mfano, kwa kuwa umeitaja Barca na mimi nitatolea mfano Barca hiyohiyo. Kabla ya Rakitic kulikuwa na Xavi, Iniesta na Sergio. Suala la ukabaji wa Timu kwa ujumla ni la Sergio, Iniesta ni kiungo mchezeshaji na mshambuliaji ila suala la kuchezesha timu lilikuwa chini ya Xavi na ufungaji lilikuwa ni la Messi.

Sasa ww unashangaa nini Sergio kuwa ndo mtibuaji wakati ktk timu hilo ndo jukumu lake!? Ni sawasawa na kushangaa kipa kudaka wakati ndo jukumu lake uwanjani, kuzuia mpira usiingie golini.
 
Wakati nacheza mpira kabla ya Match, huwa kuna kitu wachezaji tunakiita Mgongo wa timu, na baada ya timu tunaangalia wabeba timu.

Mgongo wa timu unajumuisha WATU WATANO (5) na Wachezaji ni watu WATATU (3). Mtu wa kukaba anaingia sehemu zote mbili hapo juu, na unapopewa jukumu la kukaba yaani timu nzima wewe ndo unaongoza suala la ukabaji, beki namba 5 yupo chini ya Kiungo Mkabaji. Beki namba 5 anakuja kuchukua maamuzi pale tu timu yake inaposhambuliwa na namba 6 haina msaada tena, yaani upinzani kuwafikia ila Back Line, hapo namba 5 ndo anapanga ile Back Line nini cha kufanya lakini bado pia anamtegemea 6 aje msaidie.

Sasa huyu dogo anataka amuone Sergio ndo mbeba timu wakati Sergio ndo jukumu lake. Kwani wakati Messi hayupo Sergio hakabi? Na kama anakaba, Je Barca inafungaga magoli sawasawa na Messi akiwepo?
 
Dogo umewahi kujiuliza kwanini tangu Ronaldo atue Madrid hamna Striker wa maana aliyetua Santiago Bernabeu kucheza na huyo Ronaldo!?

Unadhani kwanini Ronaldo yeye ndo anafunga sana pale kuliko Benzema, yaani hamna balance ktk tofauti ya magoli kati ya Benzema na Ronaldo!?

Jiulize kwanini Mastriker wazuri duniani hawajaenda Bernabeu kucheza na Ronaldo ambae yeye ni left wing. Nakutajia majina ya Strikers waliokataa kutua Bernabeu then ujiulizw WHY!?

1. Kun Aguero.
2. Wayne Rooney.
3. Louis Suarez.
4. Zlatan Ibrahimovic.
5. Roberto Lewandowski
6.

Hawa wote wamekataa kutua Bernabeu, ulisema ww umecheza mpira na unaujua, aya embu tueleze Wana_JF kwanini hawa watu wamekataa pesa ndefu za Madrid ili kutua Bernabeu!!???
 
Well both of you... Mpo wrong. Wewe na huyo Rakitic wako.
Na jibu ni lile lile refer kwenye philosophy ya Barca.
Rakitic yupo sahihi kabisa ila huyu mtoto ana kichwa kizito kuelewa, ukijumrisha na chuki zake kwa Messi ndo kabisaaaa.
 
Hivi we mtoto una miaka mingapi?
 
Haka katoto kanaongea shombo tu humu ndani. JF ameona kama ni group la watoto wenzie huko Watsup.
 
Haka katoto kanaongea shombo tu humu ndani. JF ameona kama ni group la watoto wenzie huko Watsup.
Kwan umeambiwa uchangie...

Shikamoo baba..

Maneno ya Rakitic sasa kosa lipo wapi?
 
sasa ww jamaa point yako ni nini unataka modric azungumzwe ili iweje,ww ukiona ronaldo ndio anyezungumzwa kuzidi huyo modric jua fika majukumu ya ronaldo ni makubwa kuzidi ya huyo modric ndio maana hazunhumzwi! au ww unadhani kufunga ni kazi rahisi,mbona ma goal keeper wanaokoa mipira sana lakini bado sifa zote hupewa ma forward na hii ni duniani kote!au unadhani watu dunia nzima kuwapa sifa ma forward na kuwaacha wechezaji wengine kama ma goal keeper,mabeti na viungo ni wajinga!.sijui kama umisha wahi kucheza mpira ww unadhani kazi ya kufunga ni kazi rahisi eeh.
 
Wakujifunza mimi au Rakitic??ok labda ungetaka Rakitic asemaje?
ww ndio wa kujifunza maana ww ndio uliyesema hii statement kwenye uzi wako

Naimani hata Messi akisifiwa anaweza kukataa na badala yake akaelekeza sifa kwa wachezaji wenzake.

Hivyo tunavyompa sifa Messi tukumbuke hao wachezaji..
 
hizo ni hisia zako vipi nami nikukuambia kuwa kama messi angeaza hiyo game basi uwepo wa messi pale mbele ni hofu tosha na labda celta vigo wangecheza mpira wa kuzuia zidi na inawezekana uwepo wa messi ungesababisha wafungwe magoli kama 3 mapema na kuwaondoa matumaini kabisa ya kushinda game
 
Funga mdomo wako sasa!
Freedom of speech itakua haizangatiwi

Kila mtu anahaki ya kuongea otherwise havunji sheria za nchi/jamii forum

Pia hakuna aliyekuforce ukoment

Kama ni irrelevant kwako unaeza kuacha tu.

Umesoma alichosema Rakitic au unaishia kukoment tu kisa mwingnwe kakoment
 
Who is wrong mimi au Rakitic??
 
hakuna game waliyofungwa wakiwepo wote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…