Pre GE2025 Bila Uwepo wa CCM Madarakani Nchi ingekuwa Imesambaratika na Kugawanyika vipande vipande

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu Lukas acha kudanganya watu, nchi zote za Afrika zilipata uhuru zikiwa na vyama vingi vya siasa.

Na nchi nyingi sasa vyama vya siasa vikongwe vimeondolewa madarakani na hakuna nchi iliyosambaratika.

Tupe mfano wa nchi moja tu iliyosambaratika kwa sababu chama kikongwe kiling'olewa madarakani.

Kwa mfano Zambia, Malawi na kenya ni nchi jirani ambapo wamebadilisha vyama vya siasa madarakani mara kadhaa zimesambaratika???
Kasome historia ya CCM na Tanzania. Kasome historia ya vyama hivyo unavyosema vikongwe na nchi zao. Ni ngumu sana kuitenganisha Tanzania na CCM. CCM Ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM. Ni kama mtu na Samia yake. CCM Ndio Damu ya Taifa letu. Ikipungua kidogo basi ni lazima Taifa letu liteteleke.
 
Mkuu hapa umemaanisha nini..... "mtu na Samia yake?"

Naona hoja yako kwa ujumla inaonesha jinsi gani wewe una uelewa haba kuhusu CCM, Tanzania, vyama vikongwe barani Afrika, siasa ya vyama vingi Afrika na mwenendo wa mambo ya siasa duniani.

Ukikuwa na kujielimisha vizuri utaelewa tu!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nikitizama na kufuatilia namna vyama vya upinzani vinavyoendeshwa ,vinavyofanya maamuzi yake,mfumo wa uongozi na namna ya kupokezana madaraka, uvumilivu na demokrasia katika vyama hivyo nafikia hitimisho kuwa kama siyo uwepo wa CCM Madarakani basi Taifa hili lingekuwa limesambaratika na kugawanyika vipande vipande.

Angalia tu namna viongozi wa upinzani wanavyong'ang'ania madarakani kwenye vyama vyao hususani kwenye nafasi ya Uwenyekiti. Jiulize Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba Na Mh Mbowe ni wenyeviti wa vyama vyao tangia lini? Wameongoza kwa miaka mingapi? Kipi walichobakisha kinachowashinda kuacha mawazo mapya yachukue nafasi ndani ya vyama vyao? Angalia tu Mh Mbatia mpaka alitoka kwenye Uwenyekiti baada ya migogoro na kufurushwa na wenzake.

Vipi kama hawa wapinzani kama CHADEMA ndio wangekuwa wanaongoza nchi? Si wangebadili hadi katiba kwa kutaka mtu mmoja tu aendelee kuongoza yeye peke yake? Angalia tu namna ya kusuluhisha na kutatua migogoro ndani ya vyama hivi vya upinzani. Mara nyingi migogoro yao imeishia kufukuzana na kutupiana maneno hadharani.kwa kuwa havina ukomavu wala stamini ya kumaliza migogoro yao kwa amani na utulivu na kuendelea kuwa pamoja ndani ya chama.

Mfano vyama hivi vingekuwa na uwezo wa kusuluhisha migogoro yao basi tusingeshuhudia akina Mheshimiwa Zitto Kabwe, Profesa Kitila Mkumbo,Samsoni Mwigamba, Dkt Slaa, Juliana Daniel Shonza, Mtela Mwampamba, Julius Mtatirilo, David Kafulila, na wengine wengi wakidhalilishwa na vyama hivyo hasa CHADEMA kwa kuwa tu walikuwa na mawazo tofauti na ya Mwenyekiti wake wa Muda wote. Hapo bado sijazungumzia habari za akina profesa Lipumba na hayati Maalim Seif au hayati Agustino Lyatonga Mrema na wenzake.

Kwa hiyo unachokuja kuona ni kuwa vyama hivi bado ni vichanga sana ,ambapo haviwezi kamwe na katu kufikiriwa wala kuwaziwa kupewa ridhaa ya kuongoza Taifa letu.kwa kuwa bado havijakomaa kimfumo na hata namna ya kuendesha mambo yake.havina uwezo wa kuishi na kuwaunganisha watu wote hata wale wenye mitizamo tofauti ndani ya chama.ndio maana kwa kukosa ustahimilivu huko wa hoja mpya au mawazo kinzani huishia kufukuzana na kuwa maadui kama paka na panya.

Lakini ukija CCM Ni Chama ambacho kina uwezo wa kuishi na kukaa na watu wa aina zote na wenye mitizamo tofauti tofauti na kutoa nafasi ya kila mmoja kusikilizwa mawazo yake na kupingwa kwa hoja au kuelimishwa pasipo kuitwa adui wa chama au msaliti na hatimaye kufukuzwa. Ndio maana CCM imekuwa kimbilio la wanasiasa wote wanaoonewa kutoka upinzani.ni chama chenye utaratibu mzuri wa kutatua migogoro yake baina ya wanachama wake,mfumo imara wa kiuongozi na namna ya kuheshimu maamuzi ya chama.

Sasa leo kwa vyama vya upinzani unakuta wamefanya maamuzi kwa pamoja halafu anatokea kiongozi mwingine anasema sijuwi jambo hili la kumualika Rais kwenye chama chetu lilifayikaje? Cha ajabu ni kuwa huyo anayeuliza hayo hadharani ni kiongozi mwandamizi na aliyeshiriki katika vikao vyote halali mpaka mwisho wa vikao. hii yote ni kukosa uelewa wa maana ya uongozi na vikao halali vya chama na maamuzi yake. Je umewahi kuona ni nani ndani ya CCM anaweza kutoka hadharani kupinga maamuzi ya vikao halali ambavyo hata yeye mwenyewe alishiriki?

Kwa uchanga wa vyama vya upinzani pamoja na uchu na uroho wao wa madaraka ndio maana vinashindwa hata tu kuungana na kuunganisha nguvu zao na mikakati yao kwaajili ya kushinda uchaguzi fulani. kwa sababu vyenyewe kwa vyenyewe tu vinadharauliana na kushambuliana muda wote.haviaminiani wala kuamini katika umoja. Ni vyama vipo vipo tu na vilivyokosa muelekeo na Dira ya kueleweka ya kuweza kuviongoza.

Kama siyo uwepo wa CCM Madarakani kwa hakika kwa sasa tungekuwa tunashuhudia Taifa likiwa limejaa na kutamalaki ukabila uliokithiri, ubaguzi, Udini, ujinsi, ukanda, kudharauliana na mpasuko wa kila aina. Maneno ya kibaguzi mnayoyasikia kutoka kwenye vinywa vya viongozi kama Lissu za kwamba huyu ni wa upande ule na sisi ni wa upande huu yangekuwa yameshamiri na kukita mizizi ardhini. Kusingekuwa na habari za upendo, ushirikiano,umoja wa kitaifa, mshikamano na Taifa moja.

Habari na sera zao za majimbo zingeendelea kuligawa na kulipasua Taifa kila uchwao kwa misingi ya ukabila na ukanda. Vita vingetokea vya wenyewe kwa wenyewe na tungekuwa tukichaguana kwa kuangalia makabila yetu,Dini zetu na kanda tunazotokea. Kwa ufupi kusingekuwa na Taifa tena zaidi ya kuwa na vipande vipande vinavyojitegemea na vinavyohitaji uhuru na utambulisho wake.

Naweka kalamu yangu chini maana naona andiko linakuwa refu sana.nitaendelea wakati mwingine tena.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

It is not true kuwa chama kinaweza kusambaratisha nchi ila watu ndio wanaweza kusambaratisha nchi
 
Luca,tunajua kama wewe ni kichaa lakini usivae kimwanandani/chupi kichwani sasa!
 
Mwl. Nyerere alijitahidi kupiga vita udini na ukabila, lakini alichochea ubaguzi wa vyama kwa kuipa kipaumbele CCM hapa ndipo uozo ulipo anzia..
Na nukuu kauli yake

"Kiongozi mzuri hawezi kutoka nje ya CCM"
Hii kauli inalimaliza taifa mimi nasema yeye kama baba wa taifa hakupaswa kusema kauli za namna hiyo

Tena vita ya vyama imekuja kuwa mbaya sana kuliko ukabila na Udini,,

""Mfumo wa vyama vingi una tija kwenye suala la maendeleo lakini maendeleo hayana tija kwenye vyama"" chenye tija zaidi ni maendeleo ya taifa lakini kiongozi anapo toka chama flani basi huanza kuangalia maendeleo ya chama kuliko taifa hili ndio tatizo propaganda nyingi kuuana kwingi mara hivi mara vile ili tu chama chake kiwe juu,, ifiki hatua tukubali kupiga vita udini, ukabila, na huu mfumo wa vyama vingi
 
Ukweli wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere unaendelea kubakia kuwa ndio ukweli wenyewe kuwa kiongozi mzuri hawezi kutoka nje ya CCM.
 
Luca,tunajua kama wewe ni kichaa lakini usivae kimwanandani/chupi kichwani sasa!
Mungu Akubariki na kuifanya wikendi kuwa yenye amani na furaha kwako binafsi na familia yako. Mkono na uso wa Mungu uwe pamoja nawe wakati wote na Mungu asikuache kama ambavyo hakumuacha Mussa na YOSHUA katika kuwavusha na kuwapeleka wana wa islael nchi ya ahadi.
 
It is not true kuwa chama kinaweza kusambaratisha nchi ila watu ndio wanaweza kusambaratisha nchi
Chama ni watu.watu wakikosa wa kuwaongoza na kuwaunganisha lazima wapotee njia. Kama unavyoona leo Lissu anavyopandikiza ubaguzi na chuki kwa wafuasi wake ,jiulize angekuwa Rais hali ingekuwaje?ni lazima angewagawa watu na kulipasua Taifa letu.
 
Tatizo ni huyo lisu wala sio chama,, huyo hata angekuwa CCM hayo yangeendelea tu, hapa watu nilio wazungumzia ni hao viongozi wachache wenye maono ya ubinafsi na kujitengenezea nguvu wao kazi yao kubwa ni propaganda tu kutafutiana weakness tu angali wao walipo pata nafasi fulani hakuna walichofanya,, sasa watu wa namna hii hawafai kwa chama na taifa kwa ujumla, maana jitihada za mtu huonekana kwa kila position atakayo kuwepo sasa kama walipata position ndg na hakuna walichofanya vipi wakipata position kubwa?? ""Tatizo sio chama tatizo ni tamaa za wanachama"" kiongozi mwenye uzalendo na taifa lake anaye tamani kufanya kitu kwenye hili taifa anaweza kutokea chama chochote,, kama matamanio yake ni kuhakikisha Tanzania inafika sehemu fulani atachagua ni chama gani apitie ili afikie pale anapo taka kufika kwa huyu mtu msukumo wake wala sio chama ni uzalendo uliopo ndani yake,,

Chama chochote kinaweza kutoa kiongozi mzuri au mbaya

ACHENI MAMBO YA UANACHAMA lazima ifike hatua watu tubadilike mitazamo yetu,, huu upuuzi uliopandikizwa kwenye vichwa vya watu unawafanya waone bila CCM basi nchi itasambaratika hii si kubaliani nayo wala si ungi mkono mawazo ya Mwl. Nyerere mnatutengenezea mifumo ya kipuuzi tu..
Mnatengeneza mifumo ya kuwa viongozi wale wale tu miaka yote kutoka na huu mfumo,, usihukumu chama kutokana na ujinga unaofanywa na mtu mmoja chama chochote kina watu wabaya na wazuri lakini wazuri hawapo kwenye hizo nafasi za juu hata kama wapo basi wameinamisha vichwa vyao tu kama kobe wana subiri time ina hitaji utulivu wa fikra kuwa tambua viongozi wa namna hii acheni UCHAMA
 
Hii nchi itakuwepo ata baada ya wewe kufa.Dunia ina nchi nyingi sana nakote uko wana maisha yao,what is so special kwa tanzania ya Ccm.Ccm itaondoka na nchi itaendelea kuwepo.Ccm alichonufaika nacho ni ukongwe tu kitu ambacho chama chochote kingeweza kufanya.Kwahiyo acha kukipa umuhimu ambao hakina.Labda kama unajipendekeza wakufikirie.
 
Ukweli wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere unaendelea kubakia kuwa ndio ukweli wenyewe kuwa kiongozi mzuri hawezi kutoka nje ya CCM.
Inahitajika nguvu sana kuwatoa watu kwenye fikra za namna hii baba wa taifa sio Mungu wenu yule,, CCM ina viongozi ambao hawako tayari kuachia position zao ili na wengine pia waingie huko kwahiyo CCM kuna ushindani mkubwa sana,, hapa kwa mtu mwenye nia ya kuinyoosha TZ anaweza kupitia Chama chochote tu
 
Jinga wewe jadanganye bibizako kijijini!! Marekani imepokezana vijiti katika uongozi nilini iligawanyika?
 
Hii nchi itakuwepo ata baada ya wewe kufa.Dunia ina nchi nyingi sana nakote uko wana maisha yao,what is so special kwa tanzania ya Ccm.Ccm itaondoka na nchi itaendelea kuwepo.Ccm alichonufaika nacho ni ukongwe tu kitu ambacho chama chochote kingeweza kufanya.Kwahiyo acha kukipa umuhimu ambao hakina.Labda kama unajipendekeza wakufikirie.
CCM inanufaika na kuendelea kusalia madarakani kutokana na uimara wake ,sera na ajenda zake nzuri zinazogusa maisha ya watu,historia yake ,mfumo imara wa kiuongozi na kujiendesha kitaasisi. Wakati vyama vingine kama CHADEMA vimejengwa katika kumzunguka na kumtegemea mtu badala ya mfumo. Ndio maana Mbowe anaonekana hana Mbadala kwa chama chake katika nafasi ya uwenyekiti.
 
Amani ni tunda la Haki ,
Haki ikiimarika Amani itaendelea kutamalaki ,
Haki ipo na inaendelea kutamalaki na ndio maana amani Inaendelea kutamalaki.kwa kuwa watu wanaona wakitendewa haki.na pale panapotokea mtu kaonewa namtu basi hatua huchukuliwa.ndio maana watu wanaendelea kuwa na imani na CCM na Serikali yake.
 
Jinga wewe jadanganye bibizako kijijini!! Marekani imepokezana vijiti katika uongozi nilini iligawanyika?
Tanzania siyo Marekani na Marekani siyo Tanzania. Kila nchi ina historia yake na mfumo wake. Mbona uingereza kuna mfalme wakati hapa Nchini hakuna? Soma uelewe historia ya nchi yako.
 
Inahitajika nguvu sana kuwatoa watu kwenye fikra za namna hii baba wa taifa sio Mungu wenu yule,, CCM ina viongozi ambao hawako tayari kuachia position zao ili na wengine pia waingie huko kwahiyo CCM kuna ushindani mkubwa sana,, hapa kwa mtu mwenye nia ya kuinyoosha TZ anaweza kupitia Chama chochote tu
Kiongozi anaweza kutokea chama chochote kile, lakini kiongozi bora ,makini na mzalendo ni lazima atokee CCM
 
Tatizo ni huyo lisu wala sio chama,, huyo hata angekuwa CCM hayo yangeendelea tu, hapa watu nilio wazungumzia ni hao viongozi wachache wenye maono ya ubinafsi na kujitengenezea nguvu wao kazi yao kubwa ni propaganda tu kutafutiana weakness tu angali wao walipo pata nafasi fulani hakuna walichofanya,, sasa watu wa namna hii hawafai kwa chama na taifa kwa ujumla, maana jitihada za mtu huonekana kwa kila position atakayo kuwepo sasa kama walipata position ndg na hakuna walichofanya vipi wakipata position kubwa?? ""Tatizo sio chama tatizo ni tamaa za wanachama"" kiongozi mwenye uzalendo na taifa lake anaye tamani kufanya kitu kwenye hili taifa anaweza kutokea chama chochote,, kama matamanio yake ni kuhakikisha Tanzania inafika sehemu fulani atachagua ni chama gani apitie ili afikie pale anapo taka kufika kwa huyu mtu msukumo wake wala sio chama ni uzalendo uliopo ndani yake,,

Chama chochote kinaweza kutoa kiongozi mzuri au mbaya

ACHENI MAMBO YA UANACHAMA lazima ifike hatua watu tubadilike mitazamo yetu,, huu upuuzi uliopandikizwa kwenye vichwa vya watu unawafanya waone bila CCM basi nchi itasambaratika hii si kubaliani nayo wala si ungi mkono mawazo ya Mwl. Nyerere mnatutengenezea mifumo ya kipuuzi tu..
Mnatengeneza mifumo ya kuwa viongozi wale wale tu miaka yote kutoka na huu mfumo,, usihukumu chama kutokana na ujinga unaofanywa na mtu mmoja chama chochote kina watu wabaya na wazuri lakini wazuri hawapo kwenye hizo nafasi za juu hata kama wapo basi wameinamisha vichwa vyao tu kama kobe wana subiri time ina hitaji utulivu wa fikra kuwa tambua viongozi wa namna hii acheni UCHAMA
Chama kinachojitambua na kuelewa dhamana kiliyoibeba kilipaswa kujitenga na kauli za Lissu na kusema kuwa kauli zake zile za kibaguzi na chuki siyo za chama wala siyo msimamo wa chama. Na kilipaswa kusisitiza umoja na mshikamano na kutoa kauli za kuwaunganisha watu. Sasa wao CHADEMA wanaendelea kwa upofu wao wa akili kuunga mkono na kushadadia kauli za kibaguzi na chuki za lissu.jambo ambalo linafanya wananchi waendelee kukipuuza chama na kukishambulia kwa kauli zake za kuligawa Taifa na watanzania kwa ujumla wake.
 
Back
Top Bottom