Bila "tumbua tumbua" haya Maendeleo tunayoyashuhudia leo yasingekuwepo

Bila "tumbua tumbua" haya Maendeleo tunayoyashuhudia leo yasingekuwepo

Kabla ya awamu ya 5 deni lilikuwa ni Trillion 36 tu...na barabara za lami zilikuwa zimejengwa km 12,000 zimefika nchi nzima, shule za sekondari kila kata, vituo vya afya, vyuo nk... Niambie Magu kwenye miaka 5 ame accomplish nini? Nothing. Hakuna cha Dam, SGR wala nini, pamoja na kukopa matrillion yote
Eti barabara zilifika nchi nzima.Eti vituo vya afya kila kata.Eti shule za sekondari kila kata.Mkuu hivi unaongelea mijini au nchi nzima maana unaongea uongo ulio dhahiri.Eti hakuna Nyerere dam.Eti hakuna SGR.Haufai kuwa last emperor kwa uongo huo.
 
Mpaka anaingia kaburini hajatoa ufafanuzi wa upotevu wa 1.5 trillion, hakuajiri, hakuongeza mishahara wala promotion, kusitisha haki za watu kuishi (ref. Kibiti), pesa za tetemeko, makinikia bado hakuchenjua, hatujui what happened to Lissu, amedhoofisha taifa na kukitia aibu chama chake kwa kutofanya uteuzi nzuri wa Presidential position, mkabila sana, wakulima walishindwa kupata fursa za masoko kutokana na mazao yao... We have to heal the nation. He was the worst president ever.
 
Tutulie kidogo tutakuwa na la kusema mbele ya safari, huyu mwizi aliyetujengea Jiji la Dodoma akatuanzishia SGR akatununulia ndege zaidi ya 11 sasa hivi Twiga yuko hewani, akatuanzishia Bwawa na daraja Kigongo Busisi hata kama alikuwa ànalenga wakwe wapite darajani bila shida akatujengea Rusumo highdro vituo vyaAfua Nchi nzima vituo vya mabasi vya kisasa nashawishika kusema huo ni wizi mzuri sana kuwahi kutokea
 
Kama unadhani ufisadi ulianza jana basi unajidanganya sana.

Awamu ya kwanza kulikuwa na ufisadi wa kutisha sema mawasiliano wakati ule yalikuwa duni tu, utakumbuka RIP Nalaila Kiula alivyopiga dili pale UDA au yule mbunge wa Temeke mh Masoud na issue ya kivuko au wale akina Balyagati na michongo ya Hazina.

Syle ya Tumbua tumbua ya awamu ya 5 ndio ilikuwa mwarobaini.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!

Maendeleo hayana vyama.
Maendeleo gani? Kwani huoni kuwa watu wenyewe wanabadilika kutaka wao wenyewe maisha nafuu na mazuri kila siku. Kwani Serikali imewajengea nyumba hizo za kisasa wanazoishi? Acha kueleza hali tofauti na uhalisia!
 
Back
Top Bottom