funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Katika zama hizi ambazo maendeleo ya nchi yamekuwa makubwa upo umuhimu wa kuwa na Serikali au Dola lenye maguvu na makucha zaidi ...la sivyo kila aliyefanikishwa kuwa tajiri atatutawala sana kutokana na uwezo wake kifedha.
Ukiwa na matajiri wenye uwezo wa kununua vyombo vya habari kutaka kupinga na kufifisha maelekezo ya Serikali basi ujue kuna hatari kubwa ya kiusalama.
Hivi wananchi wasio na uwezo wa kuzinunua media nani atawatetea??,
Ni muhimu na ni lazima kuwepo nguvu ya Serikali au dola katika kudhibiti ubwanyenye ili masikini wasiletewe tabu.
Haiwezekani eti Mkuu wa Mkoa anatoa agizo halafu kuna news media au platforms zinanunuliwa kutaka kufifisha agizo lake...huo utakuwa ni utawala wa manyani....yaani kila dume linajipiga kifua.
Leo hii tukikubali upuuzi wa namna hii inamaana kuna siku tutakuwa na utawala wa kichifu ambao ulifutwa rasmi.
Hatuwezi kuwa na Taifa moja iwapo msingi wa kuamua mambo utajikita kwenye uwezo wa rasilimali...yaani kwa mfano wa moja kwa moja nikiwa na basi natengeneza stand, hoteli ,stoo ya mizigo ,n.k na hakuna anayenieleza kitu.
Sikatai uwekezaji au kujikuza kiuchumi lakini nakataa kujijengea himaya zinazoidhoofisha serikali kwa kuwa serikali ipo kwa ajili ya walionacho ,wezi na wasionacho pamoja na wanyonge au wasiojiweza.