Toka nizaliwe walimu always hua wanalia kuhusu mishahara kutokutosha so sioni hata awamu kama wangeongezewa wangepunguza vilio vya kila siku. Huenda vilio vyao havihusiani na uhalisia bali ubinafsi. Angalia hata Mkwere aliekuwa anawaongezea mishahara kila meimosi bado kuna waliomtosa na kuondoka na Lowasa alivohamia Chadema
Tatizo la kutokutosha kwa mshahara mnalichukulia kimasihara sana.Mh.Magufuli aliwahi kusema hata yeye mshahara wake pia hautoshi,wabunge mishahara haitoshi,Wafanyakazi serikalini pia haitoshi.
Kitu ambacho hakijadiliwi ni uwiano wa kutokutosha kwa mishahara kati ya wafanyakazi ndani ya Taifa/nchi maskini/ya kipato cha kati chini.Hapa Tanzania kuna watumishi wa umma/serikali na walioajiriwa katika sekta binafsi.Sitawajadili waliopo sekta binafsi kwa sababu hawa malipo yao yanaendana na nguvu ya kiuchumi ya taasisi husika,mahitaji ya soko au ujuzi wa mwajiriwa kulingana na mahitaji ya mwajiri.
Watumishi wa umma ndiyo wenye changamoto nyingizaid kwa sababu mishahara yao hupangwa na watunga sera ambao ni Wabunge na Serikali Kuu/Mitaa kupitia kwa Madiwani.(Naweza kusahihishwa) ambapo Kima Cha Chini sasa hivi ni <300,000/= kwa mwezi na wakati huo huo Kima Cha Juu hakifahamiki(Sikifahamu),ila nasikia wengine wanalipwa hadi >30 milioni kwa mwezi.Sasa tuambiane mshahara hautoshi,tusubiriane tumalize kujenga miradi ambayo hata wakati wa kuanzishwa kwake hatukuulizwa au kushirikishwa.Wapo watakaosema kuwa kisomo ndiyo kinazingatiwa kupanga mishahara,sawa.Je,tumewahi kujiuliza kuwa aina hii ya madaraja kati ya Wafanyakazi ilipendekezwa na nani,je huo msaafu huo unakuwa chini ya usimamizi wa nani?
Ushauri wangu ni kuwa,kama mfanyakazi wa chini kabisa anatakiwa kuwa na cheti,wote wenye cheti walipwe mshahara sawa kwa wote,Diploma zote walipwe mishahara sawa,Digrii au PhD nk.Hata kama kuna tofauti ziwe si kubwa kiasi cha moja kuweza kuharibu morali ya watumishi na iwe based kwenye ufanisi wa mtumishi.
Pia wanasiasa wasipewe mishahara minono kama ilivyo sasa ili kuepusha wafanyakazi wengi kukimbilia huko kwa sababu ya green pastures katika siasa na watumishi wasizuiliwe kushiriki siasa.Haya yakifanyika tutakuwa tumeondoa rushwa automatically na uchakachuaji wa michakato ya chaguzi zetu.
Tukifanya hivyo vile vile tutakuwa tumeokoa fedha nyingi sana na miradi ingekamilika ndani ya muda mfupi tofauti na sasa ambapo hakuna ajuaye inaenda kukamilika lini/au kama wataanzisha mingine bila kuathiri huduma zingine.Tanzania tunaweza kuibadilisha ndani ya muda mfupi sana kwa kubana pia maeneo kama ya magari ya serikali,sasa hivi tunaona magari ya gharama kubwa sana serikalini ilhali kuna magari ya bei nafuu na yenye ufanisi sawa na haya tuliyonayo.
Hatupaswi kuwaminya wafanyakazi kukamilishaau kujenga miradi,maisha yanaendelea.Mambo ni mengi...