Bilionea Rostam Aziz amemalizana na Vodacom Tanzania (Auza hisa zote kwa Vodacom SA)

kila kitu ni .majaaliwa na mungu ndio anayempangia.acha roho ya kwanini ukimwona mwenzio kapata mafanikio
ndiomaana huwa hamjaaliwi kutokana na roho zenu za kwann
 
kila kitu ni .majaaliwa na mungu ndio anayempangia.acha roho ya kwanini ukimwona mwenzio kapata mafanikio
ndiomaana huwa hamjaaliwi kutokana na roho zenu za kwann
Ungeanza kumuuliza kwanza babu yako kwanini hajafanikiwa?

Au nae ni kutokana na roho yake ya kwanini?
 
kuna wale walionunua hisa huko vodacom mambo yaliishia wapi
Hata mh. Waziri Mkuu alimnunulia mkewe pia,tuendele kujipa moyo mkuu labda Msipofaidika nazo nyinyi basi hata huko mbeleni wanaweza wakafaidika watoto/wajukuu wenu.

Kwenye hisa kuna aina 2 za kufaidika

1.Kupata dividend/gawiwo

2.Kupata Capital gains(unapouza hisa zako)

So mjiulize wkt mnanunua mlilenga kupata nini kati ya hivyo viwili.
 
Kwa hiyo Rostam kaamua kuwarudishia wa south VODA yao ili CCM wakiitaka Vodacom yao walio pewa na Madiba waifute huko South upya?
 
kila kitu ni .majaaliwa na mungu ndio anayempangia.acha roho ya kwanini ukimwona mwenzio kapata mafanikio
ndiomaana huwa hamjaaliwi kutokana na roho zenu za kwann
Siyo vitu vyoye ni majaliwa kutoka kwa Mungu ,vingine vina mkono wa binaadamu!
 
Halafu haziuziki Rostam kawezaje kuuza? Soko la hisa litoe utafanunuzi kwa Nini hisa zingine Kama hizo za Rostam zinauzika na zingine haziuziki kwa Nini? Waandishi wa habari fuatilieni hilo
Voda Tz walitoa asilimia 25 tu za Hisa zao kuingizwa sokoni Rostam alibaki na zake kama zilizvyo
 
kuna wale tulionunua bila mipango yoyote swala lilikuwa umenunua hisa tu
 
Bado sijaelewa mnunuzi akija sokoni anataka hisa milioni 100 lazima ziwe za Rostam tu au humu ndani haziwezi kuwemo hata Mia mbili za watu wengine? Ina maana Rostam alizipeleka sokoni kuwa nauza na huko sokoni Kuna hisa za watu wengine mnunuzi akija si ananunua hisa anazozikuta sokoni..Fafanua hapo je za Rostam ziliingia sokoni au hazikuingia?
 
kuna wale tulionunua bila mipango yoyote swala lilikuwa umenunua hisa tu
Basi hapo ni kusikilizia gawiwo tu likitoka unavuta chako,maana ukisema uziuze sokoni kwenyewe hakuja kaa vzr.
 
Hapo Tanzania na Magufuli wetu hatupati kitu, Rostam Aziz ni mkwepa kodi mahiri
Conglomerates investment model,Hii ni ngumu sana kujua mmiliki ni nani,.Kama Rastam angalia compuni inayomiliki hisa imasajiliwa Jersey Island.Ukifuatilia tena unakuta ukifuatilia tena Iyo kampuni pia inamilikiwa na kampuni nyingine uko Solomon Island labda..Hdi kujua nani anastahili kulipa kodi ni shughuli,,
 
Wakati Vodacom inaingia Tanzania Rostam hakuwa mweka hazina wa Ccm wala kiongozi wa ngazi yeyote wa chama zaidi ya kuwa mbunge.

Wakti huo pia hisa zake zilikuwa chini ya 20% kabla ya kuwashawishi wenzake akina Noni kumuuzia hisa (maarifa ya biashara na kuona mbali). Kipindi hicho hakuna aliyekuwa anadhani biashara ya mitandao ya simu itakuwa kubwa kiasi hicho.

Mwaka 2013 akauza 17.2% ya hisa zake (maarifa ya biashara - biashara iko juu na hisa zina thamani kubwa sana na kusoma nyakati zinazokuja).

Hivi karibuni kauza nusu iliyobaki kwa 220 million Usd (maarifa ya biashara - ukweli kuwa soko la simu limekuwa na linaelekea kuwa gumu sana kwa sababu ya ushindani)

Nina hakika kama angekuwa na hisa za Safaricom Kenya (ambako imedhibiti soko) asingeuza hisa zake.

Tukubali tukatae, jamaa ana maarifa sana ya biashara. Bila kuwa na maarifa ya kutosha hata uwe mweka hazina wa vyama vyote huwezi kufanikiwa kibiashara kiasi hicho.
 
Pesa huenda kwenye pesa
 
[emoji16][emoji16][emoji16] wanapenda chai Sana ....asilimia 99 wanabackground za kimagumashi tu..tuendelee kupambana kwa njia zetu tu.
 
Hiyo US $ 20M itapelekwa kwenye kufanya figisu za uchaguzi mwakani
Nalog off
 
Kwani Vodacom iliingia nchini mwaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…