GE2025 Bila shaka Balozi Polepole anatafuta shari na huenda amejiandaa kwa shari

GE2025 Bila shaka Balozi Polepole anatafuta shari na huenda amejiandaa kwa shari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa TZ hakunaga system kubwa inayoweza kupambana na Rais aliyeko madarakani. Mbaya zaidi Polepole anashambulia hadi Rais mstaafu mwenye connection dunia nzima. Ni suala la muda tu Polepole atatoa mlio akivuka mstari.
Kuhusu kuwa na connection dunia nzima... hili halina logic. Nakubaliana na wewe kuwa kwa Tanzania rais aliyepo madarakani ana nguvu kubwa na kupambana ni nearly impossible hasa kwa nchi yenye wananchi kama yetu... Lakini siyo kanuni ambayo haiwezi kuvunjwa.
 
Mie nimeskiliza mara 2 ili nielewe! Alisema jana rasimu ya Warioba waliiweka kando baada ya kuona itawadispline wakubwa wakienda arijojo...Mambo vipi lakini?
Rasimu ya Warioba ni kundi la Lowassa liliitupilia mbali kwa sababu Lowassa alitegemea kuwa atateuliwa hivyo akaona kuwa madaraka yake yangeminywa. Nadhani hata kundi la Membe (nyuma Kikwete) lilikuwa na hofu hii hii.
 
Kimsingi kwa maoni yangu naona anayelengwa hapa ni kikwete! Kwa namna nyingine naona polepole ana watu nyuma yake yawezekana ni system kubwa kabisa ndani ya serikali inayojua kinachoendelea nimeamua kumtumia polepole na hapa nahisi! Kuna uwezekano mama kalazimishwa kugombea kwa maslahi ya kundi fulani! Na anaogopa kusema kuwa hagombei tena kwa sababu ya genge liĺilomzunsguka ( ndo maana polepole anajiamini) siyo bure!
Kweli
 
Huyu polepole ana mpango mtu apate kiharusi?

Ukiwa na adui alafu ukawa unalala hujui kesho adui yako ataamka na lipi,unakuwa na stress Kali vibaya mno. Sasa stress Zikizidi linageuka kuwa tatizo la afya.

Polepole kama hajamaliza afanye amalize tu yote yamtoke kisha tufanye mambo mengine..!
Kwani nani ya Serikali na CCM ana hofu na anachoongea Polepole?
 
Wenye Nchi , Huu mwaka Samia na genge lake, Hawatoboi Kwa namna yoyote Ile, waruke, wakae, wafanye wanavyoweza, Hawatoboi.

Imeamuliwa hivo.

Zingatia haya Maneno hapa chini

Ni Maneno ya Mzalendo Mkweli, mwenye Uthubutu, The Intelligent Mh Polepole , namnukuu 'Samia nakuomba, rekebisha hili jambo before it's too late, Mimi sipendi tufike pahala ambapo itatupeleka kwenye level ambazo zitakiumiza Chama Cha mapinduzi , wakati nafasi ya kutengeneza Iko"
Hiyo nukuu yako toka kwa H. H. Polepole ndiyo ilipaswa iwe ni msingi wa hoja ya Mr Benson Mramba...

Na Mr Benson Mramba, Polepole na Tundu Lissu na CHADEMA wala hawatafuti shari bali wanaitakia mema nchi na taifa hili...

Watu wanaotaka shari ni wavunja utartibu, sheria na katiba za chama chao na sheria mama ya nchi, Katiba...

Haiwezekani watu wanaotetea kufuatwa kwa taratibu, sheria na katiba za chama na ya nchi ili ku - harmonize situation wawe ni wataka shari...

Fikra za mtu wa namna hii daima hutoka kwa watu wenye fikra mbaya wasioweza kutumia vyema akili zao kuchakata mambo...
 
Ni wa kukaonea huruma katoto haka.Halafu hakajaoa mpaka leo.Nadhani ana matatizo mengi.Tumuombee tu.
We unafikiri kuoa ni utimamu?
Kuna njia Polepole anatengeneza ya 2030, au mko tayari kuona mchengerwa au Ridhiwani wanakua Rais
 
Kimsingi kwa maoni yangu naona anayelengwa hapa ni kikwete! Kwa namna nyingine naona polepole ana watu nyuma yake yawezekana ni system kubwa kabisa ndani ya serikali inayojua kinachoendelea nimeamua kumtumia polepole na hapa nahisi! Kuna uwezekano mama kalazimishwa kugombea kwa maslahi ya kundi fulani! Na anaogopa kusema kuwa hagombei tena kwa sababu ya genge liĺilomzunsguka ( ndo maana polepole anajiamini) siyo bure!
Very true { Kuna kitu Kiko nyuma ya Polepole Tena kikubwa}
 
Kuhusu kuwa na connection dunia nzima... hili halina logic. Nakubaliana na wewe kuwa kwa Tanzania rais aliyepo madarakani ana nguvu kubwa na kupambana ni nearly impossible hasa kwa nchi yenye wananchi kama yetu... Lakini siyo kanuni ambayo haiwezi kuvunjwa.
Nyie ndo mnamponza Polepole.
 
Kwa TZ hakunaga system kubwa inayoweza kupambana na Rais aliyeko madarakani. Mbaya zaidi Polepole anashambulia hadi Rais mstaafu mwenye connection dunia nzima. Ni suala la muda tu Polepole atatoa mlio akivuka mstari.
Connection ?!
Nguvu ya Mamba kumayi akiwa nje ya maji hamna kitu chochote !
 
Rasimu ya Warioba ni kundi la Lowassa liliitupilia mbali kwa sababu Lowassa alitegemea kuwa atateuliwa hivyo akaona kuwa madaraka yake yangeminywa. Nadhani hata kundi la Membe (nyuma Kikwete) lilikuwa na hofu hii hii.
Walaaniwe waliosababisha Rasimu ya Warioba itupwe !
 
kwa ufupi tangu jiwe aondoke,tukumbuke kuna kundi lilitamani kufanya uasi wa kisiasi na kutaka kumfanya Samia asichukue kijiti,kundi hilo ni la haohao akina polepole,bahati nzuri wamefeli mpango wao,

kwahiyo kuna umuhimu mkubwa wa samia kusimamiwa/kulindwa kwa kila hatua,kama polepole na genge lake linalomtuma kupambana na samia naamini hawatofanikiwa watafeli vibaya sana.
 
Huyu polepole ana mpango mtu apate kiharusi?

Ukiwa na adui alafu ukawa unalala hujui kesho adui yako ataamka na lipi,unakuwa na stress Kali vibaya mno. Sasa stress Zikizidi linageuka kuwa tatizo la afya.

Polepole kama hajamaliza afanye amalize tu yote yamtoke kisha tufanye mambo mengine..!
polepole hana lolote makelele hajaanza leo.Kawai kukimbia kabla ajafyekelewa mbali.Anayoongea hayana tija yoyote kwa taifa kwa sasa.Kwasababu yeye anachopigania ni kitu kile kile ktk mfumo ule ule.sasa unadhani nani atamsikiliza yeye kama annabavu Aingie msituni ila izo mbembe mbe wala hazimzuii tembo kunywa maji.Watu wenyewe anao watisha ni wakina nani ,Nchi za ulaya tu zinyewe zimeshendwa sembuse yeye.
 
Naomba nimnukuu kwenye maneno yake ya leo tarehe 03 August 2025

"...........WanaCCM wenzangu naomba tumuweke Mungu mbele, 2010 ni akina nani walitembeza fomu za mgombea Urais kama haikua familia ya Mgombea? Au hiki ni kitu nakosea kusema? Nazungumza kama mwanataaluma leo......

Natumia uhuru wangu wa kuzungumza....tuna mjadala hapa kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mkuu unaokuja na kama watu watashupaza shingo kwasababu tu wanataka lao jambo, basi tujue hawa wameamua na sisi tuamue vinginevyo.....

My take. Kama wameamua akimaanisha wanamtandao kwa maneno yake.

Je hii na sisi tuamue vinginevyo anawazungumzia akina nani?

It's him against the state au?
Atapigwa kama mbwa koko
 
kwa ufupi tangu jiwe aondoke,tukumbuke kuna kundi lilitamani kufanya uasi wa kisiasi na kutaka kumfanya Samia asichukue kijiti,kundi hilo ni la haohao akina polepole,bahati nzuri wamefeli mpango wao,

kwahiyo kuna umuhimu mkubwa wa samia kusimamiwa/kulindwa kwa kila hatua,kama polepole na genge lake linalomtuma kupambana na samia naamini hawatofanikiwa watafeli vibaya sana.
Nyie mnampa tu kichwa polepole hana genge lolote,yeye anapigania ulaji wake tu kwani anajua awa.mu inayofuata hana chake.
 
Back
Top Bottom