Wengi hapa mlinunua zile ordinary shares zilizouzwa Tsh. 850/share,so kama ulinunua hisa za Tsh.5mil maana yake ulinunnua hisa almost 5900 tu,hapo hujawaweka walionunua hisa za Tsh. mil. 1 ambao ni wengi.
Sasa mwenzenu ameuza hisa zake mil 588 ambazo zilikua ni 17.5% ya total shares, kwanini Major shareholders wasinunue fasta fasta ili waendelee kuongeza Controlling interests.
Inshort nyinyi mnamiliki vijihisa tu wala majority s/holders hawana habari na nyinyi ndio maana hata mkienda pale kwa brokers hamna mtu ana shobo na shares zenu,ila mtu yoyote tajiri mwenye hisa za mabilioni za voda akitaka kuziuza hata leo ni fasta tu.
Ushauri:Muwe mnatafuta kwanza ushauri khs mambo ya hisa kabla hamja yakimbilia kuzinunua.