Uchaguzi 2020 Bilionea Nabii Shilla ajitosa kumkabili Lijualikali jimbo la Kilombero kupitia CHADEMA

Katika kuaanda michakato ya kuwatafuta na hatimaye kufanikiwa kuwapika makada vijana na kuwa viongozi mahiri hapa nchini, basi CDM inastahili kongole zake. Kitu kama hicho ambacho alikifanya Mwl. Nyerere katika kipindi cha ile CCM iliyokuwa na agenda za kisiasa zenye kubebwa na hoja makini.

Si hii CCM ama UVCCM ya sasa, wote ni wale wale, kumejaa wababaishaji toka viongozi Taifa mpaka mashinani. Wote hutegemea tu mbeleko ya dola ktk kukabiliana na washindani wengine wa kisiasa pasipo kulimudu vyema jukwaa la kisiasa kama njia ya kujenga hoja shindani.

Hata hapa ndani ya jukwaa hili, utakuta mtu anaanzisha uzi wenye maudhui mazuri kwa ajili ya mijadala pevu, lkn wana Lumumba aka Buku 7 wao huja na kauli nyepesi nyepezi na tena zenye maudhui kama njia yao pekee ya kutaka kuleta uharibifu ktk hoja iliyotolewa, kwa malengo ya kumtoa mtoa hoja kwenye reli.

Hii ndiyo njia pekee iliyobaki kwa wao kukwepa kujibu hoja kinzani. Tunapoelekea kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, hoja mezani itakuwa ni kwa namna gani CCM ilitekeleza ilani Yao iliyopita ya uchaguzi. Ilikuwa ni kwa maendeleo ya vitu ama ya watu, hapo hakuna ujanja ktk hili, si TAKUKURU ama Jeshi la Polisi litawasaidia ktk hili.
 
Bahati mbaya huwezi kukumbatia pesa halafu ukabaki na Yesu, hawa watu wanaonesha jinsi walivyo watafutaji, nawasikitikia sana hao waumini wao, naona msimu wa fursa kwao umewadia.
Hawa watumishi bhana nadhani waumini wao wameshafahamu wanaongozwa na watu wa aina gani.
 
Huyo Gwajima si mlikuwa mnamtumia kuishambulia CHADEMA?Na hiyo ndio maana halisi ya kuchanganya dini na siasa.
Gwajima wakati anamshambulia Makonda na ccm, na kipindi kile akiwa mshenga wa kumleta Lowasa chadema hakuwa anachanganya dini na siasa?

Mkuu kwenye huu uchaguzi mnaweza kuvuna aibu
 
Gwajima wakati anamshambulia Makonda na ccm, na kipindi kile akiwa mshenga wa kumleta Lowasa chadema hakuwa anachanganya dini na siasa?

Mkuu kwenye huu uchaguzi mnaweza kuvuna aibu
Hapana,pale alikuwa anakemea matendo mabovu ya watawala(doublestandard) na hilo ni jukumu la kiongozi yoyote wa dini.
 
Clip zake ndio zitatumika kumnyoosha na tunaomba mumpitishe tu ili tuje tumuumbue.
Clip zipi mkuu? Hizihizi ambazo watu wameshaziona na kuzidampo?
Hivi kabisa Gwajima unahisi hawezi kupata ubunge kisa zile clip?
Watu walitaka kumpeleka Ikulu fisadi Lowasa sembuse crip ya video ambayo hata haijathibitishwa kama ni yeye?
 
Clip zipi mkuu? Hizihizi ambazo watu wameshaziona na kuzidampo?
Hivi kabisa Gwajima unahisi hawezi kupata ubunge kisa zile clip?
Watu walitaka kumpeleka Ikulu fisadi Lowasa sembuse crip ya video ambayo hata haijathibitishwa kama ni yeye?
Acheni maneno mengi,mleteni ulingoni na msitumie dola alafu muone mtachoambulia.
 
Haya ya Gwajima kuishambulia chadema ni side B ya tape, ukigeuza side A utayakuta pia yamegeukia kwa ccm km hayo.
 
Huyu mwepesi sana,asubuhii na mapema anapigwa mtama.
 
Huyu kwa kazi anazozifanya za Unabii mamboleo, sitashangaa akiwa PANDIKIZI. Mkimpitisha huyu, Mgombea wa CCM hatapata UPINZANI wa Chadema
 
Yuko vizuri sana. Anashinda huyu kijana hakika!
 
ninashangaa sana wakati wa uchaguzi ukifika, unakuta wakazi wa dar wanaenda kutangaza nia mikoani utasema mikoani hakuna watu wa kugombea uongozi na uwezo wa kuongoza maeneo yao wanayoishi, fikiria mtu hata haishi eneo analotaka kuwakilisha, mfano steve nyerere anagombea iringa, zaidi ya miaka kumi tunamfahamu anaishi mji huuhuu wa dar, kinachomshinda kugombea anakoishi nini anaenda mikoani, hata huyu nabii bilionea na yeye ni wa mji huuhuu anatangaza nia kilombero, hivi kilombero hakuna wenyeji waishio huko ambao wanaweza kuongoza???
 
Kabla ya hivyo vyama mbadala chama kikuu na pelee kilikua ni ccm, kwaio hivyo vyama vilivyofuata vyote ni uzao wa ccm, hakuna jipya hapo tutafuten pesa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…