mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Katika kuaanda michakato ya kuwatafuta na hatimaye kufanikiwa kuwapika makada vijana na kuwa viongozi mahiri hapa nchini, basi CDM inastahili kongole zake. Kitu kama hicho ambacho alikifanya Mwl. Nyerere katika kipindi cha ile CCM iliyokuwa na agenda za kisiasa zenye kubebwa na hoja makini.Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimaye Peter Lijualikali apata mpinzani Kilombero naye si mwingine ni Nabii Bilionea Daniel Shilla.
Nabii Shilla ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Kilombero kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
"Maendeleo hayana chama".
Wimbo wa Sholomwamba akimnadi Nabii Shilla ubunge Kilombero
Akimuonya Lijualikali na Gwajima
Si hii CCM ama UVCCM ya sasa, wote ni wale wale, kumejaa wababaishaji toka viongozi Taifa mpaka mashinani. Wote hutegemea tu mbeleko ya dola ktk kukabiliana na washindani wengine wa kisiasa pasipo kulimudu vyema jukwaa la kisiasa kama njia ya kujenga hoja shindani.
Hata hapa ndani ya jukwaa hili, utakuta mtu anaanzisha uzi wenye maudhui mazuri kwa ajili ya mijadala pevu, lkn wana Lumumba aka Buku 7 wao huja na kauli nyepesi nyepezi na tena zenye maudhui kama njia yao pekee ya kutaka kuleta uharibifu ktk hoja iliyotolewa, kwa malengo ya kumtoa mtoa hoja kwenye reli.
Hii ndiyo njia pekee iliyobaki kwa wao kukwepa kujibu hoja kinzani. Tunapoelekea kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, hoja mezani itakuwa ni kwa namna gani CCM ilitekeleza ilani Yao iliyopita ya uchaguzi. Ilikuwa ni kwa maendeleo ya vitu ama ya watu, hapo hakuna ujanja ktk hili, si TAKUKURU ama Jeshi la Polisi litawasaidia ktk hili.