Bilionea Warren Buffett: Nikifariki mali zangu wapewe wenye uhitaji

Sasa povu la nini, stress tu zinakusumbua...
stress free is my life style,
umeona povu baada ya kugundua umesapoti wazo la kiwaki, i reveal you to yourself, unaweza gawa urithi ingali uko hai?
acha kwa familia au hata mtoto wako umpendae sembuse kwa wenye uhitaji tena hata usiowajua.
shida wabongo tunadhani matajiri wakizungu hizo mali walishushiwa, au walipewa tu. Watu wanaumiza vichwa na ku sacrifice mambo mengi kama sisi tunavyoumiza miili ila hatusacrifice kitu.
Intellectual wealth you have to sacrifice your comfort zone which include everything that you think its the life to enjoy.
 
nailed it
 
Kwanini urithi?

Kwanini atoe akifa...

Atoe sasa akiwa hai, sehemu fulani kwa hao wahitaji...

Kwa tunaoamini Mungu, tumeambiwa tutoe sadaka kwa wahitaji...

Ikiwa na maana tukiwa hai sio wafu...
 
Safi sana mkuu.. Watu kama nyinyi, sijui kwa nini huwa hampati nafasi za kuongoza baadhi ya mambo.
 
Safi sana mkuu.. Watu kama nyinyi, sijui kwa nini huwa hampati nafasi za kuongoza baadhi ya mambo.
Nashukuru mkuu, unajua kutembea kumenifundisha mengi sana
Nimetembea na kuishi nchi nyingi sana na ninaona binadamu wanavyoishi ila kwa Africa kuamka ni kazi sana inataka dedication
Hebu fikiria mtu anaiba billion za walipa kodi halafu baadhi ya wapuuzi wanasema eti hata mimi nisingeziacha
Sasa hapo unategemea maendeleo kweli
Kwanza ajali yaani wangenipa kazi hapo ningehakikisha miaka 3 ya kwanza 60% ya ajali zingeisha na miaka 5 mngekuwa mnashtuka mkisikia ajali imeuwa kama Ulaya
Najua watahoji HOW?
MAMA anipe kazi tu πŸ˜„
 
Uko sahihi mkuu!

Warren Buffett "hakuuokota" utajiri wake! Aliuhenyea!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wanafurahia kuchezea tope walipokuwa na umri wa miaka saba, Warren yeye alikuwa akisoma vitabu vya biashara na uwekezaji nyumbani kwa Babu yake! Imagine mtoto wa miaka saba kusoma vitabu kama hivyo!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wakiwaza jinsi ya kupata hela ya pipi walipokuwa na umri wa miaka tisaa, yeye alikuwa akifanya biashara ya kuuza magazeti na vizibo vya soda, na hela iliyopatikana, aliiwekeza kwa kufuata mwongozo wa vitabu alivyovisoma.

Mtanzania wa leo mwenye umri wa miaka kumi na sita akipewa milioni moja atafanyia nini? Kufikia huo umri, Warren alikuwa ameshanunua shamba lake binafsi kwa hela yake binafsi aliyoipata baada ya kufanyia kazi maarifa aliyojipatia kwa njia ya vitabu.

Hata alipoanza kupata hela nyingi, bado aliendelea kuwa makini sana na kila senti anayoipata. Ndiyo maana kuna wakati alikuwa na suti moja tu na shati moja jeupe, ambalo mara nyingi lilikuwa likifuliwa kwenye kola tu na pindo za mikononi.

Si kwamba alikuwa hapendi mavazi, hapana. Alikuwa "mbahili" ili aweze kutimiza ndoto zake, na alifanikiwa.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘βœ…πŸ™πŸ™πŸ™

Una "kitu" kizuri sana. Naomba usiishie kwenye huu uzi. Fanya kitu, tafadhaliπŸ™
Nasaidia Kadri ya uwezo wangu na kama ningekuwa huko ningehakikisha hata vijana wangeacha kutupa hela zao kwenye kamari kwani ni addiction
Ulaya sehemu za kamari zote na unapocheza zimeandikwa jihadhari na mchezo huu una madhara, ukiona umedhurika piga namba hii kupata msaada
Huko unaona na uzi kabisa wazee wa kubet tukutane hapa daa

Lazima mjisaidie ukionna kosa rekebisha
Sipendi miziki kwenye mabasi maana sio mahali pake kabisa ila kwa nchi zisizostaarabika ni bonge la ujanja
Kuna wasafiri wamefiwa au wagonjwa, dereva anaweka mziki masaa 10 mpaka anapata ajali kisa kuna vyuma vimeachia ila atasikia wapi mpumbavu huyo kaweka mziki mpaka mwisho

Poleni sana 😒
 
Namfikiria mwanangu wa miaka 8 aliponiomba buku jero, nikamuuliza ya nini akaniambia naenda kununua mfuko wa pipi, nilimwangalia nikamuuliza mfuko wa pipi? Unafanyia nini
Akaniambia naenda kuwauzia watoto shule
Nikamwambia utafika wakati utakuwa na biashara yako na ninakuahidi ila kwa sasa soma pia shule ni marufuku
Sasa anasubiri duka lake πŸ˜„
 
Kwani hana mke, watoto na ndugu wa kugawiwa hizo mali mpaka atake zitapanywe akifa? Kama vipi atafute nchi moja afrika iliyo masikini na wale masikini kabisa hohahe wagawiwe huo utajiri wake.
Hao uliowataja ninaamini washajitafuta wanajiweza na sidhani kama wanasubiri mirathi ili waweze kutoboa.

Mirathi tukomae nayo sisi Waafrika
 
Njoo gombea mkuu! Una kura yangu na ya maelfu ya wana familia ya JF.

Tunataka viongozi wenye "macho" yanayoona.

"Macho" yako yanaona vizuri. Nafasi yako iko wazi. Njoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…