Bila wazungu, maisha yangekuwa magumu sana hapa duniani

Wazungu ni watu gani,? na wachina ?
 

Hivi unajua formula nyingi tu za hesabu na Physics zimetoka Misri na ndio sababu hata yale mapramidi wazungu hawajui yalijengwaje....kwa technologia ya miaka hiyo
Hivi unajua vyombo vya udongo duniani vilikuwa vinatemngezwa Ghana
Wazungu wakakata mikono waafrica mafundi

Wazungu wasingekuja Africa, tungekuwa tuna maendeleo Kama china na zaidi
 
Tatizo la hoja hii ni kuchanganya maendeleo ya binadamu na ubora wa jamii moja. Wazungu wamechangia sana katika sayansi na teknolojia, hilo halina ubishi, lakini si sahihi kufuta mchango wa Waafrika, Waarabu, Waasia na ustaarabu mingine kana kwamba kabla ya Ulaya hakukuwa na ubunifu. Historia ya binadamu ni historia ya kubadilishana maarifa, si mali ya rangi moja. Pia, kuwa na teknolojia za kisasa hakumaanishi jamii nyingine zilikuwa “zinaishi kama ngedere.” Huo ni mtazamo wa kibaguzi zaidi kuliko hoja ya kihistoria.
 
Mafuta unayojipaka yanatoka nchi gani?
 
Wengi hatukubali ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…