GE2025 Bila shaka Balozi Polepole anatafuta shari na huenda amejiandaa kwa shari

GE2025 Bila shaka Balozi Polepole anatafuta shari na huenda amejiandaa kwa shari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Naomba nimnukuu kwenye maneno yake ya leo tarehe 03 August 2025

"...........WanaCCM wenzangu naomba tumuweke Mungu mbele, 2010 ni akina nani walitembeza fomu za mgombea Urais kama haikua familia ya Mgombea? Au hiki ni kitu nakosea kusema? Nazungumza kama mwanataaluma leo......

Natumia uhuru wangu wa kuzungumza....tuna mjadala hapa kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mkuu unaokuja na kama watu watashupaza shingo kwasababu tu wanataka lao jambo, basi tujue hawa wameamua na sisi tuamue vinginevyo.....

My take. Kama wameamua akimaanisha wanamtandao kwa maneno yake.

Je hii na sisi tuamue vinginevyo anawazungumzia akina nani?

It's him against the state au?
Hizi ni vita za makundi ya CCM Sukuma Gang na Kizimkazi. Wote ni wale wale tu wanazuga watu.

Usidanganyike kufikiri kwamba kuna mtu anatetea uongozi mzuri wa nchi hapo.

Kwa kifupi CDF Mabeyo alisema kuwa Rais Magufuli alipofariki, kuna watu walitaka kupindisha katiba ili Samia asiwe rais. Wakashindwa.

Sasa Polepole alikuwa mmoja wa hao watu. Na sasa hivi anaendelea na jitihada zake za kumnyima Samia haki yake ya kikatiba ya kuendelea kuwa rais.

Please note well, simtetei Samia. Tuna tatizo la false dichotomy fallacy kuona kila mtu anayemsema Polepole anamtetea Samia. Naweza kuwasema wote wawili.

Samia kaharibu nchi, Samia na Kikwete wameharibu mchakato wa kupata mgombea wa CCM na kama wanasemwa kwa kuharibu uongozi na kuharibu mchakato wa kupata mgombea wa CCM tu, hayo yote ni sawa.

Lakini, kidemokrasia Samia ana haki ya kugombea urais. Polepole analazimisha Samia asigombee urais kwa desturi na tamaduni za kuungaunga ambazo hazijaandikwa popote.

Tamaduni na desturi hata kama zipo na ni nzuri kuzifuata, huwa zinafuatwa pale mambo yanapokuwa hayajaandikwa kisheria na kikatiba.

Jinsi ya kupata mgombea urais imeandikwa kisheria na kikatiba, chamani na kitaifa.

Kwenye hili, kwa nini Polepole anataka tufuate desturi na utamaduni mambo ambayo hata hayajaandikwa wakati mambo haya yameandikwa kisheria kikatiba, chamani na kitaifa?

Polepole alichotakiwa kufanya kama hampendi Samia na uongozi wake ni kujikita katika hoja kwamba Samia kaharibu mchakato wa uteuzi wa mgombea wa CCM. Mchakato urudiwe, Samia aruhusiwe kushiriki tena kugombea uteuzi na wanachama wengine wa CCM. Kama Polepole anataka kuwa rais aseme. Kama anamtaka mtu mwingine wa CCM awe rais amtaje na kumfanyia kampeni.

Polepole anavyojikita katika hoja za kutaka kumzuia Samia asiwe Rais kwa sababu za utamaduni na desturi, sababu ambazo hazijaandikwa popote, anatuonesha tu hamtaki Samia lakini anaogopa kushindana naye, anataka ushindi wa mezani.

Kimsingi anakuwa hana tofauti na Samia anayelazimisha uteuzi ambao haujafuata demokrasia.
 
Naomba nimnukuu kwenye maneno yake ya leo tarehe 03 August 2025

"...........WanaCCM wenzangu naomba tumuweke Mungu mbele, 2010 ni akina nani walitembeza fomu za mgombea Urais kama haikua familia ya Mgombea? Au hiki ni kitu nakosea kusema? Nazungumza kama mwanataaluma leo......

Natumia uhuru wangu wa kuzungumza....tuna mjadala hapa kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mkuu unaokuja na kama watu watashupaza shingo kwasababu tu wanataka lao jambo, basi tujue hawa wameamua na sisi tuamue vinginevyo.....

My take. Kama wameamua akimaanisha wanamtandao kwa maneno yake.

Je hii na sisi tuamue vinginevyo anawazungumzia akina nani?

It's him against the state au?
Polepole anatafuta tu sababu yule ukimuangalia ni mgonjwa sasa anataka naye asife tu bila kuongelewa
 

Attachments

  • 20250804_083912.jpg
    20250804_083912.jpg
    50.6 KB · Views: 18
Mnamjadili vipi mtu kama huyo polepole aliye tumika kuvuruga chadema kipindi cha jpm?

Chadema wakiitwa nyumbu wanakasurika
Mkuu mara hii umesahau Mbowe kuwa alitusnitch kwa miaka zaidi ya 20?!
 
Leo ndio nimemsikiliza polepole Kwa umakini nimemuelewa sana kumbe jamaa yupo sahihi katika hoja yake

Hi serikali ilishapewa miaka 10 imeisha ilitakiwa ikae pembeni ije serikali mpya

Yani Kwa mfano
Magufuli na Samia walipewa Treni waitoe Dar waipeleke mwanza na mkatana unasema wakiisha ifikisha Treni Mwanza kazi Yao imeishia happ watakao irudisha Treni Dar ni watu wengine sio wao tena

Magufuli ameendesha Treni kuele

kea Mwanza kufika Singida Magufuli amefariki Samia akashika usukani Ili Treni ifike Mwanza kama mkatana unavyotaka

Kwahiyo Baada Treni kufika Mwanza kazi aliyopewa Magufuli na Samia inakuwa imeishia hapo

Sasa kilichopo hapa Treni imeshafika Mwanza inatakiwa wapatikane watu wengine wa kuirudisha Dar

Leo nimemuelewa sana Polepole
 
polepole hana lolote makelele hajaanza leo.Kawai kukimbia kabla ajafyekelewa mbali.Anayoongea hayana tija yoyote kwa taifa kwa sasa.Kwasababu yeye anachopigania ni kitu kile kile ktk mfumo ule ule.sasa unadhani nani atamsikiliza yeye kama annabavu Aingie msituni ila izo mbembe mbe wala hazimzuii tembo kunywa maji.Watu wenyewe anao watisha ni wakina nani ,Nchi za ulaya tu zinyewe zimeshendwa sembuse yeye.
Anachopigania ni kitu kile kile katika mfumo ule ule 😂 !
Na Mwenyekiti wa CCM ndiye huyo huyo ni Mkuu wa Nchi mwenye madaraka makubwa sana aliyopewa na Katiba ya Nchi hii 👍 !

Sasa hapo ni nani wa kumtingisha Mwenyekiti ???!
😂😂😅😅

Polepole inaelekea hajui mambo mengi ya Nchi hii !
Au wamepanga kuhamisha magoli kuhusu No reforms no elections ya Chadema 😁 !
Imesahauliwa kwa muda tangu Polepole aje na drama zake 😂 !
 
Kwa TZ hakunaga system kubwa inayoweza kupambana na Rais aliyeko madarakani. Mbaya zaidi Polepole anashambulia hadi Rais mstaafu mwenye connection dunia nzima. Ni suala la muda tu Polepole atatoa mlio akivuka mstari.
Pigia mstari "dunia mzima" Hadi kumtembeza Janabi kama machinga na pampasi....

Zamani tukiwa wadogo kuna dogo kwenye kundi tulikuwa tunafuatana naye kila alipokuwa sio kwa sababu ya akili, uhodari kucheza mpira, nguvu za kutupigania, NK hapana, alikuwa na hela za kutugawia hovyo!
Kupitia kwa Kikwete ni rahisi kujichotea raslimali za nchi hii na kumpa "suti"
 
K
Leo ndio nimemsikiliza polepole Kwa umakini nimemuelewa sana kumbe jamaa yupo sahihi katika hoja yake

Hi serikali ilishapewa miaka 10 imeisha ilitakiwa ikae pembeni ije serikali mpya

Yani Kwa mfano
Magufuli na Samia walipewa Treni waitoe Dar waipeleke mwanza na mkatana unasema wakiisha ifikisha Treni Mwanza kazi Yao imeishia happ watakao irudisha Treni Dar ni watu wengine sio wao tena

Magufuli ameendesha Treni kuele

kea Mwanza kufika Singida Magufuli amefariki Samia akashika usukani Ili Treni ifike Mwanza kama mkatana unavyotaka

Kwahiyo Baada Treni kufika Mwanza kazi aliyopewa Magufuli na Samia inakuwa imeishia hapo

Sasa kilichopo hapa Treni imeshafika Mwanza inatakiwa wapatikane watu wengine wa kuirudisha Dar

Leo nimemuelewa sana Polepole
itu ambacho hakijui Polepole ni kwamba hakuna awezaye kumtingisha Mwenyekiti wa Chama ambaye ndiye Mkuu wa Nchi !

Akishalijua hilo atanyamaza mara moja !
 
Leo ndio nimemsikiliza polepole Kwa umakini nimemuelewa sana kumbe jamaa yupo sahihi katika hoja yake

Hi serikali ilishapewa miaka 10 imeisha ilitakiwa ikae pembeni ije serikali mpya

Yani Kwa mfano
Magufuli na Samia walipewa Treni waitoe Dar waipeleke mwanza na mkatana unasema wakiisha ifikisha Treni Mwanza kazi Yao imeishia happ watakao irudisha Treni Dar ni watu wengine sio wao tena

Magufuli ameendesha Treni kuele

kea Mwanza kufika Singida Magufuli amefariki Samia akashika usukani Ili Treni ifike Mwanza kama mkatana unavyotaka

Kwahiyo Baada Treni kufika Mwanza kazi aliyopewa Magufuli na Samia inakuwa imeishia hapo

Sasa kilichopo hapa Treni imeshafika Mwanza inatakiwa wapatikane watu wengine wa kuirudisha Dar

Leo nimemuelewa sana Polepole
Mkuu,

Hizi ni vita za makundi ya CCM Sukuma Gand vs Kizimkazi.

Kwa katiba ya nchi Samia anaruhusiwa kugombea urais mwaka 2025 awe rais mpaka 2030. Hii ni katiba ya nchi, zaidi ya desturi au utamaduni wowote.

Habari ya kumlazimisha Samia asigombee urais ni kumvunjia haki yake ya kikatiba.

Hiyo habari ya serikali ikishafikisha miaka 10 haijaandikwa popote ni story za kuungaunga tu. Kwanini mnaruhusu mtu aje na stories za kuungaunga ambazo hazijaandikwa popote kwenye jambo ambalo limeandikwa vizuri kikatiba?

Simtetei Samia. Samia ana mapungufu mengi, kavunja demokrasia, kaharibu uteuzi wa mgombea CCM. Akisemwa kwa haya yote ni sawa. Hata mimi namsema. Kwa hivyo sipo hapa kumtetea Samia. Natetea katiba. Tusifanye mambo kwa utamaduni na desturi kama mambo yameandikwa kwenye katiba.

Hii habari ya Samia kamaliza muda wake ni ujinga tu. No vita za makundi ya CCM kugombea utais tu. Yena wakimuogopa Samia na kutaka ushindi wa mezani bila kushindana na Samia.

Kwa sababu Katiba ya Tanzania ibara ya 42 imetueleza Samia ana haki ya kugombea urais 2025.

Sasa jambo limesemwa wazi kikatiba, kwa nini tunataka kuweka zengwe la kumuondoa Samaia asigombee urais kwa kutumia mambo ambayo hayajaandikwa ya utamaduni na desturi habari anazosema Polepole za kuungaunga?

Tunaweza kutumia desturi na utamaduni pale ambapo mambo hayajaandikwa kikatiba.

Lakoni, hili limeandikwa vizuri kikatiba. Ibara ya 43 imeeleza vizuri rais akifariki Makamu wa Rais anaweza vipi kuwa Rais, anaruhusiwa kugombea miaka gani na haruhusiwi kugombea miaka gani.

Kwa nini Polepole anataka kutumia utamaduni ambao haujaandikwa popote wakati suala limeelezewa vizuri kikatiba na kuandikwa vizuri?
 
Pigia mstari "dunia mzima" Hadi kumtembeza Janabi kama machinga na pampasi....

Zamani tukiwa wadogo kuna dogo kwenye kundi tulikuwa tunafuatana naye kila alipokuwa sio kwa sababu ya akili, uhodari kucheza mpira, nguvu za kutupigania, NK hapana, alikuwa na hela za kutugawia hovyo!
Kupitia kwa Kikwete ni rahisi kujichotea raslimali za nchi hii na kumpa "suti"
Umeandika ujinga
 
Wenye Nchi , Huu mwaka Samia na genge lake, Hawatoboi Kwa namna yoyote Ile, waruke, wakae, wafanye wanavyoweza, Hawatoboi.

Imeamuliwa hivo.

Zingatia haya Maneno hapa chini

Ni Maneno ya Mzalendo Mkweli, mwenye Uthubutu, The Intelligent Mh Polepole , namnukuu 'Samia nakuomba, rekebisha hili jambo before it's too late, Mimi sipendi tufike pahala ambapo itatupeleka kwenye level ambazo zitakiumiza Chama Cha mapinduzi , wakati nafasi ya kutengeneza Iko"
Atafanyaje anachimba wenzake Biti tu hana lolote anapiga kelele na kutapa tapa
 
Naomba nimnukuu kwenye maneno yake ya leo tarehe 03 August 2025

"...........WanaCCM wenzangu naomba tumuweke Mungu mbele, 2010 ni akina nani walitembeza fomu za mgombea Urais kama haikua familia ya Mgombea? Au hiki ni kitu nakosea kusema? Nazungumza kama mwanataaluma leo......

Natumia uhuru wangu wa kuzungumza....tuna mjadala hapa kabla hatujaingia kwenye uchaguzi mkuu unaokuja na kama watu watashupaza shingo kwasababu tu wanataka lao jambo, basi tujue hawa wameamua na sisi tuamue vinginevyo.....

My take. Kama wameamua akimaanisha wanamtandao kwa maneno yake.

Je hii na sisi tuamue vinginevyo anawazungumzia akina nani?

It's him against the state au?
Pole pole hamkubali kabisa JK, hili lipo wazi kutoka kwenye kauli zake. Tabu yake kubwa nadhani ni kumuona Rais Samia akiambatana na asiyempenda.
 
Kudhani kwamba CCM inaweza kuwa na mgombea tofauti na Dr Samia ni ukichaa
 
Back
Top Bottom