Bila wazungu, maisha yangekuwa magumu sana hapa duniani

Tatizo la hoja hii ni kuchanganya maendeleo ya binadamu na ubora wa jamii moja. Wazungu wamechangia sana katika sayansi na teknolojia, hilo halina ubishi, lakini si sahihi kufuta mchango wa Waafrika, Waarabu, Waasia na ustaarabu mingine kana kwamba kabla ya Ulaya hakukuwa na ubunifu. Historia ya binadamu ni historia ya kubadilishana maarifa, si mali ya rangi moja. Pia, kuwa na teknolojia za kisasa hakumaanishi jamii nyingine zilikuwa “zinaishi kama ngedere.” Huo ni mtazamo wa kibaguzi zaidi kuliko hoja ya kihistoria.

Binadamu ameendeleaje na bado yuko vile vile? Hiyo Sayansi na Teknolojia imekuongezea nini wewe SMART PASSENGER kama binadamu?
 
Mafuta unayojipaka yanatoka nchi gani?
Ukifikiria kisayansi na sio kihistoria; Binadamu wameumbiwa kutatua changamoto kwa namna rahisi zaidi
Kwa mazingira ya kiafrika ambapo sehemu kubwa ni joto, mafuta ya kujipaka - kuongeza nishati /joto hayawezi kuwa kipaumbele kwa mababu zetu... Ukweli tusingetawaliwa tukavurugwa, tungekuwa level ya first world!

Hata hii Elimu ya hovyo kabisa ya kukariri, tuliyoletewa na wazungu, ndiyo imetuharibu vichwa kabisa. Unakuta mtu amesoma kabisa ILA hana maarifa.....Ungekuta tunaenda na Elimu yetu ya Asili ya Hesabu na sayansi iliyo asisiwa Afrika (Misri)..hatungekuwa na watu wenye mawazo ya kijinga kijinga kama sasa hivi...

Fuatilia Nchi za Kiafrika za kaskazini zilizo jikita kwenye Elimu yetu ya Asili (Sayansi na Hesabu); Misri yenyewe, Tunisia, Libya, Morocco nk hizo Nchi ukifika kwao hakuna tofauri na mtu aliyeko Ulaya.

Huko kwengine, wamejikita kwenye Historia, Kiswahili, English nk halafu wanataka maendeleo....
 
Ukifikiria kisayansi na sio kihistoria; Binadamu wameumbiwa kutatua changamoto kwa namna rahisi zaidi
Kwa mazingira ya kiafrika ambapo sehemu kubwa ni joto, mafuta ya kujipaka - kuongeza nishati /joto hayawezi kuwa kipaumbele kwa mababu zetu...

Ukweli tusingetawaliwa tukavurugwa, tungekuwa first world!
Hata hii Elimu ya hovyo kabisa ya kukariri, tuliyoletewa na wazungu, ndiyo imetuharibu vichwa kabisa. Mtu hata amesoma anakosa maarifa.....Ungekuta tunaenda na Elimu yetu ya Asili ya Hesabu na sayansi iliyo asisiwa Afrika (Misri)..hatungekuwa na watu wenye mawazo ya kijinga kijinga kama sasa hivi....
Si ajabu tungekuwa bado kwenye ulimbo na ulindi ili kupata moto
 
Huko vyuo vikuu, vitabu vimetoka wapi?
Vitabu vinaandikwa na waandishi, ila elimu inatoka sehemu mbalimbali duniani,

Kitabu kama kitabu kwa miaka mingi kinatumia karatasi, karatasi ambayo imegunduliwa china miaka kama 2000 iliopita.

Kabla ya hapo wazungu walitumia Ngozi za wanyama, ili uandike ABCD inabisi ng'ombe ama Mbuzi adondoshwe.
Parchment_from_goatskin.jpg

Waarabu na huku Africa tulitumia udongo wa mfinyanzi na miti ya mianzi kutengeneza sheet za kuandikia
Ebers-Papyrus-Ancient-Egyptian-Medical-Text.jpg

Vyote hivyo vilikua na gharama na kufanya Elimu iwe ngumu kusambaza, imagine kitabu cha kurasa 200 utadondosha wanyama wangapi kumpa mtu mmoja kitabu?

Wachina ndio wakagundua karatasi za Leo za mbao ambazo no rahisi sana na kutusambazia technology Yao, mpaka Leo unaoenda kununua Gazeti ama kitabu kwa sh mia kadhaa ama elfu kadhaa ni juhudi zao hao wachina.
 
Si ajabu tungekuwa bado kwenye ulimbo na ulindi ili kupata moto
Fuatilia Nchi za Kiafrika za kaskazini zilizo jikita kwenye Elimu yetu ya Asili (Sayansi na Hesabu); zikiongozwa na Misri, Tunisia, Libya, Morocco nk hizo Nchi ukifika kwao hakuna tofauti na mtu aliyeko Ulaya.
Kwa Misri wataalam wake wa Hesabu na sayansi walijenga mapiramid hadi leo wazungu hawajaweza kujua yalijengwaje. Pia hizo nchi zipo jangwani ila ukiangalia Kilimo hujawahi kusikia waki lia lia kwa njaa nk nk

Huku kwengine, wamejikita kwenye Historia, Kiswahili, English nk halafu wanataka maendeleo....
 
Hizo nchi zote unazoziona, zinamtegemea mzungu, kuanzia kwenye bank ya dunia, utumiaji wa sarafu n.k
Ukiagiza mafuta Uarabuni, unalipia sarafu ya uarauni au ya mzungu?​
 
Kuna jamaa tuliwahi kubishana nilimuuliza, unaamini kwamba sisi ngozi nyeusi ni useless duniani ukilinganisha na ngozi nyeupe? Akasema hapana, ninadamu wote ni sawa.

Nikamuuliza, unadhani haya madini tunayosema wazungu wanatuibia siku ikitokea wakasema hawayataki tena tubaki nayo sisi tutayafanyia nini? Akasema tutagundua namna ya kuyafanyia.

Nikamuuliza, unadhani wazungu wamemaliza kugundua aina za vitu asilia wanavyoweza kuvitumia na kuvipa thamani? Akasema hapana wanaweza gundua vingine.

Nikamuuliza, umewahi kusikia yule mzungu aliyegundua inji ya gari inayotumia maji? Akasema nimewahi sikia.

Nikamuuliza, unadhani hawana teknolojia nyingine zaidi ya mafuta na umeme? Mfano wakasema kubadiri maji yabahari au maji yeyote tu yakaendesha gari au kitu chochote tu kama mchanga au majini ya mwembe yakaendesha chbo chenye thamani? akasema hivyo ulivyovitaja haviwezi kuwa converted to mechanical energy.

Nikamuuliza, ni nani aliyekufundiaha kuwa kuna mechanical energy? Elimu hio uliitoa wapi? Akasema kwa mzungu.

Nikamuuliza, sasa huoni kuwa wanaweza kuja na energy nyingine na wakaipa jina lingine, ikazalishwa mali ghafi zingine tu kama majani ya papai? Akasema inawezekana ila itawachukua muda sana?

Nikamuuliza, unadhani wao wanahara kama tuliyonayo sisi, ya kufikiri kuwa mimi muda wangu umeisha naelekea kufa kwa hio sipaswi kichonga njia? Akakaa kimya.

Nikamuuliza, huoni siku wakigundua mali ghafi zingine hio mali ghafi watakua wameipa thamani ambayo sasa haina? Akasema ndio.

Nikamwambia, basi, vyooote tunavyoviona ni vya maana asilimia kubwa ni wao wanaovipa thamani, wao ndio wanajua wavifanyie nini, kama tunataka na sisi kugundua, na kujua nini tukifanyie nini ni lazima tuache umimi, tuache kujifikiria sisi na tuwekeze kwa ajili ya kesho kama akina Nikola Tesla na wengine walivyoteseka huku matajiri wakiweka pesa kwao ili wafanye vumbuzi.
 
Hoja yako imejitosheleza
 
Umeongea kinyume chake Mkuu. African civilisation ilikuwa ipo juu sana kabla ya ujio wa hao viumbe. Hatukuwa na ulcers, stress, gonnorhea, HIV/AIDS, matatizo ya nguvu za kiume, saratani, WMDs na nuclear threats.
Tuliishi maisha halisi, yenye furaha na amani tele. Tulikula vyakula vyenye afya vyenye kutupa nguvu za kufurahia tofauti za kibaiolojia na wenza wetu na sio GMOs ambavyo vinatuandaa kuwa wateja wa kudumu wa dawa za viwanda vyao.

Hivi unajua kabla ya wazungu kuja wala hatukuwa na kausha damu? Ndiyo, tuliishi kwa kubadilishana bidhaa kabla ya kukutana na athari za monetization economy ambazo zimeleta ubinafsi na tamaa.
 
Bila wazungu, madini tuliyonayo yatakuwa na soko?
 
Kiukweli tuliweza kuendesha maisha yetu bila hata kuchimba hayo madini na hatukuwahi kulala njaa. Rasilimali zilizo juu ya ardhi na zile za kwenye rasilimali maji (samaki) zilitutosha na tuliridhika kuishi kwa furaha na amani.

Watu wa DRC kwao hayo madini si baraka bali ni laana kwakuwa ndiyo yanayowafanya washindwe kuishi kwa amani na utulivu
 
Back
Top Bottom