Qur'an ilishasema:
Qur'an 27:34. ...Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.
34
Kaa kitako bimkubwa nikusomeshe kwa sababu huna unalojua kuhusu Quran Wala Tafsiri ya Quran!
Majibu yangu kuhusu Aya hii ni katika pointi zifuatazo.
A. Aya hii inaelezea maneno ambayo yamesemwa na mwanamke , malikia wa Sabai ( QUEEN OF SHEBA) maeneo ya Yemen ya sasa Malikia ambaye wakati anasema maneno hayo alikuwa bado ni kafiri anayeabudu jua kabla ya kusilimu na kuolewa na Nabii na mfalme Sulayman.
B . Si wafalme wote wanaosifika na sifa zilizotajwa katika aya hiyo yaani sifa ya
(1) kuharibu nchi na (2) kudhalilisha watu.
Baadhi ya wafalme na watawala wana sifa hizo mbaya na wengine hawana sifa hizo.
Kwa ,mfano Nabii Daudi alikuwa Mfalme na alivyokufa ufalme wake ulirithiwa na mwanae Nabii/mfalme Sulayman. Sasa kwa akili yako unataka kusema kuwa hao manabii wawili pia walikuwa na sifa za kuharibu nchi na kudhalilisha watu?! Ukisema ndiyo utakuwa kafiri hapohapo kwa kuwakosea adabu mitume wa Allaah!
C. Miaka ya kama 1460 iliyopita huko Habasha ( Ethiopia/Eritrea) kulikuwa na mfalme wa kinaswara anayejulikana kama mfalme Najashiy ambaye mtume aliwashauri waislamu waliokuwa wakiteswa na makafiri mjini Makka wahamie katika nchi ya Habasha na kumsifu mfalme wa Habasha kuwa ni Muadilifu na katika nchi yake hakuna anayedhulimiwa.
Je kwa akili yako mfalme huyu pia alikuwa anaharibu nchi na kudhalilisha watu?! Ukisema ndiyo utakuwa huna adabu kwa kumchafua mtu ambaye mtume
صلى الله عليه وسلم
kamsafisha!.
D. Utawala wa kifalme sio haramu, na dini ya kiislamu haijaharamisha tawala za kifalme , kinachoangaliwa ni je mfalme huyu anatawala kulingana na maelekezo ya Quran na Sunna au anatawala kwa mawazo yake na mawazo ya washauri wake?!
Pia rejea Sura ya 3 / Suratu Aali Imran Aya ya 26.
E. Hiyo aya ya 34 ya sura ya 27/ Suurat Annamli uliyoitaja hapo juu, ukitaka kuielewa vizuri anzia aya ya 20 sura hiyohiyo ambapo Allaah kaanza kutaja kisa cha Nabii Sulayman, Ndege Hudihudi na Malikia Balqiisi wa Sabai, kisha endelea hadi aya ya 38 na ukifika aya ya 44 ndio mwisho wa kisa hicho, ama kuleta aya moja tu bila kuangalia mtiririko wa aya zilizotangulia na zilizofuatia Allaah alikuwa anazungumzia habari gani hapo lazima utaleta tafsiri iliyopotoka.
F. Kama nilivyosema kwenye nukta D, kutawala nchi kwa utawala wa kifalme siyo haramu.
Na tawala za asili zilizokuwepo zama za baba yetu Adamu hadi karne ya 18 zilikuwa ni tawala za kichifu na kifalme.
Serikali za kidemokrasia na mifumo ya kupiga kura kuchagua viongozi mifumo hii imeanzishwa na nchi za kimagharibi kwa nia ya kuinginza machafuko katika nchi mbalimbali zinazoendelea kwa ile sera ya devide and rule!, na watu wote wanajua ya kwamba hata neno democracy asili yake ni neno la kigiriki na pia ni wazi kwamba nchi nyingi zinazoendelea zimeipokea demokrasia shingoupande / mguu ndani mguu nje na chaguzi za kidemokrasia zimekuwa chanzo cha machafuko na vurugu ndani ya nchi zinazoendelea ukilinganisha na nchi za kifalme ambazo zinajitegemea kiuchumi na hazina machafuko ya mara kwa mara ukilinganisha na zile nchi zinazoendelea zilizojitangaza kuwa ni nchi za kidemokrasia hali yakuwa viongozi wake bado hawapendi kuondoka madarakani/ wanang'ang'ania kuendelea kubaki madarakani.
Mwisho nafasi ingeruhisu ningekufundisha historia ya tawala za kiislamu hadi kuanguka kwa dola ya Othman (Othman empire الدولة العثمانية) karne ya 20,
lakini muda hautoshi ila atakapo Allaah hili nitalianzishia Uzi maalumu ili watu wapate faida ,
Wabillaahil taifiyq.