Bilionea Rostam Aziz amemalizana na Vodacom Tanzania (Auza hisa zote kwa Vodacom SA)

Bilionea Rostam Aziz amemalizana na Vodacom Tanzania (Auza hisa zote kwa Vodacom SA)

Kuuliza si ujinga, hivi ikitokea unanunua hisa mfululizo mpaka umekamata umekamata asilimia kubwa ya shares mahali mahali moja kwa moja unakuwa mmiliki wa kampuni husika?
Exactly kama jumla ya hisa zilizo orodheshwa na kampuni usika let's say ni laki tano ambazo zinakuwa mikononi mwa watu mbali mbali ambao ni ordinary na preferred ukiweze kuwashawishi ukazinunu a zote basi kampuni itakuwa yako. Lkn mara nyingi sheria hairuhusu shares zote kumilikiwa na mutu mmoja maana ikitokea hvyo hyo Haitakuwa tena public company bali italudi kuwa private maana itakuwa inamilikiwa na mutu mmoja.
 
Kuna jamaa yangu alinunua hisa za vodacom kipindi wanauza mwaka juzi anasema hazijapanda bei hata sh. 1 mpaka leo.
Hii biashara ya hisa ina wenyewe.
Toka mkuu ameingia kwenye kiti biashara ya hisa imekuwa ya kidwazi sana sema kuna makampuni bei za hisa zinapanda ikiwemo na vodacom japo sio kwa proportion iliyozoeleka.
 
Kuna jamaa yangu alinunua hisa za vodacom kipindi wanauza mwaka juzi anasema hazijapanda bei hata sh. 1 mpaka leo.
Hii biashara ya hisa ina wenyewe.
Halafu haziuziki Rostam kawezaje kuuza? Soko la hisa litoe utafanunuzi kwa Nini hisa zingine Kama hizo za Rostam zinauzika na zingine haziuziki kwa Nini? Waandishi wa habari fuatilieni hilo
 
Kampuni za simu za mkononi zitaanguka sana kimapato wakati sheria ya usajili wa line za simu itakapoanza kazi rasmi hapo mwishoni mwa mwezi huu. Taarifa za TCRA wiki iliyopita ni kuwa asilimia 12 tu ya wamiliki wa line za simu ndio walikuwa wamesajiliwa.
Hivi mwisho wa kusajili ni lini mkuu, maana kila siku Wamejitahidi kunitumia sms ya kujisajili ninaignore tu
 
Halafu haziuziki Rostam kawezaje kuuza? Soko la hisa litoe utafanunuzi kwa Nini hisa zingine Kama hizo za Rostam zinauzika na zingine haziuziki kwa Nini? Waandishi wa habari fuatilieni hilo
Wengi hapa mlinunua zile ordinary shares zilizouzwa Tsh. 850/share,so kama ulinunua hisa za Tsh.5mil maana yake ulinunnua hisa almost 5900 tu,hapo hujawaweka walionunua hisa za Tsh. mil. 1 ambao ni wengi.

Sasa mwenzenu ameuza hisa zake mil 588 ambazo zilikua ni 17.5% ya total shares, kwanini Major shareholders wasinunue fasta fasta ili waendelee kuongeza Controlling interests.

Inshort nyinyi mnamiliki vijihisa tu wala majority s/holders hawana habari na nyinyi ndio maana hata mkienda pale kwa brokers hamna mtu ana shobo na shares zenu,ila mtu yoyote tajiri mwenye hisa za mabilioni za voda akitaka kuziuza hata leo ni fasta tu.

Ushauri:Muwe mnatafuta kwanza ushauri khs mambo ya hisa kabla hamja yakimbilia kuzinunua.
 
View attachment 1214645

Tanzanian Tycoon Rostam Aziz Sells Last Tranche Of Vodacom Shares For $220 Million

Tajiri Kongwe nchini Tanzania Rostam Aziz, Hatimaye amemalizia Ngwe ya Mwisho ya Mauzo fungu la mwisho la Hisa zake za Vodacom Tanzania kwa kuwauzia Vodacom South Africa.

Kwa Mujibu wa report kutoka Citizen newspaper, Aziz ameuza fungu lake la 588 million (Shea) iliyokuwa imebaki Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mirambo Holdings, Moja ya kampuni zake za uwekezaji kwendaVodacom South Africa, kwa dili lililokamilishwa kupitia Dar es Salaam Stock Exchange Jumatano iliyopita.

Shea (Shares) hizo zilithaminishwa kwa takribani dola milioni mbili na ishirini $220 wakati wa mauzo. Msemaji wa Vodacom Tanzania hakutaka kutoa ushirikiano wakati alipoombwa kutoa maoni yoyote juu ya hilo.

Dili hilo limekuja karibu Miezi kumi tangu 'Washikadau' (shareholders) wa Dar es Salaam Stock Exchange-kuorodhesha kupitishwa kwa mauzo ya sehemu ya Mirambo Holdings iliyobaki Vodacom Tanzania

Rostam Aziz (55) ndiye aliyewezesha kuingia kwa Vodacom South Africa nchini Tanzania, awali alikuwa akimili wastani wa asilimia ya 35% fungu ndani ya Vodacom Tanzania.

Mwaka 2014, aliuza asilimia 17.2% ya fungu la Vodacom Tanzania iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni yake ya binafsi ya uwekezaji Cavalry Holdings, iliyosajiliwa Jersey Island ikiwa na umiliki wa 17.8% ya hisa.

Rostam Aziz, ni bilionea wa kwanza nchini na bado anaongoza kwa biashara. Mbali na kumiliki hisa zake Vodacom Tanzania, amepata utajiri mkubwa kupitia mikataba ya uwekezaji na ujenzi wa Biashara za Mgodi Caspian Mining, Bandari ya Dar es Salaam, Majengo ya Biashara na Makazi nchini na Mashariki ya kati sambamba na uwekezaji kupitia vyombo vya habari nchini Tanzania (Channel Ten/Magic FM/ DTV/CTN/C2C nk).

Mwezi July Mwaka huu alizindua Biashara ya kiwanda cha Ujazaji gesi, Dar es Salaam (Petroleum Gas-LPG) yenye thamani ya dola za kimarekani $65Millioni.
chanel 10 na Magic kanyanganywa na ccm
 
Inshort nyinyi mnamiliki vijihisa tu wala majority s/holders hawana habari na nyinyi ndio maana hata mkienda pale kwa brokers hamna mtu ana shobo na shares zenu,ila mtu yoyote tajiri mwenye hisa za mabilioni za voda akitaka kuziuza hata leo ni fasta tu.

Ushauri:Muwe mnatafuta kwanza ushauri khs mambo ya hisa kabla hamja yakimbilia kuzinunua.
Sijaelewa.Ni hivi kwani mnunuzi wa hisa ukienda kununua hisa unaenda kusema unataka hisa za Juma au hamisi au Rostam?.Si unaomba tu kununua hisa zilizoko sokoni .Kwani Kuna mahali pa kujaza kuonyesha unazitaka za Magdalena au za Asha Ngedere?
 
Channel 10&Magic fm-Ilikua Mali ya Rostam kwa sasa inamilikiwa na CCM,jiulize ilikuaje ikarudi CCM?

Vodacom Tz-Ililetwa na CCM nchini wkt Jamaa akiwa mweka hazina wa CCM,akaipiga juu kwa juu.

Leo ukiwauliza mlipateja pesa nyingi hivi?zina anza story ooh babu yetu alikua anafanya biashara za ngozi kutoka huko Igunga&Bukene kupeleka nchi za nje,hajah kalaghabaho.
Kaibe na wewe CCM,
Haya ndio matatizo ya Mswaha,mtu akifanikiwa tu kimaisha mnamwita mwizi
kaibe na wewe sasa tuone kama utafanikiwa[emoji2211]
 
Huyo jamaa ni noma..
Kapiga bei fasta kabla kitumbua hakijaingia Mchanga..
Musiba aliwahi kusema Vodacom ni msaada wa Mandela kwa CCM , sasa sijui ni akina nani ndani ya CCM waliichomoa Vodacom ndani ya CCM kiaina..
Sasa hiyo ni Vodacom , vp kuhusu mali zingine za chama zilizokwapuliwa kiujanja ujanja...!
 
Demand&Supply ina rule kwny uuzaji wa hisa

Rostam alikua at 1st ana 35% percent ya tota shares,so alikua ni minor s/holder akauza akabakiza 17.5% alizozimalizia kuuza sasa.

So point ya msingi hapa ni kwamba rostam alikua anauza shares mil. 588 at per zinazo represent 17.5%,kitu ambacho lazima akitaka kuuza shars zake Major shareholder watazitaka fasta kuongeza % ya umiliki wa hisa kwny Co.

Nyie wananchi mnaouza hisa zenu sijui 100 au 500 mjiulize zina represent % ya total shares za Voda?Mngekua na shares za maana wala msingepata tabu kuuza,brokers wangewagombania wale commision ya maana.
Sijaelewa.Ni hivi kwani mnunuzi wa hisa ukienda kununua hisa unaenda kusema unataka hisa za Juma au hamisi?.Si inaomba tu kununua hisa zilizoko sokoni .Kwani Kuna mahali pa kujaza kuonyesha unazitaka za Magdalena au za Asha Ngedere?
 
Cha ajabu babu yako ameanza kufuga ng'ombe,kuku,kuuza mazao shambani,kuuza ngozi kitambo kabla hata ya babu yake Rostam lkn mpk leo bado analimia jembe la mkono.

Kamwambie na yeye aanze ku-export awe tajiri kama Rostam,hahah.
Kaibe na wewe CCM,
Haya ndio matatizo ya Mswaha,mtu akifanikiwa tu kimaisha mnamwita mwizi
kaibe na wewe sasa tuone kama utafanikiwa[emoji2211]
 
Back
Top Bottom