Uchaguzi 2020 Bila unafiki unamshawishije mwalimu ambaye hajaongezwa mshahara kwa miaka mitano na bado ukambambika makato ya bodi kibabe aipende CCM?

Uchaguzi 2020 Bila unafiki unamshawishije mwalimu ambaye hajaongezwa mshahara kwa miaka mitano na bado ukambambika makato ya bodi kibabe aipende CCM?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Hebu tuwàsaidie hawa wenzetu kujibu swali hili japo naamini watumishi wote hawajaongezewa mishahara kwa miaka mitano mfululizo.

Mimi sio mwajiriwa wa Government Ila hebu leo nivae viatu vyao.

Imagine wewe ndio mwenyekiti wa chama cha siasa taifa unakuja kumuomba kura mwalimu ambae hujamuongeza mshahara wake kwa miaka mitano na Kama haitoshi ukampiga makato ya bodi ya mikopo ya 8% kibabe je mwalimu huyu unamshawishije akupe kura leo?

Hebu nisaidieni Mimi nimeshindwa.

Tiririka namna utakavyomshawishi mwalimu huyu akupe kura, tena mwaka huu na asahau ubaya uliomfanyia.

Kazi kwenu mabingwa wa kutongoza!
 
Mtachonga sana lakini akifika mwanaume lazima msaule.
 
Mimi nimewaza labda mwanasiasathe huyu ataanza hivi;

Unajua ndugu mwalimu nimekujengea flaiova (japo mwl yupo kakonko).

Unajua mwalimu nimekununulia bombadia kwi kwi kwi (mwl na bombadia wapi na wapi).

Unajua mwl nimekujengea bwawa la umeme (khaaaaaaaa mwl anashangaa).

Mwalimu niombee nikamilishe standaj geji (hapa ticha anafariki kwa presha).
 
Mama yangu mzazi mwaka jana nimemwambia uwalimu kwa Tanzania ni laana ulivyofika mwezi wa tano kazi kaacha.
 
Mimi nimewaza labda mwanasiasathe huyu ataanza hivi;

Unajua ndugu mwalimu nimekujengea flaiova (japo mwl yupo kakonko)...
😃😃 Mkuu wewe huyo huyo ndo mleta uzi halafu wewe huyo huyo ndo mtoa comments 😁 waachie walimu tuone wanachangia Nini hapo!.

Meaning no offense 😅.
 
😃😃 Mkuu wewe huyo huyo ndo mleta uzi halafu wewe huyo huyo ndo mtoa comments 😁 waachie walimu tuone wanachangia Nini hapo!.

Meaning no offense 😅.
Mkuu Lordrank sijajikataza kuvaa koti la mwenyekiti.
 
Mama yangu mzazi mwaka jana nimemwambia uwalimu kwa Tanzania ni laana ulivyofika mwezi wa tano kazi kaacha.
Mtoto mjinga humuudhi mamake, same thing you did broh!.

Congratulations because you made it 😃😃.
 
Kwa niaba ya walimu wenzangu tunasema mshahara unatosha na wala hatuhitaji nyongeza na kura tutampa Magufuli.
CCM oyee...😅
 
Walimu wanaelewa sana ,hawana tatizo labda ni were tu huelewi kwa nini most shahara haipandi.
Tunajenga nchi kwanza.
Ndio maana nimewaomba walimu waache unafiki waseme ukweli kwasababu nasikia mshahara wako ukiathiriwa kwa namna yoyote ile inaathiri mafao Yao ya uzeeni ya kustahafu ! Sasa je kama wanakubalina na kujenga nchi wanajua consequences zake baadae?

Maana Kama tu sasahivi wanaweka kadi kwa wakopeshaji vipi wakistahafu nguvu hakuna Tena nawakati huo mshawaingiza chakike kwamba hatuwaongezi mishahara tunajenga nchi?
 
Kwa niaba ya walimu wenzangu tunasema mshahara unatosha na wala hatuhitaji nyongeza na kura tutampa Magufuli.
CCM oyee...😅
Mleta uzi nilikwambia subiria maoni ya walimu, maoni mwenyewe ndo Kama haya Sasa, kwako mleta uzi.
 
Back
Top Bottom